Je unajua kuwa kuna siri nyingi katika damu yako?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kila dakika, kila chembe nyekundu ya damu husafiri kutoka kichwani hadi katika vidole kwenye miili yetu na kukamilisha safari yake kupitia mfumo wa mzunguko wa damu.
Mwili wako hutoa chembe nyekundu za damu milioni mbili kila sekunde. Inachukua nafasi ya seli nyekundu za damu ambazo tayari zimekufa katika mwili wetu. Inaitwa erthosiaties.
Moja kati ya ripoti zilizokusanywa kwa BBC na mtaalamu wa hisabati Hannah Frey na mtaalamu wa vinasaba Adam Rutherford na kugundua siri 12 za damu.
1. Kuna seli nyekundu za damu milioni 30 katika miili yetu
Seli nyekundu za damu ndio seli nyingi zaidi katika mwili wetu. Zipo nyingi zaidi katika mwili wa mwanaume na kidogo katika mwili wa mwanawake
Pia ina chembe za damu zaidi lakini, idadi yake ni ndogo sana. Kati ya chembe zote za mwili wetu, asilimia 90 ziko kwenye damu yako.
2. Seli nyekundu za damu hukaa katika mwili wetu kwa miezi 3 au 4
Huzunguka mara 1,50,000 katika mwili wetu
Inapita katika miili yetu kwa kasi ya kilomita 2 kwa saa, katika mapigo ya moyo na mishipa yetu.

Chanzo cha picha, Getty Images
3. Seli nyekundu za damu zilizokufa katika mwili wetu zina rangi ya kahawia.
Mwili wetu hautoi seli nyekundu za damu za zamani kwa sababu kuna chuma inayosaidia kutengeneza seli nyekundu za damu.
Kinyume chake, huaribu chuma iliyopo katika seli na kuzalisha kemikali inayoitwa bilirubin. Ikifika kwenye ini. Kiungo hiki hupeleka kwenye mfumo wa utumbo.
4. Kuna zaidi ya makundi 30 ya damu
Aina pekee za damu zinazojulikana ni A, B, AB na O. Lakini, kuna aina nyingi za damu.
"Kwa kweli, kuna makundi 30 tofauti ya damu na aina 300 tofauti," asema Profesa Robert Flahr wa Chuo Kikuu cha Sydney, Australia, ambaye anafanya kazi katika Benki ya Damu ya Msalaba Mwekundu.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Zote zina sifa ya 'antijeni' zinazopatikana kwenye uso wa seli zetu nyekundu za damu." "Antijeni ni molekuli (zaidi ya protini, lakini pia wanga) ambayo ina uwezo wa kushambulia mfumo wetu wa kinga," aliongeza.
5. Makundi mawili makuu hupimwa - ABO na Rh chanya au hasi
Kipimo cha ABO kinaonyesha kama una aina yoyote kati ya hizo nne za damu: A, B, AB, au O.
Kipimo cha Rh hupima uwepo wa antijeni ya Rh.
Hivi vina vipengele vidogo.
6. Kuongezewa damu kwa mafanikio kwa mara ya kwanza
Utiaji-damu mishipani uliofanikiwa wa kwanza ulifanywa na daktari wa uzazi Mwingereza James Blundell mnamo 1818.
Uhamisho huu wa damu ulifanywa kwa mwanamke aliyejifungua mtoto.
Blundell alichukua damu kutoka katika mkono wa mume wa mwanamke huyo na kutumia sindano kumdunga mwanamke huyo. Alinusurika. Wale wanaofariki katika kuongezewa damu hii wanachukuliwa kuwa hufariki kutokana na kutofanana kwa aina ya kundi la damu.
7. Wakati aina tofauti za damu zinachanganywa, mwili wako hautakubali
Baada ya kufanya kipimo cha ABO, aina yako ya damu inaweza kuwa A, B au O.
Ikiwa mtu aliye na aina ya damu A atapokea damu kutoka kwa aina ya damu 'B', mwili wake utajaribu kushambulia protini za kigeni kutoka kwa aina ya damu B.

Chanzo cha picha, Getty Images
8. Ikiwa una aina ya damu ya AB, wewe ni 'mpokeaji wa wote'
Kwa sababu una A na B, mwili wako utakubali aina zozote za damu ambazo zina A na B katika kuongezewa damu mishipani.
9. Ikiwa una damu kundi 'O', unaweza kutoa damu kwa kila mtu
Kundi la damu 'O' halina antijeni zozote ambazo hazikubaliwi na kundi lingine lolote la damu. Kwa hivyo, wanaweza kutoa damu kwa watu wa kundi lolote la damu.
Ni kitengo cha damu ambacho huwekwa katika vyumba vya dharura vya hospitali na magari ya kubeba wagonjwa. Hii ni kwa sababu hakuna muda wa kuangalia aina ya damu kabla ya kuongezewa.

Chanzo cha picha, Getty Images
11. Rh ni aina nyingine ya protini nje ya chembe nyekundu za damu.
Protini ya 'Rh Factor' hurithiwa kupitia jeni. Ikiwa una hii katika mwili wako, una Rh chanya. Ikiwa mwili wako hauna, wewe ni Rh hasi Kwa ujumla, wanawake wajawazito hupimwa kwa Rh hasi. Ikiwa mtoto wako ana Rh chanya na aina zozote za damu zimechanganyika wakati wa kujifungua, mama anaweza kusababisha athari ya kinga ambayo inaweza kudhuru mimba inayofuata.
Rh factor inapaswa kupimwa wakati wa ujauzito.
Uwepo wa 'Rh factor' hugunduliwa na ikiwa ni lazima, mama anaweza kupewa dawa za viuasumu antibiotics ili kuzuia kinga kudhurika na kulinda viinitete vya siku zijazo.
12. Makundi fulani ya damu yana sifa fulani
Kwa mfano, ikiwa una damu ya "Duffy Negative", unastahimili malaria zaidi.
Katika Afrika Magharibi, zaidi ya 95% ya watu wamefaidika nayo.















