Nini kinachofahamika kuhusu mamluki wa 'siri' wa kundi la Wagner ndani ya Ukraine na katika maeneo mengine ya dunia?

Chanzo cha picha, TELEGRAM GROUP @RSOTM
Vikosi vya Ukraine vilipiga moja ya ngome za kikundi cha mamluki wa siri cha Wagner katika majimbo ya Luhansk, na Donbas mashariki mwa Ukraine, alisema gavana Serhiy Haidai alisema Jumapili.
Haidai anasema hoteli ambazo yalikuwa makao makuu ya kundi hilo katika miji ya Kadiivka, Luhansk, zilishambuliwa, na upande wa Urusi ulishindwa vibaya. BBC haikuweza kuthibitisha uwepo wa kikundi cha wagner katika eneo hilo.
Katika mwaka 2014, kundi la Wagner lilionekana Donbas kuwaunga mkono wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi na kuvilazimisha vikosi vya Ukraine kurudi nyuma katika mapigano.
Ujasusi wa jeshi la Uingereza inaonyesha kuwa takriban mamluki 1,000 walipelekwa katika eneo hilo.
Hivi karibuni, kundi hilo limekuwa likiendesha harakati zake katika maeneo kama Ukraine na Syria, pamoja na baadahi ya nchi za Kiafrika, na limekuwa likishutumiwa mara kwa mara kwa uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu.
Kundi la Wagner linafanya nini nchini Ukraine?
Mamluki wa kikundi cha -Wagner wanaaminiwa kuwa wamekuwa wakihusika katika msururu wa mashambulio yanayofanywa katika maeneo ya mshariki mwa Ukarine ambayo yamepangwa na Urusi.
Mara ya kwanza Wagner waliwasili katika maeneo hayo mwaka 2014, anasema Tracey German, Profesa wa mizozo na usalama katika taasisi ya King's College London.
"Mamluki wapatao 1,000 walisaidia wanamgambo wanaounga mkono Urusi katika mapigano ya udhibiti wa majimbo ya Luhansk na Donetsk ," anasema.

Chanzo cha picha, SERHIY HAIDAI
Waendesha mashtaka wa Ukraine wanadai kwamba mamluki watatu kutoka kikundi cha Wagner walitekeleza uhalifu wa kivita katika kijiji cha Motyzhyn, karibu na Kyiv, katika operesheni ya pamoja na vikosi vya Urusi mwezi Aprili.
Na sasa, kulingana na DKT. Samuel Ramani, Mhadhiri katika taasisi Royal United Services Institute, wajumbe wa Wagner wanapigana sambamba na vikosi vya Urusi katika jimbo la Donbas.
"Kikundi cha Wagner kilishiriki pakubwa katika kuiteka miji kama vile Popasna na Severodonetsk katika jimbo la Luhansk," anasema.
Je kikundi cha Wagner kilianza vipi?

Chanzo cha picha, Reuters
Uchunguzi wa BBC ulifichua madai ya uhusika wa afisa wa zamani wa jeshi la Urusi mwenye umri wa miaka 51, Dmitri Utkin, katika kundi. Inaaminiwa kuwa alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Wagner na kukipatia jina lake mwenyewe, kwa kuzingatia jina lake bandia la awali katika jeshi.
Utkin ni mwanajeshi wa zamani aliyepigana vita vya Chechenya, akiwa afisa wa vikosi maalumu, na Luteni Kanali katika kikosi cha Urusi cha huduma za ujasusi, GRU.
Kikundi cha Wagner kilihusika katika mapigano yaliyopelekea kutwaliwa na Urusi kwa jimbo la Crimea mwaka 2014, anasema profesa German.
"Mamluki wake wanaaminiwa kuwa baadhi ya 'wanaume wadogo walivaa magwanda ya kijani ‘ waliovamia jimbo na kulitwa," anasema.
Vyanzo vya mamluki viliiambia BBC kuwa ngome yao ya mafunzo iko katika mji wa Mol'kino, uliopo kusini mwa Urusi, karibu na ngome ya kijeshi ya Urusi.
Urusi imekuwa ikikana kila mara kwamba Wagner ina uhusiano wowote na taifa hilo.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Uchunguzi wa BBC pia ulibaini kuwa uhusiano wa Utkin na kikundi hicho pia ulionyesha nafasi ya Yevgeny Prigozhin,tajiri anayefahamika kama "mpishi wa Putin", ambaye aliitwa hivyo kwasababu alianza kazi yake kama mhudumu wa mgahawa na hatimaye akawa mpishi wa Kremlin.
Mwezi Septemba 2022, rekodi moja ya sauti ilitolewa ambapo ilibainisha Prigozhin alikuwa akijaribu kuwaajiri wafungwa wa Urusi katika kundi la Wagner kufanya kazi nchini Ukraine.
Prigozhin aliwaambia wafungwa kwamba wataondolewa hukumu zao za jela iwapo watajiunga na kikundi hicho.
Katika mwaka 2015, kundi la Wagner kilianza operesheni zake nchini Syia, kikipigana Pamoja na vikosi vinavyoiunga mkono serikali na kulinda machimbo ya mafuta.
Limekuwa likiendesha harakati zake nchini Libya tangu mwaka 2016, likiunga mkono vikosi vya vinavyomtii jenerali Khalifa Haftar.
Hadi mamluki 1,000 wa kundi la Wagner wanaaminiwa kuhusika katika mashambulizi ya Haftar yaliyopelekea vikosi hivyo kufanikiwa dhidi ya serikali rasmi mjini Tripoli mwaka 2019
Mnamo mwaka 2017, kikundi cha Wagner, kilialikwa Katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kulinda migudi ya almasi. Pia kuna ripoti kwamba wanafanya kazi nchini Sudanm wakilinda migodi ya dhahabu.
Je shughuli za Kundi la Wagner zimekuwa zikiripotiwa wapi?

Chanzo cha picha, @RSOTM TELEGRAM GROUP
Mwaka 2020, Waziri wa fedha wa Marekani, alisema kuwa Wagner wamekuwa "wakihudumu katika maeneo ya vita" katika nchi hizi kwa ajili ya makampuni ya madini ya Prighozin, kama vile M Invest ana Lobaye Invest, na akaweka vikwazo dhidi yao.
Hivi karibuni zaidi, Kundi la Wagner lilialikwa na serikali ya Mali Afrika Magharibi magharibi kutoa usaidizi wa usalama dhidi ya makundi ya Islamic State. Kuwasili kwao mwaka 2021 kuliishinikiza Ufaransa kuchukua uamuzi wa kuondoa vikosi vyao nchini humo.
Katika Burkina Faso, Kanali Ibrahim Traoré, ambaye alinyakua mamlaka katika mapinduzic, ameonyesha kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na kundi la Wagner kupambana na Islamic State, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi.
Ramani anasema kwamba nje ya Ukraine, Kundi la Wagner lina jumla ya mamluki 5,000 wanaoendesha operesheni zao katika maeneo mbali mbali ya dunia.
















