Nani atamrithi Lizz Truss kuwa Waziri mkuu Uingereza

Boris, Sunak, Mordaunt

Liz Truss ametangaza kujiuzulu, hatua inayomaanisha kwamba kutakuwa na uchaguzi mwingine wa uongozi kuamua ni nani atakayekuwa kiongozi mpya wa chama cha Conservative lakini pia Waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Mchakato wa kumrithi unatarajiwa kukamilika kufikia Oktoba 28. Wagombea wanahitaji angalau uungwaji mkono wa wabunge wenza 100 kutoka chama hicho, ili kufuzu kuwania kiti hicho. Hatua hii ina maanisha kwamba sio zaidi ya wagombea watatu watakaoweza kuingia kwenye kinyanganyiro hicho kwasababu kuna jumla ya wabunge 357 wa Tory.

Wabunge wa Conservative wameanza kutangaza ni nani wanayemataka awe Waziri mkuu. Siku ya Ijumaa Penny Mordaunt alikuwa mbunge wa kwanza kutangaza rasmi kugombea nafasi hiyo huku wengine wakiatarajiwa kufuata mkondo.

Hawa ndio wanaoweza kuwa wagombea.

Penny Mordaunt

Chanzo cha picha, Reuters

Penny Mordaunt

Penny Mordaunt alipata kionjo cha kuwa Waziri mkuu mapema wiki hii wakati aliposimama kwa niaba ya Lizz Truss wakati kulipoulizwa swali la dharura bungeni. Alipongezwa kwa namna alivyojiamini na huenda akapendelea fursa nyingine katika uongozi. Aliwania katika uchaguzi wa mwisho uliofanyika na kupata uungwaji mkono mzito kutoka kwa wabunge wenzake lakini hakufanikiwa kufika kiwango cha wawili wa mwisho. Baada ya kumuunga mkono Truss, alichaguliwa kuwa kiongozi wa bunge la wawakilishi na rais wa baraza kuu – hatua iliomaanisha alisimamia hafla ya kutawazwa kwa mfalme mpya.

Mnamo 2019, Mordaunt aliweka historia kwa kuwa Waziri wa kwanza Uingereza wa Ulinzi, wadhifa uliomkaa vizuri kutokana na kwamba yeye ni afisa wa jeshi la maji aliyewahi pia kuhudumu kama waziri wa usalama wa kitaifa chini ya David Cameron. Akitangaza azma yake ya kugombea kwenye Twitter, Bi Mordaunt amesema: "Nimehimizwa kwa kuungwa mkono na wenzangu wanaotaka mwanzo mpya, chama kilicho na umoja na uongozi kwa maslahi ya taifa. Nawania kuwa kiongozi wa chama cha Conservative na Waziri wenu mkuu – kuiunganisha nchi yetu, kuwasilisha ahadi na kushinda katika uchaguzi mkuu ujao."

Rishi Sunak

Chanzo cha picha, Reuters

Rishi Sunak

Rishi Sunak aliwania kumrithi Boris Johnson kama kiongozi na alifanikiwa kuwa mojawapo ya wagombea wawili wa mwisho pamoja na Bi Truss, aliyeishia kupata uungwaji mkono zaidi wa wabunge wa Conservative.

Wakati wa kampeni alionya kuwa mipango ya kupunguza kodi ya mpinzani wake Truss huenda yangeathiri uchumi, lakini ujumbe wake ulishindwa kuwavutia wanachama wenzake na alishindwa kwa kura 21,000.

Sunak alipata ubunge mnamo 2015, wa eneo la North Yorkshire huko Richmond. Ni wachache nje ya Westminster waliomfahamu, lakini alikuwa Waziri wa fedha kufikia Februari 2020.

Alibidi kupambana kwa haraka na janga la Corona, na kutumia kiwango kikubwa cha fedha akijaribu kuokoa uchumi wakati wa marufuku ya kutotoka nje. Hili halikuwa rahisi kwa mtu ambaye anapendelea na kuhimiza kiwango kidogo cha kodi kutoka chama hicho, lakini iliimarisha umaarufu wake.

Hatahivyo sifa yake iliathirika kufuatia mzozo kuhusu masuala ya mkewe ya kulipa kodi na muda mfupi baada ya hapo alitozwa faini kwa kukiuka masharti ya kutotoka nje wakati wa janga la Corona.

Boris Johnson

Chanzo cha picha, Getty Images

Boris Johnson

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Zikiwa zimesalia wiki kadhaa kumchagua kiongozi , wagombea wengi huenda ni sura zilizo zoeleka hasaa mwanamume ambaye mwenyewe aliwahi kuwa Waziri mkuu wiki kadhaa zilizopita.

Boris Johnson alilazimika kutangaza kujiuzulu mnamo Julai baada ya kugeukiwa na wabunge wengi na mawaziri. Ilifuata miezi kadhaa ya mzozo kuhusu dhifa zilizofanyika wakati wa marufuku ya kutotoka nje wakati wa janga la Corona – zilizoandaliwa huko Downing Street na mizozo mingineyo, ikiwemo pia uteuzi wake wa Chris Pincher kama kiranja mkuu bungeni licha ya kutambua kuwepo malalamiko rasmi kuhusu mienendo isio sawa ya mbunge huyo.

Mbunge huyo wa Uxbridge anakabiliwa na uchunguzi wa kamati ya bunge kuhusu iwapo alilizuia bunge kwa kuwaambia wabunge kwamba sheria za kutotoka nje zilifuatwa Downing Street. Yeye na wengine walitozwa faini kwa kukiuka sheria za wakati wa janga la Covid.

Hatahivyo bado ana washirika ndani ya bunge na wanachama kwa jumla. Mfuasi wake wa muda mrefu, Nadine Dorries anadai anapaswa kurudi kwasababu alipokea jukumu kutoka kwa wananchi wa Uingereza katika uchaguzi mkuu wa 2019.

Kemi Badenoch

Chanzo cha picha, PA Media

Kemi Badenoch

Kemi Badenoch ni mgombea aliyeshangaza katika ushindani wa hivi karibuni wa uongozi – licha ya kwamba hakushinda. Hatahivyo kuwania kwake kulisaidia kuiinua sifa yake. Licha ya kwamba ni Waziri mdogo , alipata kuungwa mkono na kiongozi mkuu wa chama cha Conservative Michael Gove, na kupata kuwavutia watu kwa mashambulio yake kuhusu utamaduni wa kuwa macho au kuwa na ufahamu wa yanayoendelea maarufu ujulikanao kama "woke".

Alizaliwa Wimbledon, London kusini, alikulia Marekani na Nigeria ambako mamake ambaye ni mwanasaikolojia alikuwa na kazi za uhadhiri.

Kabla ya kuwasili bungeni - anakoliwakilisha eneo la Saffron Walden – alifanya kazi katika mabenki ya kibinfasi na jarida la The Spectator magazine. Wadhifa wake mkuu serikalini mpaka sasa ni kuongoza idara ya biashara ya kimataifa.

Suella Braverman

Chanzo cha picha, Getty Images

Suella Braverman

Kujiuzulu kwa waziri wa zamani wa usalama wa kitaifa kuliongeza shinikizo kwa Liz Truss na Waziri mkuu huyo alijiuzulu siku moja baadaye. Licha ya kwamba kuondoka Braverman kulitokana na kuvuja kwa barua rasmi, barua yake ya kujiuzulu iliojaa hasira ilidokeza kuhusu kutokubaliana katika suala la uhamiaji. Braverman ametafuta kuuomba mrengo wa kulia wa chama chake kuhusu masuala ya kijamii, akieleza kwamba ni ndoto yake kuanza kuwasafirisha wahamiaji kwenda Rwanda. Anaunga mkono Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya. Alihudumu kama mkuu wa sheria kwenye serikali ya Boris Johnson.

Aliwania katika uchaguzi uliopita wa uongozi kufuatia kujiuzulu kwa Jonson lakini hakupata kuungwa mkono katika duru ya pili. Wazazi wake walihamia Uingereza mnamo miaka ya 1960 kutoka Kenya na Mauritius, na wote walijihusisha katika siasa mamake akiwahi kuwa diwani kwa miaka 16.

Braverman ni Waziri wa kwanza kuchukua likizo ya kujifungua mtoto – baada ya sheria kubadilishwa kuwaruhusu mawaziri kupokea malipo wanapokuwa likizo baada ya kujifungua, tofuati na hapo awali ambapo walitarajiwa kujiuzulu.

g