Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Habari katika picha:Hii ni Sudan halisi ninayotaka kuionyesha dunia
"Watu huku hawajazoea kumuona mwanamke ameshika kamera na kuzunguka katika mitaa kupiga picha lakini niliamua kuwa napiga picha ya kila nnachopendezewa nacho" mpiga picha Ola Alsheikh aeleza
Kuchekwa,kutokubalika au kudharaulika na watu wasiomjua ndio mambo ambayo Ola anakabiliana nayo kila mara katika mji huo wa Khartoum lakini alikataa kukatishwa tamaa.
"Nataka kuonesha maisha halisi ya Sudan kwa maana tumekuwa tunapewa picha za kusadikika na dunia yote kwa muda mrefu juu ya Sudan"Ola aliongeza.
Hizi ni miongoni mwa picha anazozipenda mpiga picha huyo