Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Ruto ajiandaa kuunda serikali huku Odinga akisimamia msimamo wake

Chanzo cha picha, William Ruto/facebook
- Author, Abdalla Seif Dzungu
- Nafasi, BBC Swahili
Rais Mteule William Ruto: Mawaziri wangu watajibu maswali Bungeni.
Rais Mteule William Ruto amesema kwamba mawaziri katika serikali yake watawajibishwa bungeni, kupitia kujibu masuali ya jinsi serikali yao inavyofanya kazi.
Vilevile William Ruto amewataka wafanyakazi wa umma kutojihusisha na siasa na badala yake kuwahudumia Wakenya wote bila kupendelea , chama, kabila au eneo wanalotoka.
Akizungumza alipokutana na viongozi mbali mbali waliochaguliwa kupitia Muungano wa Kenya Kwanza, Ruto amesema kwamba watabadili sheria za vikao vya bunge kuhakikisha kwamba mawaziri wa serikali yake wanajibu masuali.
Amesema kwamba haitoshi kwa mawaziri kukutana na kamati za bungee pekee na kwamba ni muhimu waelezee Wakenya jinsi serikali yao inavyowahudumia.
Amesema kwamba licha ya kuwa serikali yake itakuwa ya kidemokrasia ni lazima iwajibishwe.
Kuhusu wafanyakazi wa Umma , Ruto amesema kwamba anawahakikishia kwamba kazi zao zipo salama na kwamba hawatahusishwa tena na masuala ya kisiasa kama ilivyo sasa.
Matamshi ya Ruto yanajiri siku mbili tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliopita ambapo matokeo yake yamezua mvutano katika ya tume ya uchaguzi nchini IEBC.
Siku ya Jumanne makamishna wanne wa tume ya uchaguzi IEBC kati ya saba walipinga matokeo yaliotolewa na mwenyekiti wao wafula Chebukati, wakidai kwamba yalikabiliwa na kiza kinene.
Makamishna hao wanadai kwamba hesabu ya matokeo iliotangazwa na Wafula Chebukati haiingiliana na jumla ya idadi ya kura ya wagombea wanne wa Urais.
Vilevile wanadai kwamba wafula Chebukati hakuwahusisha katika kuhakiki matokeo ya mwisho kabla ya kuyatangaza kwa umma.
Tayari Aliyekuwa mpinzani mkuu wa William Ruto na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ameapa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo akisema kwamba mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alikiuka katiba kwa kuytowahusisha makamishna wake katika mchakato wote wa kutangaza matokeo hayo.

- YA MSINGI: Uchaguzi Kenya 2022: Kwa nini uchaguzi wa Kenya mwaka huu ni muhim
- MIUNGANO: Uchaguzi Kenya 2022: Musalia Mudavadi kujiunga na naibu rais William Ruto itabadilisha siasa za Kenya?
- UNAYOFAA KUJUA: Uchaguzi Kenya 2022: Je Naibu wa rais wa Kenya William Ruto anakabiliwa na changamoto gani katika kumteua naibu wake wa rais?
- UCHAMBUZI: Uchaguzi wa Kenya 2022: Je hatua ya Rais Kenyatta kumuunga mkono Raila Odinga itamsaidia au kumharibia?
- WASIFU:William Ruto: Muuza kuku aliyepanda ngazi hadi kuwa naibu wa rais wa Kenya
- RAILA ODINGA:Uchaguzi Kenya 2022: Siwezi kuwa kibaraka wa mtu yeyote-Raila Odinga
- WAGOMBEAJI:Wafahamu wagombea 4 wanaowania urais nchini Kenya













