Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 30.08.2024


Raheem Sterling amefungiwa nje ya kikosi cha kwanza cha Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raheem Sterling amefungiwa nje ya kikosi cha kwanza cha Chelsea
Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Muingereza Raheem Sterling, 29, au winga wa Bayern Munich Mfaransa Kingsley Coman, 28, baada ya kuombwa kuwanunua wote wawili siku mbili za mwisho za uhamisho. (Independent)

Newcastle wanaelekea kusitisha juhudi za kumsajili mlinzi wa Uingereza Marc Guehi, 24, baada kuchoshwa na mazungumzo ya muda mrefu na Crystal Palace. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Uingereza na Brentford Ivan Toney, 28, anakabiliwa hatari ya kuachwa katika hali ya kutatanisha huku muda wa uhamisho ukizidi kuyoyoma. (Mirror)

 xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Saudi Arabia, Al-Ahli ina matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, 25, katika hatua itakayodidimiza matumaini ya Chelsea kumsajili mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Nigeria. (Sportsport)

Liverpool wamekataa ofa ya pesa taslimu pamoja na mchezaji kutoka Nottingham Forest kwa ajili ya mlinda mlango wao wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 25. (Athletic - musajili unahitajika)

Chelsea wanakaribia kumnunua winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, lakini wamewasilisha masharti yao kwa Manchester United kabla ya kufanya uamuzi huo. (Teamtalk)

Ipswich inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard mwenye umri wa miaka 26 wa Crystal Palace baada ya usajili wa mkopo wa mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 22, kugonga mwamba. (Standard)

Fulham haitamsajili kiungo wa Newcastle mwenye umri wa miaka 30 kutoka Paraguay Miguel Almiron. (Mail)

Beki wa West Ham Mfaransa Kurt Zouma, 29, amekamilisha uchunguzi wa matibabu na anakaribia kukamilisha uhamisho wa awali wa mkopo kwenda kwa Al-Orouba ya Saudi Pro League. (Sky Sports)

Chelsea wamemuuliza beki wa Benfica Mreno Tomas Araujo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)


Kurt Zouma alikuwa nahodha wa West Ham msimu uliopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kurt Zouma alikuwa nahodha wa West Ham msimu uliopita

Kiungo wa Scotland Billy Gilmour, 23, hataweza kuhamia Napoli msimu huu baada ya kiungo mpya wa Brighton Matt O’Riley kuthibitishwa kuwa amepata jeraha baya kwenye mechi yake ya kwanza. (Telegraph - usajili unahitajika)

Brighton wamewasilisha ofa ya pauni milioni 17 kwa Nordsjaelland kumnunua mshambuliaji wao wa miaka 19 raia wa Denmark Conrad Harder.

Leeds United wanakaribia kumsajili beki wa Uswizi Isaac Schmidt, 24, kutoka FC St Gallen. (Sky Sport Germany)

Hull wamewasilisha ofa mpya kwa winga wa Norwich City Muingereza Abu Kamara, 21. (Eastern Daily Press)

Wakati huo huo, Hull wanajaribu kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Jamaica wa Coventry Kasey Palmer, 27, kabla dirisha la uhamisho kufungwa leo Ijumaa. (Coventry Telegraph)

QPR wanajiandaa kumsajili bekiwa Scotland Harrison Ashby, 22, kwa mkopo kutoka Newcastle. (West London Sport)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi