Uchaguzi Kenya 2022: Mfahamu mgombea mwenza wa Raila Odinga Martha Karua

Martha Karua

Chanzo cha picha, Martha Karua/facebook

Maelezo ya picha, Martha Karua

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amemteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza wake, na kumfanya mwanasiasa huyo mkongwe kuwa mwanamke wa kwanza kuwania unaibu rais kwa tiketi ya chama kikuu cha siasa.

Bi Karua, aliyekuwa waziri wa sheria na mgombeaji urais, anatoka eneo la kati ambalo lina idadi kubwa zaidi ya wapiga kura waliosajiliwa nchini.

Iwapo atachaguliwa mwezi Agosti mwanasiasa huyo mkongwe atakuwa naibu wa rais wa kwanza mwanamke wa Kenya.

Lakini Martha Karua ni nani?

Martha Karua alizaliwa tarehe 22 mwezi Septemba 1957 na ni mama wa watoto wawili.

Alianza shule katika shule ya msingi ya Mugumo na baadaye kujiunga na shule ya upili ya wasichana ya Kabare katika eneo la Kerugoya. Katika masomo kidato, mara ya kwanza alijiunga na shule ya upili ya Kiburia baadaye akaelekea shule ya upili ya Ngiriambu na hatimaye shule ya upili ya Karoti ambapo alikalia mtihani wake wa cheti cha Afrika mashariki.

Baadaye alijiunga na shule ya upili ya Nairobi kwa msomo ya A level. Alihitimu na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi 1980, kabla ya kujipatia Diploma katika mafunzo ya sheria 1981.

Kazi ya kuwa mwansheria: Alihudumu kuwa hakimu katika mahakama kadhaa miaka ya 1980 hadi 1987, ambapo alianza kuhudumu kama wakili hadi 2002.

Bi Karua alikuwa na jukumu muhimu katika upanuzi wa demokrasia nchini Kenya na masuala ya Jinsia wakati wa harakati za kupigania vyama vingi miaka ya tisini.

Martha karua na Raila Odinga

Chanzo cha picha, Martha Karua/facebook

Maelezo ya picha, Martha karua na Raila Odinga

Alikuwa miongoni mwa mawakili waliojipatia jina la 'Young Turks' ambao waliipinga serikali ya aliyekuwa rais wa Kenya Daniel Arap Moi na kufanikiwa kuleta siasa za vyama vingi nchini Kenya.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Akiwa Wakili, aliwawakilisha wapiganiaji wa haki za kibinadamu pamoja na wanaharakati wa kisiasa waliokosana na utawala wa rais Moi.

Baadhi ya kesi alizowakilisha ni pamoja na ile ya uhaini dhidi ya bwana Koigi Wamwere na marehemu Mirugi Kariuki mwaka wa 1990.

Siasa

Alichaguliwa mara ya kwanza kama mbunge wa Gichugu 1992 na kuhudumu hadi 2013 wakati alipowania urais na kumaliza wa sita akiwa na kura 43,881.

Bi Karua amehudumu kama waziri katika wizara ya maji na ile ya haki hadi alipojiuzulu kwa ghafla baada ya kukosana na aliyekuwa rais Mwai Kibaki mwaka 2008.

Alikuwa akijulikana kwa jina la utani 'Iron Lady' likimaanisha mwanamke mkakamavu na asiyetetereka kutokana na umaarufu wake katika jukumu la kutetea serikali yake.

Katika Uchaguzi wa 2017, aliwania kiti cha ugavana cha Kirinyaga lakini akashindwa na Anne Waiguru.

Alikwenda mahakamani kupinga matokeo hayo akidai udanganyifu, lakini akapoteza tena katika mahakama kuu, mahakama ya rufaa na mahakama ya kilele.

Alichukua suala hilo hadi katika mahakama ya haki ya Arusha , ambapo aliishtaki serikali ya Kenya kwa kumnyima uhuru wa kupata haki yake.

Katika kesi yake alipeleka ushahidi wa kanda ya video aliowasilisha mbele ya mahakama kuu, lakini uushahidi huo ulipotea chini ya usimamizi wa mahakama hiyo.

Hatahivyo mahakama ilitoa uamuzi bila ya kufanya uchunguzi na kuipata serikali ya Kenya na makosa na ikampa Bi Karua fidia ya ksh millioni 2.7 kwa kukiuka uhuru wake wa kupata haki.

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma