"Mabomu yanapiga hadi nyumba zinatetemeka"

Chanzo cha picha, Reuters
- Author, Ghoncheh Habibiazad
- Nafasi, BBC News Persian
- Muda wa kusoma: Dakika 2
Raia wa Iran wamekuwa wakielezea yale waliyoyashuhudia wakati Israel na Marekani imekuwa ikitekeleza mashambulizi nchini humo.
Mashambulizi hayo yalianza Jumamosi asubuhi, na kumuua kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei, suala ambalo liliwashtua wafuasi wake na wapinzani wake.
Kuanzia hapo, vituo vingi vya kijeshi vya Iran vimekuwa vikilengwa usiku na mchana.
Mamlaka za Iran zimezima mtandao wa Intaneti, na kufanya kuwa vigumu kwa raia wa taifa hilo kuwasiliana na watu wa maeneo tofauti ya dunia.
Licha ya vikwazo hivyo, BBC imeweza kuzungumza na raia wa taifa hilo, ila tumebadlisha majina yao kamili ili kulinda usalama wao.
Hossein, ambaye ni mkazi wa mji wa Karaj, magharibi mwa Tehran,anatuambia kulikuwa na mlipuko mkubwa karibu na nyumbani kwake siku ya Jumatatu.
"Ilitupiga na nguvu hadi nyumba ilikuwa inatetemeka. Nilisikia mlipuko mkubwa, na najaribu tu kutafuta eneo salama."
Anatuelezea kuwa usiku kucha mabomu yalikuwa yakirushwa eneo hilo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Nilihesabu milipuko 17 zikifuatana. Watu wamejawa na wasiwasi hawajui nini kitatokea baadaye baada ya mashambulizi haya.
Matumaini yao ni kuwa Iran itaafikia makubaliano na Marekani ili wasitishe mashambulizi hayo.
"Jana usiku kulikuwa na watu wengi barabarani wanaoiunga mkono serikali, ila uso zao zilikuwa zimejaa hasira na ghadhabu. Polisi wamekuwa wakishika doria ili kuwaogofya watu. Tanuri za kuoka mikate na vituo vya mafuta vimekuwa vimekuwa vikipokea wateja wengi.
"Barabara hazina watu watu wengi, na watu wako manyumbani kwao, ila hali sasa ya ukosefu wa intaneti imewakasirisha watu. Hii ni mara ya tatu utawala wa Iran unazima mtandao wa intanet mwaka huu."
Hossein anaongezea kuwa "Nadhani jeshi la ulinzi la Islamic Revolution Guard, bado lina nguvu na hili linatia watu hofu.
"Nadhani kifo cha Khamenei, na kwamba aliwaua watu wengi wakati wa maandamano ya hivi karibuni, kimeongeza pengo ambalo tayari lilikuwepo kati ya wanaounga mkono serikali na wanaoipinga."
Amir ambaye anaishi mjini Tehran anasema wakaazi wengi wa mji huo, wamekuwa wakinunua vyakula kwa wengi ili kuweka akiba.
"Watu wamenunua na kuhifadhi vyakula kadiri wanavyoweza. Sote tumekaa nyumbani tukisikia milipuko inapopiga. Lakini hakuna huduma ya mawasiliano"
Inategemea ni watu wangapi muhimu watakaouawa, lakini tuna wasiwasi kwamba viongozi wa Iran wanaweza kuafikia makubaliano."
"Kuna vituo vingi vya usalama mjini vinavyowasimamisha watu wanaowashuku huenda wakawa na nia mbaya"
"Kama ilivyokuwa katika vita ya siku 12 na Israel mwezi Juni mwaka uliyopita, tumechoka. Tumechoka sana. Kifo cha Khamenei hakitoshi utawala wote unapaswa kuondoka."












