Mambo matano tunaweza kujifunza kutoka kwa sokwe kuhusu siasa

Chimpanzee with fingers in its ears

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanasiasa wa sasa wanaweza kujifunza mambo mawili au matatu kutoka kwa sokwe

Kuna tofauti kati ya siasa zetu na zile za viumbe wengine wanaofanana na binadamu.

Profesa James Tilley amekuwa akifanyia utafiti kile tunaweza kujufunza kisiasa kutoka kwa mivutano ya mamlaka kutoka kwa makundi ya sokwe.

1. Kuwa na uhusiano wa karibu na marafiki lakini pia maadui wawe karibu zaidi

Two chimpanzees, sitting on sand,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwa na uhusiano wa karibu na marafiki lakini pia maadui wawe karibu zaidi

Siasa za sokwe ni miungano inayozidi kubadilika na ikiwa utahitaji kubakia madarakani unahitaji kuwa tayari kuwageuka marafiki na kuwaenzi maadui.

2. Wakati wa kujenga miungano chagua mtu dhaifu badala ya yule aliye na nguvu

Two smiling chimpanzees sitting on a tree with arms crossed

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati wa kujenga miungano chagua mtu dhaifu badala ya yule aliye na nguvu

Sokwe hupanda kuwa na miungano dhaifu.

Hii inamaanisha kuwa sokwe wawili dhaifu watamuunga mkono sokwe mmoja mwenye nguvu.

Ikiwa tutafikiria hivyo basi inaweza kuwa na manufaa.

3. Ni vizuri uogopwe lakini pia ni vizuri zaidi upendwe.

Chimpanzees sitting on a rock

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni vizuri kuwa maaarufu kwenye siasa

Viongozi wa sokwe huogopwa sana na hutawala kwa nguvu, lakini viongozi hawakai siku nyingi.

Kuwa kiongozi mwenye kufanikiwa ni lazima utafute uungwaji mkono kutoka kwa wengi na kuwa mkarimu ndio suluhu.

4. Ni vizuri kupendwa, lakini pia ni vizuri zaidi kutoa vitu kama zawadi

Three chimpanzees sit in a group appearing to have a meeting

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chukua hii rafiki yangu

Viongozi wanaotawala kwa muda mrefu ni wale huchukua mali na kuitumia mali hiyo kununua uungwaji mkono.

5. Vitisho vya nje vinaweza kuchangia uungwaji mkono (ikiwa ni vya kweli...)

Chimpanzee family is sitting in a tree

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati kuna vitisho vya kutoka nje, makundu ya sokwe huja pamoja na kupambana kwa pamoja.

Wakati kuna vitisho vya kutoka nje, makundu ya sokwe huja pamoja na kupambana kwa pamoja.

Isipokuwa hili hufanyika tu kwa binadamu kama kuna tisho lisilotarajiwa kama mashambulizi ya 9/11