Putin na Erdogan wajadili vita vya Ukraine na hali ya Syria

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuomba mwenzake wa Urusi Vladmir Putin, kusitisha vita dhidi ya Ukraine haraka iwezekanavyo, pamoja na kutatua tatizo la Wakurdi nchini Syria.

Moja kwa moja

  1. Putin na Erdogan walijadili vita vya Ukraine na hali ya Syria

    Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan leo amefanya mazungumzo kwa njia na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin, ambapo alimtaka kusitisha vita dhidi ya Ukraine haraka iwezekanavyo, pamoja na kutatua tatizo la Wakurdi nchini Syria.

    Viongozi hao walijadili uhusiano wa Uturuki na Urusi, haswa nishati, pamoja na maswala ya kikanda, pamoja na ukanda wa nafaka na mapambano dhidi ya ugaidi, huduma ya vyombo vya habari ya Kremlin inaarifu.

    Kulingana na ripoti iliyosambazwa na mashirika ya habari ya Urusi, Putin alisema kuwa Urusi inadai kuondolewa kwa vikwazo kwa usambazaji wa bidhaa za kilimo na mbolea za Urusi kwa nchi zinazohitaji.

    Kulingana na Shirika la Anadolu, Erdogan alisema kuwa zaidi ya tani milioni 13 za nafaka tayari zimewasilishwa kwa wale wanaohitaji kupitia juhudi za pamoja.

    Kulingana na yeye, tayari inawezekana kuanza kufanya kazi katika usafirishaji wa bidhaa zingine za chakula na polepole bidhaa zingine ndani ya ukanda wa nafaka.

    "Wakati wa mazungumzo, Rais Erdogan alielezea matakwa yake ya dhati kwamba vita vya Urusi na Ukrain vikomeshwe haraka iwezekanavyo," Reuters ilinukuu idhaa ya kiongozi wa Uturuki ikisema.

    Erdogan pia alimwambia Putin kwamba, kwa mujibu wa makubaliano ya Sochi ya 2019, "ni muhimu kabisa kufuta" mpaka wa Uturuki na Syria kutoka kwa kikosi cha PKK kilichopigwa marufuku nchini hadi kina cha angalau kilomita 30.

  2. Miili 27 yatupwa kando ya barabara nchini Zambia

    Manusura mmoja aliyepatikana katika eneo la tukio amepelekwa hospitalini

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Manusura mmoja aliyepatikana katika eneo la tukio amepelekwa hospitalini

    Miili ya watu 27, wanaoaminika kuwa wahamiaji kutoka Ethiopia, "imetupwa" kando ya barabara katika eneo la Ngwerere kaskazini mwa mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

    Huenda walikosa hewa hadi kufa walipokuwa kwenye usafiri, Msemaji wa Polisi Danny Mwale aliambia BBC.

    Manusura mmoja aliyepatikana "akihema kwakukosa hewa" amekimbizwa katika hospitali ya eneo hilo, alisema.

    Zambia ni kituo cha kupitisha wahamiaji, wengi wao kutoka Pembe ya Afrika, ambao wanataka kufika Afrika Kusini.

    Bw Mwale alisema wakazi wa Ngwerere walipata miili hiyo Jumapili saa 06:00 kwa saa za huko (04:00 GMT).

    Alisema polisi wanaamini wahamiaji hao ni raia wa Ethiopia kulingana na hati za utambulisho zilizopatikana kwao.

    "Uchunguzi wetu wa awali unaonyesha kuwa jumla ya watu 28, wote wanaume wenye umri kati ya miaka 20 na 38, walitupwa Meanwood Nkhosi kando ya barabara ya Chiminuka eneo la Ngwerere na watu wasiojulikana," polisi ilisema katika taarifa yake.

    Miili hiyo imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Chuo Kikuu cha Zambia.

    Katika nchi jirani ya Malawi, mamlaka ilipata miili 25 ya wahamiaji wa Ethiopia katika kaburi la pamoja mwezi Oktoba.

    Polisi huko walisema walikuwa na ushahidi wa kumhusisha mtoto wa kambo wa aliyekuwa Rais wa Malawi Peter Mutharika na ugunduzi huo mbaya.

    Soma:

  3. Mshukiwa wa shambulizi la Lockerbie anazuiliwa Marekani

    Jumla ya watu 270 walikufa katika shambulio la bomu la Lockerbie mnamo Desemba 21, 1988.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Jumla ya watu 270 walikufa katika shambulio la bomu la Lockerbie mnamo Disemba 21, 1988.

    Mwanamume mmoja raia wa Libya anayetuhumiwa kutengeneza bomu lililoharibu ndege ya Pan Am nambari 103 kwenye eneo la Lockerbie miaka 34 iliyopita yuko chini ya ulinzi wa Marekani.

    Marekani ilitangaza mashtaka dhidi ya Abu Agila Masud miaka miwili iliyopita, kwa madai kwamba alihusika katika shambulio la bomu la tarehe 21 Disemba, 1988.

    Mlipuko huo wa ndege hiyo aina ya Boeing 747 katika mji wa Scotland ulisababisha vifo vya watu 270.

    Ni tukio baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea katika ardhi ya Uingereza.

    Mwezi uliopita iliripotiwa kuwa Masud alitekwa nyara na kundi la wanamgambo nchini Libya, na kusababisha uvumi kwamba angekabidhiwa kwa mamlaka ya Marekani ili kujibu mashtaka.

    Mwaka wa 2001 Abdul Basset al Megrahi alipatikana na hatia ya kulipua kwa bomu ndege ya Pan Am 103 baada ya kusikilizwa katika mahakama maalum ya Uskochi nchini Uholanzi. Alikuwa mtu pekee aliyehukumiwa kwa shambulio hilo.

  4. Ujasusi wa Uingereza: Matumizi ya kijeshi ya Urusi 2023 yatafikia theluthi moja ya bajeti

    Idara ya ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imechunguza bajeti mpya ya shirikisho la Urusi, iliyotiwa saini mnamo Desemba 5 na Rais Putin.

    Dola bilioni 143 zimetengwa kwa mahitaji ya kijeshi, huduma maalum na polisi mnamo 2023.

    Hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka jana kwa karibu asilimia 30 ya bajeti yote, wachambuzi wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza wamesema katika muhtasari wa kila siku asubuhi ya Jumapili.

    Pia wanaziona pande za matumizi na mapato ya bajeti kuwa zenye matumaini kupita kiasi, na wanaamini kwamba shinikizo katika sehemu zisizo za kijeshi za bajeti huenda zikaongezeka kwa kiasi kikubwa ili kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza oparesheni ya Ukraine.

  5. Base editing: Tiba mpya yamponya msichana huyu saratani isiyotibika

    Alyssa

    Saratani isiyotibika imeondolewa kwenye mwili wa msichana kupitia matumizi ya kwanza ya aina mpya ya dawa.

    Matibabu mengine yote ya leukemia aliyofanyiwa Alyssa yalikuwa yamegonga mwamba.

    Kwa hivyo madaktari katika Hospitali ya Great Ormond Street walitumia aina ya tiba inayofahamika kama "base editing" kufanya kazi ya uhandisi wa kibaolojia ili kumtengenezea dawa mpya hai.

    Miezi sita baadaye saratani hiyo haionekani, lakini Alyssa bado anafuatiliwa ikiwa itarudi.

    Alyssa, mwenye umri wa miaka 13 na kutoka Leicester, aligundulika kuwa na T-cell acute lymphoblastic leukemia mwezi Mei mwaka jana.

    T-seli zinatakiwa kuwa mlinzi wa mwili - kutafuta na kuharibu vitisho - lakini kwa Alyssa seli hoyo ilikuwa hatari kupita kiasi.

    Saratani yake ilikuwa kali. Tiba ya kemikali, na kisha upandikizaji wa uboho, haikuweza kuuondoa mwilini mwake.

    Bila dawa ya majaribio, chaguo pekee lililobaki lingekuwa tu kumfanya Alyssa astarehe iwezekanavyo.

    “Mwisho ni kifo tu,” alisema Alyssa. Mama yake Kiona, alisema wakati huu mwaka jana alikuwa akiiogopa hataona Krismasi, "akifikiri huu ndio mwisho wetu kuwa pamoja ...na hakua na lingine ila alilia tu"

    \Kilichotokea baadaye hakikuwahi kufikiriwa miaka michache iliyopita na kimewezekana kwa maendeleo ya ajabu teknolojia ya kutumia hembe za vinasaba.

    Kundi la wataalamu kutoka Great Ormond Street lilitumia teknolojia inayoitwa uhariri wa msingi, ambayo ilivumbuliwa miaka sita iliyopita.

  6. Vita vya Ukraine: Urusi yashambulia vikali miji ya Odesa na Melitopol

    Mamlaka zinazoungwa mkono na Moscow huko Melitopol zilichapisha picha za moto

    Chanzo cha picha, BALITSKYEV

    Maelezo ya picha, Mamlaka zinazoungwa mkono na Moscow huko Melitopol zilichapisha picha za moto

    Kusini mwa Ukraine imekumbwa na mashambulizi kutoka pande zote mbili huku Urusi ikirusha ndege zisizo na rubani huko Odesa na Melitopol.

    Jeshi la Ukraine lilidai kudungua ndege 10 zisizo na rubani siku ya Jumamosi lakini zingine tano ziligonga vituo vya nishati, na kuwaacha takriban watu milioni 1.5 bila umeme.

    Baadaye, meya wa Ukraine aliye uhamishoni wa Melitopol alisema mgomo umefanywa katika mji huo unaoshikiliwa na Urusi.

    Picha zilizoshirikishwa na maafisa nchini Urusi zinaonyesha moto mkubwa.

    "Hali katika eneo la Odesa ni ngumu sana," Rais Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake ya usiku kwa njia ya video.

    Tangu Oktoba, Moscow imekuwa ikilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine kwa mashambulio makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani.

  7. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja.