Tetesi za soka Ulaya: Klabu 12 zinamtaka Mainoo

Kobbie Mainoo,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kobbie Mainoo
Muda wa kusoma: Dakika 1

England midfielder Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 20, atakuwa na nafasi ya kuchagua kati ya klabu angalau 12 iwapo Manchester United watamruhusu aondoke kwa mkopo Januari. (Mail)

Nottingham Forest wanatarajiwa kuongeza ada yao ya £100m kwa kiungo wa England Elliot Anderson, mwenye umri wa miaka 23, majira ya kiangazi yajayo. (Football Insider)

Kuna imani kubwa kwamba klabu kutoka Saudi Pro League itaweza kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 33, kutoka Liverpool Januari kwa ada ya bei nafuu. (The i Paper)

Lyon wako kwenye mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Ufaransa wa Chelsea Axel Disasi, 27, Januari. (L'Equipe)

Crystal Palace wanaendelea kumfuatilia beki wa kati wa Kiingereza Max Kilman, 28, wa West Ham. (Football Insider)

mO

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mo Salah

Everton na West Ham wamefanya mawasiliano ya awali kuhusu mshambuliaji wa Brazil Yuri Alberto, 24, anayekipiga Corinthians. (Teamtalk)

Flamengo wanapanga kumsajili winga wa Colombia Jhon Arias, 28, ambaye alijiunga na Wolves mwezi Julai. (Ekrem Konur)

Manchester United na Tottenham ni miongoni mwa klabu za England zilizoulizia upatikanaji wa mshambuliaji wa Ecuador Nilson Angulo, 22, anayechezea Anderlecht. (Teamtalk)

Mchezaji wa Lille Ayyoub Bouaddi anasakwa na klabu kadhaa za Ulaya, huku Arsenal wakiwa wanaoongoza katika mbio za kumsajili kiungo huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 18. (RMC Sport)