Tetesi za soka Ijumaa: Salah huenda akaelekea Saudia

Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Ligi Kuu ya Saudia bado iko katika nafasi ya kufadhili uhamisho wa Mohamed Salah endapo mshambuliaji huyo wa Misri, mwenye umri wa miaka 33, ataamua kuondoka Liverpool. (Telegraph)

Vigogo wa Uturuki, Galatasaray, wanapanga kumshawishi Salah kwa mkataba wa thamani ya kati ya pauni milioni 15 hadi 16.5 kwa msimu. (Fichajes)

Real Madrid watamenyana na Manchester United kuwania saini ya kiungo wa Olympiakos na Ugiriki, Christos Mouzakitis, mwenye miaka 18. (Sun)

 Christos Mouzakitis

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wanaweza kutoa ofa ya pauni milioni 40 kumsajili mlinzi wa Brighton raia wa Uholanzi, Jan Paul van Hecke, mwenye umri wa miaka 25. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, ameijulisha Crystal Palace kuwa anataka kutazama uwezekano wa kuondoka mapema Januari. (Teamtalk)

Leeds wanavutiwa kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Mexico, Santiago Gimenez, 24, mwezi Januari. (Fichajes)

Wolves watamruhusu kiungo wa Uhispania Fer Lopez, mwenye miaka 21, kuondoka kwa mkopo Januari baada ya kupata nafasi ndogo ya kucheza. (Fabrizio Romano)

Fer Lopez

Chanzo cha picha, Getty Images

Brighton wanamfuatilia kiungo wa Aston Villa raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 21, Lamare Bogarde. (Telegraph)

Newcastle wanamnyatia kiungo wa Palmeiras raia wa Brazil, Allan Elias, mwenye miaka 21. (Goal)

Arsenal wamekuwa wakimchunguza kiungo wa Elche na timu ya taifa ya vijana ya Uhispania chini ya miaka 21, Rodrigo Mendoza, mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)

Chelsea wanafanyia kazi dili la kumsaini kiungo kinda wa SF Cascades na Burkina Faso, Mohamed Zongo, 16, licha ya ushindani kutoka Manchester City na Manchester United. (Mail)