'Nikikuona, nitakuua': Jamii ya Waarabu wa Israeli iliyonaswa katikati ya vita

- Author, Feras Kilani
- Nafasi, BBC Arabic
- Akiripoti kutoka, Rahat, southern Israel
Simu ya Ata Abu Madighem haiachi kukereza.
Lakini simu si za kumjulia hali -- zote ni vitisho vya kifo.
“Nikikuona, nitakuua,” mwanamume mmoja anapaza sauti.
Madighem anatoka katika jamii ya Wabeduin Waarabu 200,000 wenye nguvu nchini Israel, ambao pia ni Waislamu. Walipoteza watu 16 katika shambulio la Hamas.
Yeye ndiye meya wa Rahat katika jangwa la Negev, jiji kuu la Bedouin.
"Simu hizi zinatoka Ukingo wa Magharibi na kutoka Gaza," ananiambia, simu yake ya mkononi ikiita bila kukoma mfukoni mwake.
Mtu fulani ameshiriki nambari yake ya simu kwa nia mbaya kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati fulani anajaribu kujadiliana na mtu aliye upande mwingine wa mstari, na wakati mwngine , anapiga kelele ili kufikisha ujumbe wake.
Haijafaulu kwani Madighem anatuhumiwa kuwakabidhi wapiganaji wa Hamas kwa mamlaka ya Israel.
"Wanasema kwamba wao [wapiganaji wa Hamas] waliuawa huko Rahat. Hakuna mtu [wapiganaji wa Hamas] aliyeuawa huko Rahat. Yote ni uwongo, "anasema.

Uhusiano kati ya Wabeduin wa Kiarabu na serikali ya Israel unazua mvutano mkubwa na jamii ya Wapalestina.
Baadhi ya Wabeduin wa Kiarabu wanahudumu katika jeshi na vikosi vingine vya usalama, jambo ambalo linawakasirisha baadhi ya Wapalestina.
Lakini jumuiya hiyo pia inasema wanabaguliwa na taifa la Israel.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Fuatilia moja kwa moja:Matukio ya hivi punde na kinachoendelea
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
Waathiriwa wa shambulio hilo
Watu saba kutoka eneo karibu na Rahat katika jangwa la Negev hawapo.
Familia zao zinaamini kuwa wamepelekwa Gaza na wanashikiliwa mateka na Hamas. Hawatazungumza hadharani kwa kuogopa jamaa zao wanaweza kuuawa.
Dham AlZiadna alisaidia kusafirisha baadhi ya miili ya wafu kurudi kwa familia zao.
Alisema mashambulizi hayakuwalenga hasa Waarabu wa Bedouin lakini wametekwa katikati yake.
"Yeyote anayetaka kutoka na kufanya hivi anajua anachofanya," alisema.

Chanzo cha picha, Family handout
Abdel Rahman AlZiadna kutoka Rahat aliuawa na Hamas alipokuwa katika safari ya kupiga kambi pwani, kilomita 3 tu kutoka mpaka wa Gaza. Alikuwa na umri wa miaka 26.
Baba yake Aatef ana huzuni sana kuweza kuongea. Ilikuwa ni kaka wa baba ambaye alilazimika kutoa habari hiyo.
“Mungu atakufidia,” Adam alimwambia kaka yake Aatef.
"Alizirai," Adam aliongeza. "Mtu anawezaje kukabiliana na wakati kama huu?"

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kamanda mkuu wa zamani wa Jeshi la Ulinzi la Israeli, Yair Golan, alifika kuzungumza na familia.
Alisema alikuwepo kutoa rambirambi zake lakini ziara yake ikawa kitovu cha hasira dhidi ya mamlaka ya Israel.
“Tulikula upumbavu katika vita hivi,” mwanamume mmoja alifoka. "Ninazungumza kwa ajili ya Wabedui wote. Ni aibu kwa serikali na wizara.”
Waarabu wa Bedouin wanahisi kuwa vifo katika jamii yao havijakubaliwa katika kuripoti kwa mapana kuhusu shambulio la Hamas dhidi ya Israel.
Na kihistoria, mamlaka za Israel mara nyingi zinashutumiwa kwa kushindwa kuweka viunganishi vya maji na umeme kwa Waarabu wa Bedouin, hasa katika "vijiji visivyotambulika" ambavyo serikali inasema vilijengwa kinyume cha sheria.
Nje ya maeneo hayo, wengi wa jamii wanaishi katika miji masikini.
"Shambulio hili la kigaidi halikutofautisha kati ya Waarabu, Beduin na Wayahudi," Golan ananiambia baada ya kuzungumza na familia ya AlZiadna.
"Waliua kila mtu."
Alipoulizwa kwa nini jamii ilikasirishwa sana na mamlaka, alikubali kwamba mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kuboresha uchumi.
"Tunapaswa kujenga mustakabali wa pamoja," Golan aliongeza.

Lakini ndoto hii inaonekana kuwa mbali kufuatia shambulio la Hamas.
Nilimsikia mtu mmoja wa Bedouin akisema aliogopa kutembea barabarani, akiwaogopa Wapalestina na Wayahudi wa Israeli.
Tangu shambulio hilo, serikali ya Israeli inajaribu kukuza wazo kwamba Waisraeli na Bedouin wana adui wa pamoja katika Hamas.
Lakini Beduin wanahisi wamebanwa kati ya pande hizo mbili.












