Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina

Bendera ya Israel na kitambaa cha Palestinian

Chanzo cha picha, Getty Images

Miaka hamsini baada ya Vita vya Yom Kippur, vilivyoanza kwa shambulio la ghafla dhidi ya Israel na Misri na Syria, wanamgambo wa Kipalestina wametekeleza mashambulizi mengine makubwa.

Hili pia halikutarajiwa kufanyika wakati wa sherehe nyengine ya Kiyahudi.

Mvutano ulikuwa umeongezeka hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza, lakini hekima iliyozoeleka ni kwamba si Hamas, kundi la Kiislamu linalotawala huko, wala Israel na badala yake, Hamas imekuwa ikipanga operesheni kali dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Lakini mgogoro huu ulianza lini na kipi chanzo chake?

Ijapokuwa taifa la Israel halipo katika bara Ulaya, limeshiriki katika michezo ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 45.

Lakini kumekuwa na wito wa kutohudhuria ghafla hiyo kutoka kwa wakosoaji wa Israel kutokana na sera yake dhidi ya Palestina katika eneo la Gaza.

Mgogoro kati ya Israel na Palestina umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa na swala la umiliki wa ardhi ndio limetajwa kuwa nyeti.

Je mzozo huo ulianzaje?

Mji wa Bethlehem mapema katika karne ya 20th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mji wa Bethlehem mapema katika karne ya 20th

Ni mzozo uliokuwepo kwa takriban miaka 100 sasa

Uingereza ilichukua na kudhibiti eneo linalojulikana kama Palestine baada ya mtawala wa eneo hilo la mashariki ya kati mfalme wa Ottoman kushindwa katika vita vya duniani vya kwanza.

Ardhi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Wayahudi walio wachache na Waarabu walio wengi.

Uhasama baina ya makundi hayo mawili ulianza wakati jamii ya kimataifa ilipoipatia Uingereza jukumu la kuwapatia makaazi Wayahudi katika eneo la Wapalestina.

Kwa upande wa Wayahudi eneo hilo lilikuwa la mababu zao, lakini Waarabu Wapalestina pia nao walidai kumiliki ardhi hiyo na hivyobasi wakapinga mpango huo.

Mpiganaji wa Israel kwa jina haganah kabla ya kuanza kwa vita vya uhuru wa Israel 1948

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mpiganaji wa Israel kwa jina haganah kabla ya kuanza kwa vita vya uhuru wa Israel 1948

Kati ya mwaka 1920 na miaka ya 40, Idadi ya Wayahudi iliowasili katika eneo hilo iliongezeka, huku wengi wakitoroka kuuawa barani Ulaya na kutafuta eneo la kuishi baada ya mauaji ya Holocaust ya vita vya dunia vya WWII.

Ghasia kati ya Wayahudi na waarabu na dhidi ya utawala wa Uingereza ziliongezeka.

Mwaka 1947, Umoja wa Mataifa ulipiga kura kwa Palestina kugawanywa kati ya mataifa ya Wayahudi na Wapalestina huku mji wa Jerusalem ukiwa mji wa kimataifa.

Mpango huo ulikubaliwa na Wayahudi lakini ukakataliwa na Waarabu na haukutekelezwa.

Wanajeshi wa Kiarabu wakiwashambulia wapiganajai wa Kiyahudi wa Haganah 1948

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Kiarabu wakiwashambulia wapiganajai wa Kiyahudi wa Haganah 1948

Uanzishaji wa taifa la Israeli na 'changamoto' zake

Mwaka 1984 ,baada ya kishindwa kutatua mzozo huo , watawala wa Uingereza waliondoka na viongozi wa Kiyahudi wakatangaza uanzishwaji wa tiafa la Israel.

Wapalestina wengi walipinga na vitaa vikaanza.

Wanajeshi kutoka mataifa jirani ya Kiarabu walivamia. Mamia ya maelfu ya raia wa Kipalestina walitoroka ama kulazimishwa kutoka katika makaazi yao kwa kile walichokiita Al Nakba aua 'janga'.

Wakati vita vilipoisha mwaka uliofuata , Israel ilikuwa ikidhibiti eneo kubwa.

Jordan iliteka aradhi iliojulikana baadaye kama West Bank huku Misri ikilinyakua eneo la Gaza.

Jerusalem iligawanywa kati ya wanajeshi wa Israel waliopo magharibi na wanajeshi wa Jordan waliopo mashariki.

kwa kuwa hakukuwepo kwa mkataba wa amani - kila upande ulilaumu mwengine - kulikuwa na vita zaidi kwa miongo kadhaa.

Ramani ilivyo hii leo

A map of Israel and the Palestinian territories
Presentational white space

Katika vita vyengine 1967, Israel ililiteka eneo la mashariki mwa Jerusalem na lile la West Bank pamoja na eneo kubwa la milima ya Golan iliopo Syria , Gaza na rasi ya Sinai iliopo Misri.

Wakimbizi wengi wa Palestina wanaishi katika eneo la Gaza na West Bank pamoja na mataifa jirani ya Jordan, Syria na Lebanon.

Wao na wajukuu wao hawakuruhusiwa na Israel kurudi katika makaazi yao-Israel inasema kuwa hatua hiyo itaizidi nchi hiyo na kutishia uwepo wake kama taifa la Wayahudi.

Makamanda wa jeshi la Israel wawawili mashariki mwa Jerusalem wakati wa vita vya siku sita 1967

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makamanda wa jeshi la Israel wawawili mashariki mwa Jerusalem wakati wa vita vya siku sita 1967

Israel bado inasalia kulidhibiti eneo la West Bank, na ijapokuwa iliondoka katika ukanda wa Gaza Umoja wa mataifa unalitambua eneo hilo kama eneo lililotekwa.

Israel inadai kumiliki Jerusalem kama mji mkuu wa Israel huku Palestina ikidai kuwa Jerusalem ya mashariki ndio itakayokuwa mji wake mkuu wa taifa lijalo la Kipalestina.

Ni Marekani pekee inayotambua kwamba Jerusalem ni eneo la Israel . katika kipindi cha miaka 50 iliopita , Israel imekuwa ikijenga makaazi katika maeneo hayo ambapo takriban raia 600,000 wa Kiyahudi wanaishi.

Palestina inasema kuwa makaazi hayo ni haramu na kinyume na sheria ya kimataifa na kikwazo cha kuleta amani , lakini Israel imekana hilo.

Ni nini kinachoendelea?

Mkaazi wa Palestina na mwenzake wa Israel wakikaripiana

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali ya wasiwasi ipo juu kati ya raia Israel na Wapalestina wanaoishi mashariki mwa Jerusalem, katika eneo la Gaza na lile la West Bank.

Gaza inatawaliwa na kundi la wapiganaji wa Kipalestina kwa jina Hamas, ambalo lilipigana na Israel mara nyingi.

Israel na Misri wanadhibiti eneo la mpakani la Gaza ili kuzuia silaha kusafirishwa hadi kwa wapiganaji wa Hamas.

Raia wa Palestina wanaoishi Gaza pamoja na West Bank wanasema kuwa wanateseka kutokana na vitendo vya Israel na vikwazo.

Israel nayo inasema kuwa inbatekeleza vitendo hivyo ili kujilinda dhidi ya ghasia za palestina. Kwa kipindi cha mwaka mmoja kilichopita, kumekuwa na ghasia katika mpaka wa Gaza na Israel.

Raia wa Palestina wamekuwa wakifanya maandamano , wakiwataka wakimbizi kurudi katika makaazi yao katika eneo ambalo sasa ni la Israel.

Israel inasema kuwa waandamanaji hao wanatumika kama ngao ili kuwashambulia.

Makumi ya raia wa Kipalestina wameuawa na wanajeshi wa Israel ambao wanasema wanachukua hatua hiyo kujilinda.

Vitoa machozi vyarusha dhidi ya waandamanaji karibu na mpaka kati ya ukanda wa Gaza na Israel.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vitoa machozi vyarusha dhidi ya waandamanaji karibu na mpaka kati ya ukanda wa Gaza na Israel.

Lakini matatizo ni yapi?

Kuna maswala kadhaa ambayo Israel na Palestina hawawezi kukubaliana.

Maswala hayo yanashirikisha maswali kama vile ni nini hatma ya wakimbizi wa Palestina, Iwapo makaazi ya Wayahudi ya West bank yanafaa kuondolewa ama yaachwe , iwapo wawili hao wanafaa kutumia kwa pamoja mji wa Jerusalem na pengine kubwa zaidi ni iwapo taifa la Palestina linafaa kutengezwa pamoja na lile la Israel.

Mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika kwa zaidi ya miaka 25 sasa , lakini kufikia sasa hakuna suluhu ya mzozo huo.

Je hatma ya mzozo huo ni upi?

Hakuna anayejua kilicho ndani yake , lakini Marekani inasema kuwa huenda ikautangaza mpango huo mnamo mwezi Mei ama Juni 2019.

Chanzo cha picha, Reuters

Kwa ufupi, hali hiyo haiwezi kutatuliwa hivi karibuni.

Mpango mpya wa amani unaandaliwa na Marekani ambayo imeutaja kuwa mpango muzri wa karne hii.

Hakuna anayejua kilicho ndani yake , lakini Marekani inasema kuwa huenda ikautangaza mpango huo mnamo mwezi Mei ama Juni 2019.

Hatahivyo Wapalestina wanasema kuwa Marekani inaipendelea Israel na kwamba hawatakubali mpango wowote utakaoandaliwa na Marekani.

Israel imesema kuwa itasubiri kuona ni mpango gani.

Iwapo mpango huo utafanikiwa , uatamaliza mojawapo ya mizozo mikubwa zaidi duniani. Lakini iwapo itashindwa vita vitaendelea.

line