Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Villa inavutiwa na Sancho

Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Aston Villa imekuwa klabu ya hivi punde kuonyesha nia ya kumsajili winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, kutoka Manchester United. Sancho amekuwa akiichezea klabu ya Chelsea kwa mkopo.(Team Talk)

Newcastle United imemfanya mlinda lango wa Burnley na England James Trafford, 22, kuwa kipaumbele chao msimu huu wa kiangazi. (Times - usajili unahitajika)

Liverpool haina nia ya kumuuza winga wa Colombia Luis Diaz, 28, na haijapokea ofa, licha ya Barcelona na klabu ya Saudia Al-Nassr kumtaka. (Times - usajili unahitajika)

Liverpool inafikiria kumsajili winga wa Newcastle mwenye thamani ya pauni milioni 80 Anthony Gordon, 24, endapo Diaz ataondoka. (Team Talk)

Liverpool pia huenda akamenyana na Arsenal kumsajili Benjamin Sesko kutoka klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig, huku mshambuliaji huyo wa Slovenia mwenye umri wa miaka 22 akipewa ofa ya pauni milioni 67 na The Gunners. (TBR Football)

Harvey Elliott anapigiwa upatu kujiunga na klabu ya Serie A iwapo kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 22, ataondoka Liverpool msimu huu wa joto. (Football Insider)

Chelsea haiko tayari kulipa kitita cha pauni milioni 25 kunachoitishwa na AC Milan kumuachia mlinda lango wao wa Ufaransa Mike Maignan, 29. (Standard)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Brentford ina nia ya kumsajili kocha wa Ipswich Kieran McKenna ikiwa mkufunzi wa wa sasa Thomas Frank ataamua kurithi mikoba ya Ange Postecoglou katika klabu ya Tottenham. (Football Insider)

West Ham wamewasiliana na Club Brugge kuhusu usajili wa kiungo i wa Nigeria Raphael Onyedika, 24, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan. (TBR Football)

Manchester City na Barcelona wameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Arsenal na Uingereza Max Dowman mwenye umri wa miaka 15. (Football transfers)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi