Tetesi za soka Ulaya: PSG inamtaka Rashford

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Paris St-Germain wanaweza kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Bradley Barcola, mwenye miaka 23, kwenda Manchester United kama sehemu ya dili la kubadilishana na Marcus Rashford, 28, ambaye kwa sasa yuko Barcelona kwa mkopo. (Football Insider)

Beki wa Hispania Sergio Reguilon, 28, ambaye aliondoka Tottenham majira ya kiangazi, yuko karibu kutua Inter Miami ya Lionel Messi. (Marca)

Manchester United wamekataa ombi la awali la Roma kutaka kumsajili mshambuliaji Joshua Zirkzee, 24, kwa mkopo unaolazimisha kumnunua moja kwa moja baadaye. (Corriere dello Sport)

United wenyewe wako tayari kumuuza Zirkzee kwa uhamisho wa kudumu tu ili waweze kutumia fedha hizo katika dirisha la Januari. (Metro)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wako tayari kutoa ofa kwa kiungo wa Lille, Ayyoub Bouaddi, mwenye miaka 18. (RMC Sport, via Teamtalk)

Liverpool wako tayari kukubali dau la karibu £15m kumuuza beki Ibrahima Konate, 26, iwapo watapata mbadala. (Football Insider)

Hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya klabu za Saudi Arabia na Liverpool kuhusu mshambuliaji Mohamed Salah, 33. (Fabrizio Romano)

Tottenham wamearifiwa kuwa mshambuliaji wa Porto, Samu Aghehowa, 21, hataki kuondoka Januari. (Teamtalk)

Manchester United wanaweza kumkosa kiungo chipukizi wa Ugiriki Christos Mouzakitis, 18, ambaye anapendelea kujiunga na Real Madrid. (Football Insider)