Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi Uingereza Liz Truss ni nani?

Chanzo cha picha, Reuters
Siku 44 tu baada ya kuwa Waziri mkuu, Liz Truss ametangaza kuwa anajiuzulu.
Hadi sasa Waziri mkuu aliyeudumu kwa muda mfupi zaidi alikuwa ni George Canning ambaye alifariki Agosti 1827. Alihudumu kwa siku 119 pekee mamlakani.
Bi Truss alimrithi Boris Johnson kama Waziri mkuu baada ya kushinda ushindi wa wazi dhidi ya Rishi Sunak katika uchauzi wa wajumbe wa chama cha Conservative Party.
Siku mbili baadaye, Malkia Elizabeth II alifariki, nchi ikaingia katika kipindi cha maombolezo na siasa za kawaida ziliahirishwa.
Lakini mwishoni mwa wiki ambayo ilianza kwa mazishi ya Malkia, mbegu ya kuondoka kwenye siasa ya Bi Truss ilikuwa imeanza kupandwa katika bajeti ndogo ya aliyekuwa Kansela wa wakati huo Kwasi Kwarteng.
Ilijumuisha kukatwa kwa pauni bilioni 45 za ushuru, uliodhaminiwa kwa mkopo, uliotikisa masoko ya kifedha na kusababisha kuporomoka kwa thamani ya pauni.
Baada ya muda mfupi serikali ililazimika kuvuruga mipango yake ili kupunguza viwango vya juu vya ushuru, lakini kuendelea kuporomoka kwa masoko ya fedha kulimaanisha Benki Kuu ya England ilazimike kuingilia kati kuzuia kuanguka kwa thamani ya dhamana za serikali.

Katika wiki moja kabla Bi Truss atangaze kuwa anajiuzulu, alimfuta kazi Bw Kwarteng -rafiki wa karibu – na alilazimika kukubali punguzo zilizosalia za mapungufu madogo madogo ya ushuru pamoja na ajenda pana za kiuchumi.
Baada ya chini ya miezi miwili mamlakani, Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss ameachia mamlaka kama Waziri mkuu wa uingereza, huku shindano la kumtafuta mrithi wake likimalizika katika kipindi cha wiki ijayo.
Liz Truss amekuwa ofisini kwa siku 45 pekee - muda mfupi zaidi wa waziri mkuu yeyote wa Uingereza. Waziri Mkuu wa pili aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi alikuwa George Canning, ambaye alihudumu kwa siku 119 baada ya kufariki mwaka 1827.
Shida ilianza wakati Kansela wake wa kwanza, Kwasi Kwarteng, alipohatarisha masoko ya fedha kwa bajeti yake ndogo tarehe 23 Septemba.
Tangu wakati huo, hali ya utulivu ya kihafidhina imebadilika na kuwa hasira iliyoenea ndani ya chama cha wabunge.
Kujiuzulu kwake leo kunafuatia matukio ya ajabu katika Baraza la Commons jana usiku juu ya kura ya fracking. Wito wa kumtaka aende uliendelea kuongezeka saa chache baadaye.

Lakini je Lizz Truss ni nani?
Katika umri wa miaka saba, Liz Truss alicheza nafasi ya Margaret Thatcher kwenye maigizo yaliyohusu uchaguzi mkuu katika shule yake.
Lakini tofauti na waziri mkuu, ambaye alishinda kura nyingi mnamo 1983, hakuweza kufanikiwa.
Mary Elizabeth Truss alizaliwa Oxford mwaka 1975. Analeza kuwa baba yake ni profesa wa hisabati na mama yake ni nesi.
Akiwa msichana mdogo, mama yake alishiriki maandamano kwa ajili ya Kampeni ya Kupunguza Silaha za Nyuklia, shirika lililopinga vikali uamuzi wa serikali ya Thatcher kuruhusu vichwa vya nyuklia vya Marekani kuwekwa katika kituo cha anga cha RAF Greenham Common, magharibi mwa London.
Liz Truss: Maelezo ya msingi
Umri: 47
Mahali pa kuzaliwa: Oxford
Nyumbani: London na Norfolk
Elimu: Shule ya Roundhay huko Leeds, Chuo Kikuu cha Oxford
Familia: Ameolewa na mhasibu Hugh O'Leary na ana mabinti wawili vijana
Eneo bunge: Kusini Magharibi mwa Norfolk Familia ilihamia Paisley, magharibi mwa Glasgow, wakati Truss akiwa na umri wa miaka minne.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Akiongea na BBC kaka yake alisema familia ilifurahia kucheza michezo ya ubao, lakini Truss akiwa mdogo alichukia kupoteza na mara nyingi alitoweka alipoona kuna hatari ya kutoshinda.
Familia hiyo baadaye ilihamia Leeds, ambapo alisoma Roundhay, shule ya sekondari ya serikali. Ameelezea kuona "watoto waliofeli na kukatishwa tamaa na matarajio madogo" wakati alipokuwa huko.
Huko Oxford, Truss alihamia Conservatives.
Baada ya kuhitimu alifanya kazi kama mhasibu wa Shell, na Cable & Wireless, na alifunga ndoa na mhasibu mwenzake Hugh O'Leary mwaka wa 2000. Wanandoa hao wana watoto wawili.
Truss alisimama kama mgombea wa Tory wa Hemsworth, West Yorkshire, katika uchaguzi mkuu wa 2001, lakini alishindwa.
Truss alishindwa tena huko Calder Valley, pia huko West Yorkshire, mnamo 2005.
Lakini, matarajio yake ya kisiasa hayajafifishwa, alichaguliwa kama diwani huko Greenwich, kusini-mashariki mwa London, mwaka wa 2006 na kuanzia 2008 pia alifanya kazi katika taasisi ya wataalamu wa Mageuzi ya right-of-centre Reform think tank.
Baadhi ya wanafunzi wa rika la Truss huko Roundhay wamepinga maelezo yake kuhusu shule hiyo, akiwemo mwandishi wa habari wa Guardian Martin Pengelly, ambaye aliandika: "Labda anachagua kupeleka malezi yake, na kutafsiri kwa urahisi shule na walimu waliomlea, kwa manufaa rahisi ya kisiasa."
Bila kujali masomo yake, Truss alifika Chuo Kikuu cha Oxford, ambako alisoma falsafa, siasa na uchumi na alikuwa akijishughulisha na siasa za wanafunzi, awali akiwa na chama cha Liberal Democrats.
Katika mkutano wa chama wa 1994, alizungumza kuunga mkono kukomeshwa kwa utawala wa kifalme, akiwaambia wajumbe huko Brighton: "Sisi Wanademokrasia wa Kiliberali tunaamini fursa kwa wote. Hatuamini watu wamezaliwa kutawala."
Miaka mingi baadaye, Truss anakumbuka: "Nilijitosa katika nafasi hiyo na nikatoa hotuba ya iliyogusa moyoni kwenye mikutano ya uchaguzi, lakini nikaishia kupata kura sifuri. Hata sikujipigia kura."
Miaka thelathini na tisa mbele, alijitosa kwenye nafasi hiyo kufuata nyayo za uongozi wa Iron Lady katika maisha ya kweli kuwa kiongozi wa Conservative na waziri mkuu.














