Tetesi za soka Ulaya: Al-Hilal yaanda ofa ya Mo Salah

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mo Salah
Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Saudi, Al-Hilal, iko tayari kumtoa Mohamed Salah, 33 Liverpool na inajiandaa kutuma ofa mwezi Januari (The Sun).

Liverpool tayari wamepanga mbadala wa Salah, mshambuliaji wa Bournemouth, Antoine Semenyo, 25 (The Express).

The Reds pia hawana wasiwasi kuhusu mustakabali wa Salah, ambaye pia anasakwa na klabu ya MLS San Diego (GiveMeSport).

Tottenham wanafuatilia hali ya mkataba wa mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 28 (Football Insider).

Kiungo wa England na Crystal Palace, Adam Wharton, 21, anapanga klabu yake ijayo iwe inayoshiriki Ligi ya Mabingwa, kwa sasa yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na Manchester United (Mirror).

Ederson

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ederson

Liverpool na Barcelona wameambiwa wanaweza kumsajili kiungo wa Brazil, Ederson, 26, kwa pauni milioni 50 kutoka Atalanta mwezi Januari (Football Insider).

Arsenal wako tayari kupambana na Real Madrid katika kumuwania winga wa Uturuki, Kenan Yildiz, 20, ambaye mazungumzo yake ya mkataba na Juventus yamekwama (Goal).

Roma wanaoongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi anayechezea Manchester United, Joshua Zirkzee, 24 (Football Insider).

Newcastle na West Ham ni miongoni mwa vilabu vinavyoopanga kumnasa beki wa Chelsea, Axel Disasi, 27 (Caught Offside).

Manchester United wameamua kutomsaini kiungo wa Senegal mwenye umri wa miaka 17, Mouhamed Dabo, licha ya kutafuta wachezaji wa kuongeza ubora katikati ya uwanja (MEN).