William Ruto, ni miongoni mwa wanasiasa wengi wakubwa nchini Kenya walioweka wazi nia zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kurithi mikoba ya aliyekuwa 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.
Mwanasiasa huyu tajiri ambaye amekuwa na ndoto za kuwa Rais wa Kenya, amekuwa akikutana na vikwazo lukuki vya kisiasa, ikiwemo kuzuiwa kwa sababu ama kuzuiwa kwa makusudi kufanya shughuli kadhaa za kisiasa na binafsi kutokana na msukumo wa kisiasa.
Ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini humo, walioweka wazi nia zao za kuingia Ikulu ya Kenya, kupitia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022, kurithi mikoba ya 'swahiba wake', Uhuru Kenyatta.
Lakini Ruto ni nani hasa?
Ruto anatoka katika familia ya kawaida tu na kuwa mwanasiasa tajika nchini Kenya. Anatokea kwenye jamii ya Wakalenjin akizaliwa Disemba 21, 1966 katika kijiji cha Sugoi, magharibi mwa Rift Valley.
Elimu yake ya msingi na sekondari amesomea katika shule za kawaida kabla ya kujiunga na Chuo kikuu cha Nairobi. Waliosoma naye hasa shule ya sekondari wanamkumbuka Ruto kama 'mtu mtaratibu, mwenye haya na wakati wote akijiweka kama mtu wa kawaida tu".
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Ruto (katikati), amekuwa hafichi nia yake ya kuingia Ikulu ya Kenya katika uchaguzi mkuu wa 2022
Kwa mujibu wa mama yake, Sara Cheruiyot, "hakuwa mkaidi" na wakati wote alikuwa 'mtiifu, mwaminifu na anayefika kwa wakati'. Hakuwa mtu anayependa ugomvi ama kugombana na wenzake, muda mwingi alikuwa akibeba kitabu kwa ajili ya kujisomea.
Akiwa chuo Kikuu, alikuwa kiongozi wa kwaya ya umoja wa wakristo chuoni hapo. Akiwa kwenye masuala hayo ya kwaya ya kanisa, alikutana na mtu aliyemuhusudu sana kwenye siasa, rais wa zamani wa nchi hiyo, Daniel arap Moi. Kama ilivyo kwa Ruto, Rais Moi pia anatokea kenye jamii ya Wakalenjini na muumini wa kanisa.
Ruto alisaidia kuanzishwa kwa kikundi cha vijana kilichoitwa Youth for Kanu 92 (YK92), ambacho Moi alikitumia kurejea madarakani mwaka 1992. Moja ya kampeni kubwa ya kikundi hicho ilikuwa ni kumwaga mabilioni ya pesa, hatua ambayo baadae ilikuja kulaumiwa kuwa chanzo cha mtikitiso wa uchumi katika miaka ya mwanzoni mwa 1990s. Inaeleweka kwamba wakati huu, ndio Ruto alipotengeneza utajiri wake.
Siasa zake hazitofautiana na wanasiasa wengi wa Kenya
Ruto aliingia kwenye siasa kwa mgongo wa kundi la vijana la Youth for Kanu 92 (YK92). Alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 1997 na muda mfupi baadae akawa mmoja wa wanasiasa wakubwa nchini Kenya.
Wakati KANU ilipoanguka mwaka 2002, Moi alimteua Ruto kuwa naibu waziri wa mambo ya ndani, kabla ya kumpandisha cheo na kuwa waziri kamili. Mpaka wakati huo maafisa wengi wakubwa walijiondoa katika chama tawala hasa baada ya kuteuliwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa mrithi wa kiti cha Urais na kupewa Baraka na Moi.
Ingawa KANU ilishindwa uchaguzi, Ruto alitetea kiti chake cha Ubunge na akachaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho mwaka 2005. Ilipofika mwaka 2006 akatangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Kenyatta (kushoto) na naibu wake Ruto (kulia) walikuwa wakiitwa mapacha, kutokana na 'uswahiba wao kwenye chaguzi zilizopita kupitia Jubilee
Akaanza kufanya kazi kwa karibu na Raila Odinga, waziri wa zamani na hasimu mkubwa wa Rais Moi. Alitumia sana Radio maarufu kwa Wakalenjini, Kass FM, kama jukwaa la kupitishia ajenda zake.
Alikahama chama cha KANU na kujiunga na chama cha Odinga cha Orange Democratic Movement (ODM). Kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kutafuta fursa nzuri ya kisiasa ni siasa zilizoshamiri sana Kenya kwa sasa, na wanasiasa wengi wamekuwa wakifanya hivyo, jambo ambalo halimtofautishi na wanasiasa wengine.
Ruto alishindwa katika kura za ndani za kumsaka mgombea urais kupitia ODM, lakini alikuwa mstari wa mbele kushawishi mamilioni ya wananchi wa eneo bonde la Ufa anakotokea na maeneo mengine kumuunga mkono Raila Odinga, kiasi cha hata kura za maoni kuonyesha kwamba alikuwa anashinda uchaguzi mkuu wa 2007.
Alikuwa mtu wa karibu wa Odinga na mpiganaji wake wakati wote wa uchaguzi na zoezi la kuhesabu kura. Mamlaka za uchaguzi zikamtangaza Rais Mwai Kibaki kumshinda Odinga na hapo ukawa mwanzo wa ghasia kubwa za kikabila zilizodumu mwaka hadi Februari 2008, Kibaki na Odinga walipokubaliana kuunda serikali ya Muungano. Ruto akateuliwa kuwa waziri wa kilimo.
Maelezo ya picha, Ruto (kushoto) na Odinga (kulia), walikuwa 'maswahiba' wanaotarajia kusigana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022
Kama sehemu ya makubaliano, uchanguzi wa vurugu hizo ukafanyika, na wote Rais Kibaki, waziri mkuu Odinga wakaishia kwenye tuhuma za ndani, huku Ruto ambaye tayari walishatofautiana na Odinga, akapelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC).
Ruto alikana kwa nguvu tuhumza zozote za kuhusika kwake na ghasi na kusema anachokiamini ni kwmaba, tuhuma hizo ni za kutungwa.
Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?
Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya
Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake
Raila Amollo Odinga
Muungano wa Azimio la Umoja
Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.
William Samoei Ruto
Muungano wa Kenya Kwanza
Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC
George Wajackoyah
Chama cha Roots
Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito
David Mwaure Waihiga
Chama cha Agano
David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
Kupambana na ufisadi uliokithiri.
kuunda nafasi za ajira.
Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.
Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa
Novemba 2012, aliungana na Kenyatta kuunda Jubilee Alliance. Kupitia muungano huo, walitumia kesi yao huko ICC kujijenga kisiasa na kueleza mashataka dhidi yao ni kuingilia uhuru wa Kenya. Mkakati wao ulifanya kazi na kuendelea kuwa Rais na makamu wake mpaka sasa
Ruto na Misukosuko yake ya kisiasa
Kuwa mwanasiasa kunahitaji uwe na ngozi ngumu, lakini kuwa sehemu ya Ruto kunahitaji kuwa ngozi ngumu zaidi, ni miongoni mwa wanasiasa wachache waliopitia masahibu makubwa katika maisha yao ya siasa Kenya.
Amekuwa akizongwa na vitendo vya rushwa ambavyo mara zote amekuwa akikana kuhusika navyo. Mwezi Februari 2009, almanusura apigiwe kura za kutokuwa na Imani naye kutokana na kashfa ya mahindi chini ya wizara yake. Oktoba 2010 akawekwa kando kwenye baraza la mawaziri kufuatia tuhuma za kuuza ardhi ya umma. Baadae akarejeshwa. Juni 2013, mahakama kuu ilimuamuru kusalimisha heka 100 na kumpa fidia mkulima ambaye alimtuhumu Ruto kumpokonyaa ardhi hiyo wakati wa vurugu za mwaka 2007.
Hata hivyo naibu rais huyo amekuwa akisisitiza kwamba yeye hana shida, hana tatizo, na kusema utajiri wake unatokana na juhudi zake za kuchapa kazi.
"Niliuza kuku katika maeneo ambayo reli inakatiza karibu na nyumbani kwetu, nikamjengea baba yangu nyumba kwa kutumia mkopo wangu wa chuo, nikawalipia ada ndugu zangu. Mungu amekuwa mwema kwenye juhudi zangu, nashukuru nimejaliwa," aliiambia gazeti la The Star nchini Kenya.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ruto akihudhuria kesi yake kwenye Mahakama ya ICC, Mei 14, 2013
Kasheshe lingine kubwa ambalo hawezi kulisahau Ruto ni la kufikishwa katika mahakama ya ICC. Aliyewasilisha majina ya waliohusika kwenye ghasia za Kenya, alikuwa Kofi Annan msuluhishi na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ruto aliwahi kuliambia gazeti la Sunday Nation la Kenya mwaka 2009 kwamba, Annan "anapaswa kuwasilisha bahasha hiyo… ili uchunguzi mzuri uweze kuanza."
Mahakama hiyo iliondoa mashitaka kwa washukiwa wengine na kusalia na Kenyatta, Ruto na Joshua arap Sang, mwandishi kutoka redio Kass FM radio ambaye alituhumiwa kwa kuchochea vurugu kwa kusaidia kuratibu mashambulizi dhidi ya jamii ya wakikuyu.
Mbali na hayo, Ruto amezuiwa mara kadhaa kufanya mikutano ya kisiasa na hivi majuzi amezuiwa kusafiri kwenda Uganda , kwa shughuli binafsi kukutana na Rais Yoweri Museven.
Kupeana mikono kwa Uhuru na Odinga, kulikotingisha uhusiano wake na Uhuru
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Hatua ya Rais Kenyatta (kushoto) na aliyekuwa hasimu wake Odinga (Kulia) kupeana mikono, kumekuwa mwanzo wa mtikisiko wa siasa za Ruto kwenye Ikulu
Uhusiani wa Ruto na Kenyatta, kwa mara ya kwanza ulianza kutikisika mwezi machi 2018, wakati Rais Uhuru Kenyatta, alipomtambulisha na kumkaribisha hasimu wake wa zamani Odinga kama mshirika wake mwingine wa tatu.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 Odinga, ambaye alikuwa sehemu ya muungano mwingine wa NASA, akiwa na washirika wengine, alipinga matokeo ya uchaguzi huo akisema hayakuwa sahihi kwa vile uchaguzi haukuwa huru nawa haki.
Uhuru akatumia nafasi yake ya Urais kumleta karibu zaidi Odinga wakati huu anakwenda kumaliza muhula wake wa pili wa urais, na kupeana mikono kuashiria kumalizika kwa uhasama wao kisiasa na kusisitiza Amani iliyoanza kutetereka baada ya matokeo ya uchaguzi.
Kenyatta hakutaka kurejea kwenye ghasia za mwaka 2007 zilizoua maelfu ya Wakenya. Alitaka Amani, na Amani hiyo aliona inawezekana kama atamsogeza karibu Odinga.
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, uswahiba wa Kenyatta (katikati) na Odinga (Kulia), unamuweka njia panda Ruto (kushoto) katika harakati zake za kuingia Ikulu
Taaratibu, Ruto akawa anawekwa mbali huku Odinga akisogezwa karibu. Kwa sasa uhusiano wao wa mashaka umekuwa wazi zaidi. Namna wanavyozungumza, namna wanavyoshughulikia masuala yao na namna wanavyoshirikiana, inakuonyesha uhusiano wao hauko kama wa zamani, na hilo linaleta picha ya uchaguzi ujao utakavyokuwa.
Pamoja na kuonekana wazi, kwenda tofauti na Uhuru, Ruto amegoma kuachia ngazi nafasi yake ya naibu Rais, kama inavyoshauriwa na wengi. Lakini wadadisi wanasema kusalia kwakwe kwenye nafasi hiyo kunampa nguvu na jukwaa la kuendelea na harakati zake za kuingia Ikulu mwakani.
Huenda Odinga akaungwa mkono kwa uwazi na Uhuru kwenye uchaguzi mkuu ujao, na kumuacha 'swahiba' wake Ruto aliyejipanga kwa muda mrefu kuwania urais.