Je, Marekani na Iran zinakaribia kukabiliana kivita?

Chanzo cha picha, AFP
Kuna nadharia mbili kuu zinzaokinzana juu ya mgogoro unaoendelea baina ya Marekani na Iran
Nadharia ya kwanza, ambayo inapigiwa chapuo na uongozi wa rais wa Marekani Donald Trump, ni kuwa Iran ni taifa la kuaminika na wana nia ovu ya kuhatarisha usalama wa Mashariki ya Kati. Uongozi huo unadai kuwa Iran inajipanga pia kushambulia maslahi na maeneo ya Wamarekani, japo ushahidi mchache kuthibitisha hilo umetolewa hadhararni.
Marekani tayari imeshapeleka zana kali za kijeshi katika ukanda wa mashariki ya kati; pia imepunguza wafanyakazi wake wasio na umuhimu sana katika ubalozi wake wa Iraq. Yote hayo yanaonekana kuwa ni maandalizi ya vita.
Ujumbe unaotumwa na Marekani kwenda Iran ni kuwa: shambulio lolote kwa maslahi ya Wamarekani au washirika wake kutoka kwa Iran ama washirika wake kutajibiwa na mashambulizi makali zaidi ya kijeshi kutoka Marekani.
Nadharia ya pili inailaumu moja kwa moja Marekani juu ya mgogoro wote unaoendelea.
Iran - bila ya mshangao - ndiyo kinara inayopigia chapuo nadharia hii, lakini pia kuna wapinzani wa Trump ndani ya Marekani wanaoamini kuwa uongozi wa nchi hiyo ndio wakulaumiwa.
Mawazo kama hayo pia japo si kwa uzito sawa pia yanaaminiwa na baadhi ya washirika wa Marekani barani Ulaya.
Kwamujibu wa nadharia hiyo, wakosoaji wa Iran ndani ya utawala wa Trump, watu kama Mshauri wa Masuala ya Usalama John Bolton au Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo wamepata fursa ya kushambulia.
Lengo la viongozi hao, kwa mujibu wa wanandharia ni kubadili uongozi wa Iran, na kama vikwazo vya kiuchumi havifui dafu katika kutekeleza hilo, basi njia ya kijeshi inaweza kutumika.

Chanzo cha picha, AFP
Nadharia hizi mbili zinaakisi tafsiri mbili tofauti juu ya mgogoro uliopo na unaoendelea kukua. Tafsiri hizo zinatumika na kila upande katika kujieleza na kujaribu kutafuta uhalali wa kile ufanyacho
Lakini tafsiri hizo ni za muhimu kama ilivyo kwa ukweli wa mambo, na wakati mwengine, tafsiri hizo ndio huwa uhalisia wenyewe wa kinachoendelea.
Na ukweli ni kuwa, mapambano baina ya Iran na Marekani - iwe kwa bahati mbaya ama kwa makusudi - yananukia kuliko kipindi kingine chochote toka Donald Trump alipochukua hatamu za uongozi Marekani.
Hofu pia zinapanda katika ukanda wote wa Mashariki ya Kati.
Iran, ambayo uchumi wake unapitia kipindi kigumu baada ya kurudishwa kwa vikwazo vya kiuchumi baada ya kuvunjika kwa Mkataba wa Silaha za Nyuklia, inafurukuta kubaki salama.
Nchi hiyo imesema haitakuwa tayari kuendelea kukubali vikwazo juu ya matumizi yake ya nyuklia.

Chanzo cha picha, AFP
Kuchaguliwa kwa Trump Madarakani ndio kulikobadili kila kitu.
Trump aliitoa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia mwaka mmoja uliopita, na kuazisha sera ya kuibana Iran kwa kila namna.
Iran kwa sasa imechoshwa na kuminywa huko. Inawalazimisha mataifa ya Ulaya kuusaidia uchumi wake unaoyumba au la ikitishia kukiuka makubaliano ya mkataba wa nyuklia.
Lakini tishio hilo la Iran linasubiriwa kwa hamu na uongozi wa Trump.

Chanzo cha picha, AFP
Mustakabali wa kitakachotokea baadae kwa kiasi kikubwa unategemeana na mipango ya uongozi wa Trump na kwa jinsi gani Iran wanaliangalia suala hilo.
Trump anajaribu kupuuzia taarifa kuwa maafisa wake wakuu wanatofautiana juu ya nini kifanyike kwa Iran, na kuna ripoti kuwa hataki vita.
Msimamo wake dhidi ya vita unajulikana vyema. Lakini ni dhahiri kuwa hatorudi nyuma endapo wananjeshi ama zana za Marekani zitashambuliwa.
Lakini Irana wanaweza wakawa na mpango mwengine, mathalan kuwachonganisha Bolton na Trump ili mshauri huyo aonekana ni mtaka vita na aangushwe.
Kama Iran wataamua kufanya hivyo inaweza kuwaletea matatizo makubwa.

Chanzo cha picha, EPA
Japo washirika wakuu wa Marekani katika ukanda wa Mashariki ya Kati - Israeli na Saudi Arabia - yawezekana wakawa wanafurahia jinsi mambo yanavokwenda, washirika wa bara Ulaya wana mawazo tofauti kabisa.
Uhispania, Ujerumani na Uholanzi wote wameyaondoa majeshi yao katika eneo hilo ambao walikuwa wakisaidiana na Marekani kutokana na mgogoro unaoendelea.
Endapo mgogoro huu utazaa vita, basi itakuwa ni vita ya kipekee ambayo haitalingana kabisa na ile ya Iraq mwaka 2003.
Vita hiyo itapiganwa zaidi majini na angani, huku Iran ikitarajiwa kujibu mapigo kwa nguvu zote, hali itakayotishia usalama wa ukanda mzima.

Chanzo cha picha, Reuters
Kuna wale waliotabiri kwamba kutakuwa na janga kuu katika sera ya kigeni ya bwana Trump wakati alipochukua mamlaka. Badala yake kumekuwepo na migogoro kutoka pande mbalimbali na ule wa Iran ni mmojawapo tu.
Kutojali mikataba ya kimataifa kuwategemea sana washirika wake walio na aganeda zao , kumeongezeka hali ya wasisi kati yake na washirika wake wa muda mrefu katika shirika la NATO, na zaidi ni hatua ya taifa hilo kushindwa kuchagua malengo na mahitaji yake.
Huku kukiwa na ushindani mkubwa wa kiuwezo, wakati Marekani inatafuta kuimarisha jeshi lake ili kukabiliana na ushindani mkubwa wa China na Urusi, je Iran inajipata wapi katika mipango hiyo ?

Chanzo cha picha, Reuters
Je tishio la Iran linaweza kuzaa vita? Wachambuzi wengi ndani ya Marekani watakujibu hapana.
Wengi wao wanakubaliana na kuibana Iran, na pia kuwapa onyo kali dhidi ya kushambulia maslahi ya Marekani lakini si kufikia kiwango cha vita.
Kitu cha msingi zaidi ni kuwa, hakuna bahati mbaya katika kuanzisha vita, si kitu ambacho hutokea bila watu kujua nini cha kufanya.
Kama vita italipuka basi itakuwa ni maamuzi pambanifu ya viongozi wa mataifa hayo mawili hasimu.












