Moja kwa moja, Trump atangaza Mlango Bahari wa Hormuz kuwa eneo la Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwa sasa Mlango Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani na Iran inaonekana haiko tayari kufikia makubaliano.

Muhtasari

Trump atangaza Mlango Bahari wa Hormuz kuwa eneo la Marekani

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Raia 13 wa Tunusia hawajulikani walipo baada ya boti lao kuzama bahari ya Mediterenia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Takriban raia 13 wa Tunisia, hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kuzama katika pwani ya Tunisia ikiwa njiani kuelekea Italia, huku watu wawili wakiokolewa.

    Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Mostafa Abdelkebir, mkuu wa shirika la Tunisian Observatory for Human Rights, alisema boti hiyo iliondoka mapema siku ya Alhamisi.

    Mmoja wa manusura hao wawili aliwaambia waokoaji kuwa walikuwa wamekwama baharini kwa saa kadhaa kabla ya chombo chao kupinduka.

    Tunisia ni mojawapo ya maeneo makuu yanayotumiwa na wahamiaji wanaovuka Bahari ya Mediterania, lakini safari hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na operesheni kali dhidi ya uhamiaji na kuimarishwa kwa usalama wa baharini.

    Njia ya katikati ya Bahari ya Mediterania ni mojawapo ya njia hatari zaidi za uhamiaji duniani, inayotumiwa na wahamiaji kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wanaotaka kufika Ulaya, mara nyingi kwa kutumia boti zisizo salama kwa safari za baharini.

  2. Marekani yatangaza ushuru wa 50% kwa bidhaa kutoka Canada

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani imetangaza ushuru wa asilimia 50 kwa baadhi ya bidhaa kutoka Canada, baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kibiashara.

    Ushuru huo, ulioanza kutekelezwa jana usiku, itaathiri bidhaa za Canada zenye thamani ya takribani dola bilioni 20 za Marekani.

    Ushuru huo mpya umeongeza mvutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, na huenda ukalemaza biashara huru kati ya mataifa hayo mawili.

    Carney amesema amesitisha mazungumzo ya kibiashara na Marekani na kwamba Canada italipiza kisasi kwa kuweka ushuru wa thamani sawa, “dola kwa dola,” dhidi ya ushuru huo mpya.

    “Nimeamua kusitisha mazungumzo ya kibiashara na Marekani na nimewaelekeza wajumbe wa Canada wanaoshiriki katika mazungumzo hayo kurejea Ottawa,” alisema Carney.

  3. Mlango Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani - Trump

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Mlango bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani.

    “Kwa sasa natangaza Mlango wa Hormuz kuwa eneo la Marekani.”

    Akifanya kampeni katika jimbo la South Carolina, Trump alisisitiza kuwa hawataruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia.

    Kauli hizo mpya zinakuja wakati Marekani imeongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Iran katika siku za hivi karibuni, huku ikiendelea kuweka kizuizi cha kijeshi katika eneo hilo la bahari.

    Washington inatarajiwa kutangaza siku ya Jumatatu vikwazo vipya dhidi ya Iran. Maafisa wa Marekani wanasema vikwazo hivyo vinaweza pia kuathiri washirika wakuu wa kibiashara wa Iran, ikiwemo China.

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja