Mzozo wa Ukraine: Putin ayaonya mataifa yanayoingilia mzozo wa Ukraine kwamba 'yatapata jibu la haraka'

Chanzo cha picha, Getty Images
Taifa lolote litakalojaribu kuingilia vita vya Ukraine litakabiiwa na jibu la haraka , rais wa Urusi Vladmir Putin ameonya.
''Tuna kila silaha ambazo tunajivunia…Tutazitumia iwapo tutahitajika kufanya hivyo'', alisema, katika kile kinachoonekana kuzungumzia kuhusu silaha za masafa marefu na zile za kinyuklia''.
Washirika wa Ukraine wameongeza idadi ya silaha zinazoingia nchini humo , huku Marekani ikiapa kwamba Ukarine itaishinda Urusi.
Maafisa wa magharibi wanasema kwamba Urusi inashindwa kupiga hatua zozote mashariki mwa Ukraine.
Wiki iliopita, Urusi ilitekeleza mashambulizi makali ili kujaribu kulinyakua eneo la Donbas baada ya kujiondoa katika maeneo karibu na mji mkuu wa Kyiv.
Lakini kulingana na afisa mmoja, vikosi vya Urusi vinapata upinzani mkali katika kuyakabili majeshi ya Ukraine na kwamba yanapata hasara kubwa.
Katika tukio jingine, kamishna wa tume ya bara Ulaya ameishutumu Urusi kwa baada ya Moscow kukata usambazaji wa gesi yake kwa mataifa ya Bulgaria na Poland.
Rais wa tume hiyo Ursula von der leyen amesema kwamba inaonesha kwamba Urusi haiaminiki kama muuzaji bidhaa hiyo.
Kremlin imesema kwamba Urusi ilikuwa imelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na hatua ya mataifa ya magharibi ..kuchukua hatua ''zisizo za kirafiki''.
Hatua ya kampuni ya Gazprom kusitisha usambazaji wa gesi - baada ya Poland na Bulgaria kukataa kulipa kwa kutumia sarafu ya Rubles - matakwa yaliowasilishwa na Rais Vladmir Putin mwezi Machi kuonesha kuanguka kwa sarafu hiyo inayokabiliwa na vikwazo vya mataifa ya magharibi.

Chanzo cha picha, Reuters
''Iwapo mtu kutoka nje atajaribu kuingia nchini Ukraine na kuweka vitisho vya kimkakati dhidi ya urusi, jibu letu litakuwa la haraka'' , alisema.
''Tuna vifaa vyote vya kujibu ambavyo ni sisi pekee tunaojivunia'', na hatutajisifu, tutavitumia iwapo itahitajika
Kiongozi huyo wa Urusi aliongezea kwamba maamuzi yoyote ya jibu hilo yamefanyika - bila kutoa maelezo zaidi.
Urusi ilivamia Ukraine mnamo Februari 24, na ndani ya siku chache Rais Putin aliamuru jeshi lake kuweka vikosi vya nyuklia katika hali ya tahadhari.
Wachambuzi wanaashiria vitisho kama hivyo ni jaribio la Bw. Putin kuonya washirika wa Ukraine kutoingili kati mzozo huo.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Rais Putin alisema hayo siku moja baada ya mataifa ya magharibi kufanya mkutano wa kilele nchini Ujerumani , na kuahidi kuunga mkono jeshi la Ukraine.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliahidi kufanya kila juhudi "angani na ardhini" kuhakikisha Ukraine inashinda vita hivyo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la nchi zinazoahidi Ukraine msaada wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na tangazo la Ujerumani kwamba itatuma vifaru 50 vya kudungulia ndege, katika mabadiliko makali ya sera.

Maafisa wa Magharibi wamekuwa wakitoa maelezo ya hivi karibuni kuhusu vita hivyo na wanasema Urusi imeendelea kupeleka wanajeshi wake katika eneo la Donbas na imepata mafanikio madogo.
"Lakini wanapopigana na malengo halisi ya kijeshi, wanaona kuwa ni vigumu kushinda upinzani mkali wa Ukraine na wanapata hasara," afisa mmoja alisema.
Mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo pia imelemaza juhudi za Urusi kusonga mbele. "Warusi hawapendi kupigana kwenye mvua," afisa mmoja alisema, akiongeza kwamba Warusi wana ufahamu duni wa kimbinu na wanaendelea kuteseka kutokana na matatizo ya vifaa.
Wana uwezo wa kufanya kazi nje ya barabara , lakini maafisa wanasema inashangaza kwamba wamechagua kutofanya hivyo.
Hata katika maeneo ambayo vikosi vya Ukraine vimejikuta vimezingirwa, vimeweza kudhibita hali hiyo "kwa muda wa kushangaza". (Mariupol ikiwa mfano dhahiri zaidi)
Maafisa walibainisha kuwa hata katika maeneo ambayo Urusi imepiga hatua, vikosi vya Ukraine vimeonyesha uwezo wa "ajabu" wa kukabiliana na mashambulizi - wakati mwingine wakifanya hivyo kwa kasi kwamba Warusi wanalazimika kurudisha mguu nyuma.
Vikosi maalum vya Ukraine, vinavyofanya kazi, nyuma ya mstari wa oparesheni ya Urusi, vinatumia udhaifu wa njia ya usambazaji, ambayo inasaidia Ukraine kupata muda wa kuipanga.












