'Je, huu ndio mwanzo wa maisha ya Liverpool bila Salah?'

Chanzo cha picha, Getty Images
Mohamed Salah ana historia katika Uwanja wa London Stadium, na hii inaweza kuwa siku ambayo Liverpool walianza kuandika sura mpya kwa kuwa na kizazi kijacho bila yeye katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham.
Kocha mkuu Arne Slot alimuweka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kwenye benchi kwa mechi ya Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2024 - pia akiwa West Ham, uamuzi huo ukichukuliwa na mtangulizi wa Mholanzi huyo Jurgen Klopp.
Hiyo ilikuwa ni siku ambayo Salah aligonga vichwa vya habari.
Kwanza alipohusika katika mzozo na Klopp wakati West Ham wakifunga bao aliposubiri kuingia kama mchezaji wa akiba katika sare ya 2-2, na kisha mshambuliaji huyo ambaye alikuwa msumbufu alipowapita waandishi baadaye na kutangaza: "Nikizungumza kutakuwa na moto."
Hapa, uteuzi wa Slot ulikuwa na umuhimu mkubwa zaidi, sio kuonyesha mwanzo wa mwisho wa Salah katika uwanja wa Anfield bali kuonyesha jinsi mageuzi ya meneja huyo ya pauni milioni 450 katika majira ya joyto yanaweza kuzaa matunda bila Mmisri huyo mashuhuri.
Slot amehimizwa hadharani, haswa na nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney, kumtoa Salah kufuatia msururu wa kiwango cha chini cha mchezo msimu huu.
Hii ndiyo sehemu rahisi - sehemu ngumu ni jinsi ya kuchukua fursa ya kumbadilisha mchezaji huyo mwenye talanta ya kiwango cha kimataifa, ambaye ni wa tatu katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu hiyo akiwa nyuma ya Ian Rush na Roger Hunt.
Hapa, Slot alitoa jibu lenye mwafaka.
Muundo wa sura mpya ya Liverpool ulileta matokeo ambayo yeye na timu yake walihitaji sana, baada ya kushindwa kwa mara tisa katika mechi 12 zilizopita, na sita kati ya saba kwenye ligi.
Na, ili kuongeza furaha kwa Slot, ushindi huo ulijiri baada ya Alexander Isak kufunga bao lake la kwanza la ligi tangu rekodi yake ya Uingereza ya £125m kuhama kutoka Newcastle United, na kwa £116m Florian Wirtz akionyesha mchezo mzuri ambao ulisababisha ushindi huo muhimu.

Chanzo cha picha, GETTY
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Chaguo la Slot lilizaa matunda , huku Dominik Szoboszlai akiondolewa majukumu ya beki wa kulia, ambapo anatumika vibaya akipelekwa upande wa kulia katika safu ya mashambulizi, huku naye Cody Gakpo akiwa kushoto na Isak kama mshambuliaji mkuu.
Mholanzi Gakpo alicheza vyema na mpira wa krosi kwa bao la Isak, kisha akamaliza dakika za lala salama kwa bao la pili.
Slot pia alimtumia Joe Gomez katika nafasi ya beki wa kulia - ikiwa ni mara ya kwanza katika ligi baada ya miezi 11 - hatua iliomuondolea vikwazo Szoboszlai, na kuimarisha safu ya ulinzi ya Liverpool kwa bao safi baada ya kuruhusu mabao 10 katika mechi tatu.
Kuhusu Salah, ambaye hivi karibuni atashiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, alitazama mechi hiyo kutoka benchi.
Slot alikuwa na uchungu kuashiria fowadi huyo - ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka miwili msimu wa joto - "atakuwa na mustakabali mzuri sana katika klabu hii kwa sababu ni mchezaji maalum".
Lakini kulingana na kiwango chake msimu huu, Salah ameingia kwenye hatari ya kuachwa.
Alan Shearer aliiambia BBC Sport: "ulikuwa uamuzi mgumu kutoka kwa Slot, lakini nadhani umerahisishwa na matokeo ya Liverpool.
"Wakati mambo hayaendi sawa kwako, lazima ufanye maamuzi makubwa - na hilo lilikuwa kubwa kwa sababu ya kile ilichofanya Liverpool hapo awali.
"Lakini Salah hawezi kulalamika kwa sababu amekuwa hachezi vizuri, na inapotokea hivyo basi lazima ukubali uamuzi.
"Umefanya kazi kwa Liverpool, na umefanya kazi kwa Isak, kwa sababu alikuwa tofauti."

Chanzo cha picha, Getty Images
Salah hapaswi kusahaulika. Huo ni mchezo hatari.
Alikuwa ameanza mechi 53 za Premier League mfululizo kabla ya hii, mara nyingi alionekana kuwa na jukumu la pekee la kurudisha taji kwa Liverpool msimu uliopita, hatua ambayo hatimaye ilifanikiwa.
Salah ameichezea Liverpool mechi 419 akianzishwa mara 383 na kufunga mara 250. Amecheza mechi 300 za ligi, na alianza mara 288, tangu kuhamishwa kwake kutoka Roma msimu wa joto wa 2017, akifunga mabao 188 na asilimia ya ushindi ya 64%.
Katika mashindano yote, Liverpool wameshinda michezo 263 wakati Salah amecheza - ukiwa ushindi wa 63%.
Kipaji chake hakiwezi kupuuzwa, lakini pia Slot hangefanya kazi yake kama hangeangalia maisha ya Liverpool zaidi ya Salah - na ushindi wa Jumapili ulitoa dalili.
Itakuwa jambo la kushangaza kuona kama Slot atamrudisha Salah dhidi ya Sunderland kwenye Uwanja wa Anfield siku ya Jumatano.
Akiwa amefunga dhidi ya Southampton kwenye Kombe la Carabao mnamo Septemba, imani ya Isak utaimarishwa na bao hilo kumaliza ukame wa mabao wa dakika 310 katika mechi yake ya sita.
Wirtz, pia, alionyesha baadhi ya dalili za mchezo mzuri wakati mchezaji huyo wa Kijerumani mwenye umri wa miaka 22 alipowasili Liverpool akionesha mchezo mzuri.
"Nimekuwa nikingojea na nikifuatilia bao hili na wakati mwingine inachukua muda mrefu kuliko unavyotarajia, lakini nina furaha kufunga bao na kusaidia kuelekea ushindi," Isak aliiambia Match of the Day.
"Siyo rahisi kamwe. Kama mshambuliaji unahitaji kasi. Wakati mwingine unapitia matatizo haya, lakini tunatumai hii itasaidia kujenga kiwango kizuri. Tuliweka ulinzi mzuri na kufunga mara mbili"
Kwa Liverpool na Slot, hii yote ilihusu ushindi huo - ukiwa ni wa pili kwenye ligi tangu walipoifunga Everton 2-1 mnamo 20 Septemba.
Kwa kuwa bao hilo lilifungwa na mchezaji waliyemnunua bei ghali wakati wa majira ya kiangazi, inaonyesha kwamba kiwango bora cha Liverpool kitasaidia kupunguza shinikizo kuhusu mustakabali wa Mholanzi huyo.















