Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Saudia inavutiwa na kiungo wa Spurs Son

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min analengwa na vilabu vya Saudi Arabia na Spurs wanaweza kuchagua kumnunua Mkorea Kusini mwenye umri wa miaka 32 huku wakitafuta pesa za uhamisho. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Real Sociedad Martin Zubimendi, 26, ametia shaka juu ya kuhamia Arsenal, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania akisema ana "chaguo" na hana uhakika ni wapi ataishia. (Redio Nacional de Espana, via Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Manchester United Jadon Sancho pia anaweza kuelekea Saudi Pro League huku Al-Hilal , Al-Ittihad na Al-Nassr wote wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Mirror)
Mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, anatumai mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki - mara tano ya mshahara wake wa sasa - ikiwa atajiunga na Manchester United . (Time - subcription require)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wameweka mikakati ya kumsajili mlinda mlango wa Ufaransa Mike Maignan, 29, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na AC Milan. (Sport)
Inter Milan wamefanya mawasiliano na meneja wa Como Cesc Fabregas kuhusu kiungo huyo wa zamani wa Uhispania kuchukua nafasi ya meneja wao mpya baada ya kuondoka kwa Simone Inzaghi. (Sky Sports Italia - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 39, amekubali kwa kauli yake kujiunga na AC Milan atakapoondoka Real Madrid baada ya Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa msimu huu wa joto. (Gianluca di Marzio, via Football Italia)
Mmiliki wa sehemu wa Crystal Palace John Textor, ambaye pia anamiliki klabu ya Ufaransa ya Lyon , anajaribu kuuza sehemu yake kubwa katika klabu hiyo huku The Eagles wakijaribu kuepuka kuondolewa kwenye Ligi ya Ulaya msimu ujao kwa kuvunja sheria za Uefa za umiliki wa vilabu vingi. (Mirror)
Mlindalango wa Uingereza Aaron Ramsdale amefanya mazungumzo kuhusu kuhamia West Ham kutoka Southampton, ambao wanatarajia kupata pauni milioni 20 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kufuatia klabu hiyo kushuka daraja kutoka Ligi ya Premia. (Sport)














