Kwanini Matheus Cunha anataka kuhamia Man United, na je, atacheza nafasi gani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matheus Cunha
Muda wa kusoma: Dakika 5

"Nimeweka wazi kwamba ninahitaji kuchukua hatua inayofuata," Matheus Cunha aliiambia The Guardian, mwezi Machi. "Nataka kupigania mataji, kwa mambo makubwa. Nina uwezo."

Mshambulizi huyo wa Brazil sasa anatazamiwa kuchukua hatua hiyo inayofuata lakini inahusisha kubadilisha timu iliyomaliza katika nafasi sita za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu , kwa kuhamia kutoka Wolves hadi Manchester United kwa dau la £62.5m.

Cunha atawasili katika klabu ambayo imemaliza miaka 12 bila kushinda taji la ligi, ikiwa imemaliza msimu mbaya zaidi wa ligi kuu tangu 1973-74, na ambapo morali iko chini kabisa.

Kwa nini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anafurahia kujiunga na kikosi cha United kilichomaliza pointi 42 nyuma ya mabingwa Liverpool?

United 'wana bahati' kumpata Cunha

Wakati Liverpool, Arsenal, Manchester City, Chelsea, Newcastle na Tottenham zote zinapanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, United haiwezi kutoa fursa kwa wachezaji wapya kushiriki katika soka la Ulaya - mbali na nafasi ya kushiriki katika mashindano ya vilabu kuu barani Ulaya.

Hakika, ni zaidi ya miaka mitatu tangu United ilipocheza mara ya mwisho mechi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.

Licha ya kumalizika katika nafasi ya chini katika ligi ya premia na kutoweza kushiriki katika soka la Ulaya msimu ujao, BBC Sport inaelewa kuwa Cunha bado anaitazama United kama klabu kubwa - na kwamba haoni kama hatari.

Badala yake Cunha, ambaye alitimiza umri wa miaka 26 siku ya Jumanne na yuko katika kiwango cha juu, anafurahishwa na changamoto kubwa ya kufufua bahati ya United.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuna hisia kwamba hatua hiyo ni muhimu kwa pande zote.

Cunha anataka kuhamia klabu kubwa zaidi, huku Wolves wakipata zaidi ya pauni milioni 60 kuwekeza tena.

Wakati huo huo, Wolves tayari wameonyesha kuwa wanaweza kushinda mechi bila Cunha baada ya kupata pointi 10 kutokana na mechi nne za Ligi Kuu ya Uingereza alizokosa kwa kufungiwa kufuatia kadi nyekundu dhidi ya Bournemouth kwenye Kombe la FA mwezi Machi.

United, ambao wanatazamiwa kumruhusu fowadi wa Uingereza Marcus Rashford na winga wa Argentina Alejandro Garnacho kuondoka msimu huu wa joto, wanahitaji kuongeza chaguo zilizopo kwa kocha Ruben Amorim.

Kikosi chake kilifanikiwa kufunga mabao 44 pekee ya ligi kuu msimu wa 2024-25 - ikiwa rekodi ya chini ya klabu hiyo katika enzi ya Ligi Kuu. Mshambulizi wa Ipswich Town Liam Delap na mwenzake wa Brentford Bryan Mbeumo wamehusishwa.

Cunha ana mabao 27 katika mechi 65 za Premier League katika misimu miwili iliyopita na anachukuliwa na United kama mtu anayeweza kuleta matokeo ya papo hapo, wakati huohuo akiongeza uzoefu kwenye timu.

"United wana bahati bado wana mvuto wao wa kihistoria na sifa kama klabu, hivyo wachezaji wa ubora na uwezo wa Mbrazil huyo wanataka kuhamia huko," kiungo wa zamani wa Uingereza Fara Williams aliambia BBC Sport.

"Akifanya hivyo, hakuna shaka ataboresha kikosi."

.

Chanzo cha picha, Opta

'Cunha ana kila kitu kinachohitajika na United'

Ubunifu, kasi na umaliziaji mkali - Ustadi wa Cunha na mchezo wake umeleta tofauti katika michezo migumu.

Amekuwa tishio la safu ya mashambulizi ya Wolves, akifunga mabao muhimu, akiunganisha uchezaji na kusumbua mabeki kupitia uchezaji wake wenye ustadi ustadi.

Kwa kuongezea, 2024-25 ilimfanya kufikia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ya mchezaji wa Brazil katika msimu wa Ligi Kuu pamoja na Roberto Firmino (2017-18) na Gabriel Martinelli (2022-23).

"Cunha ana kila kitu ambacho timu ya United ingetaka," aliongeza Williams.

"Huwezi kuhoji sifa alizonazo na tabia aliyonayo ndani ya mchezo katika suala la kutaka kufanya lolote ili kushinda."

Cunha alizungumzia kuhusu kuwacha nyuma nyakati za huzuni alipokuwa Atletico Madrid baada ya kujiunga na Wolves kwa mkopo mwezi Desemba 2022 kabla ya kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu msimu uliofuata.

.

Chanzo cha picha, Opta

Alicheza kwa mara ya kwanza kama nambari tisa huko Wolves lakini wale ambao wamemtazama mara kwa mara katika miaka kadhaa iliyopita wanasema nafasi yake bora ni kucheza nambari 10 ya upande wa kushoto.

Mchezo wake huanza nyuma akiingia katikatika ya uwanja na mpira na nguvu zake ni pamoja na kukimbia mbele ya mabeki na kufunga.

Takwimu zake za 2024-25 zinalingana na zile za Bruno Fernandes, ambaye bila shaka ndiye mchezaji bora wa United.

Cunha alifunga mara sita nje ya eneo la hatari - idadi sawa na Fernandes aliyoweza katika mashindano yote. Cunha pia alisajili majaribio 51 ya kulenga shabaha katika mashindano yote - ikiwa ni idadi sawa na Fernandes.

Hata hivyo, alitumia muda wake mwingi uwanjani akitembea kuliko mchezaji mwingine yeyote wa nje kwenye Premier League msimu huu akiwa na asilimia 77%.

Je, ana tabia ya hasira za karibu?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Vyanzo vingine vya Wolves vitakuwa vinafuatilia kwa karibu jinsi Cunha atakavyokuwa huko United - baadhi katika klabu hiyo wametilia shaka mtazamo wake.

Cunha alimzomea Milos Kerkez wa Bournemouth mara tatu mwezi Machi - akimpiga teke kabla ya kulenga kumpiga kichwa beki huyo wa pembeni wa Hungary aliposimama.

Wiki chache mapema, alifungiwa michezo miwili na Chama cha Soka baada ya kugombana na mfanyikazi wa Ipswich Town na kumpokonya miwani usoni.

Je, tabia ya Cunha imezivunja moyo klabu zitakazocheza Ulaya msimu ujao kumfuatilia?

Vilabu vingine vilifikiria kumnunua mnamo Januari, ikiwa ni pamoja na Arsenal ambao waliamua kutofanya hivyo, huku timu saba bora za Premier League pia zikivutiwa.

Hatahivyo, kulikuwa na chaguzi chache kwa fowadi huyo msimu huu wa joto, huku wengine wakisema kwamba mchezaji huyo alikuwa amesalia na vhaguo la kuichezea United au kuhamia huko Saudi Arabia.

"Kumekuwa na matukio kadhaa msimu huu kuhusu tabia ya Matheus Cunha ambayo yangekushangaza," Rory Smith, mwandishi wa kandanda wa The Observer, alisema mnamo Aprili kwenye kipindi cha The Monday Night Club.

"Tabia ya hasira'', je! ni neno sahihi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matheus Cunha

Hatahivyo, Chris Sutton, ambaye alishinda Ligi ya Premia akiwa na Blackburn Rovers mnamo 1994-95, anapinga hilo.

"Sio swali la kuuliza," alisema kwenye onyesho hilo hilo. "Ni kama kusema usimsajili tena Wayne Rooney."

Williams anaamini kuchanganyikiwa kwa Cunha kumetokana na "kuwa kwenye vita vya kushuka daraja kwa muda mrefu na kucheza pamoja na wachezaji ambao yeye ni bora kuwaliko".

Aliongeza: "Cunha angeleta nguvu kubwa kwa United.

"Ikiwa wangeajiri wachezaji wengine pamoja naye, nadhani usingeona mfadhaiko United hata kidogo.

"Ninampenda sana kama mchezaji na nadhani atamsaidia sana Ruben Amorim."

Imetafsiriwa na Seif Abdalla