Martha Karua: Raila Odinga amteua Karua kuwa mgombea mwenza wake wa Urais

Martha Karua

Chanzo cha picha, Odinga campaign

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amemteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza wake katika ushaguzi mkuu ujao wa urais.

Bi Karua, aliyekuwa waziri wa sheria na mgombeaji urais, anatoka eneo la kati ambalo lina idadi kubwa zaidi ya wapiga kura waliosajiliwa nchini.

Akizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta, Bw Odinga alimsifu Bi Karua kwa bidii na rekodi yake ya haki za binadamu.

"Nilimhitaji Joshua wa kweli kando yangu, ambaye hatakuwa koti la ziada. Baada ya kutafuta na kutafakari, pamoja na mashauriano, nimefikia uamuzi kwamba anayeshikilia nafasi hii lazima awe mwanamke," Bw Odinga alisema.

Bw. Raila Aliongeza: "Ofisi ya Naibu wa Rais ni ofisi mbayo haiwezi kushindana na urais. Anayeshikilia wadhifa huo lazima awe mfanyakazi mwenza"

Iwapo atachaguliwa mwezi Agosti mwanasiasa huyo mkongwe atakuwa naibu wa rais wa kwanza mwanamke wa Kenya.

Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa mgombea mwenza Bi Karua alisema: ''Huu ni wakati wa wanawake wa Kenya. Ni wakati ambao bibi yangu angejivunia...lakini sishangai kwa sababu vizazi vya wanawake vimepigania mabadiliko. Huu ni wakati wetu kama wanawake wa Kenya. Pia ni wakati kwa wanaume: ni ndugu na baba zetu.

Martha Karua speaking

Chanzo cha picha, Odinag campaign

Pia alichukua muda huo kuelezea safari yake ya kisiasa na kiongozi huyo wa Azimio akiongeza kuwa ana rekodi imara ya kutetea Wakenya na hivyo basi ndiye anayefaa zaidi kuwa rais.

Bi Karua, alijiunga na timu ya Azimio mnamo Machi amekuwa akizunguka nchi nzima akipigia debe uungwaji mkono kwa Bw Odinga.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Wiki iliyopita, alihudhuria mahojiano ya mgombea mwenza ambapo alisema atakubali uamuzi wa jopo la mahojiano.

Chaguo la Martha Karua limegawanyika Azimio ambayo ilimfanya kiongozi wa chama cha Wiper Kenya na makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka kujitenga na muungano huo.

Katika kikao tofauti na wanahabari, Bw Musyoka alimtakia Bi Karua kila la kheri.

"Namtakia kheri mgombea mwenza wa Raila Martha Karua. Tumekubali kwenda njia tofauti. Nilimwambia Raila uamuzi wa kuchagua Karua utakabiliwa na upinzani mkubwa. OKA itapambana kivyake na hivi karibuni Wiper itazindua manifesto yake yenyewe," alisema.

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma