Urusi na Ukraine: Tunachofahamu kuhusu mashambulio ya Moscow katika eneo la Donbas

Soldado ucraniano usa binoculares en la región de Donetsk.

Chanzo cha picha, Reuters

Ni vita ambayo onyo ilikuwa limetolewa mapema.

Mashambulizi mapya na makubwa yaliyotarajiwa kufanywa na Urusi katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine yalianza Jumatatu katika ukanda wa mbele umbali wa maili 300 kutoka ncha ya kusini hadi kaskazini ya mbali, kuelekea mji wa Kharkiv.

Jumanne hii, mashambulio ya mizinga ilirindima huku Moscow ikisema kuwa imefanikiwa kulipua maeneo zaidi ya 1,000.

Mashambulizi haya ni matokeo ya mkakati mpya uliotangazwa na serikali ya Vladimir Putin mwishoni mwa Machi, mwezi mmoja baada ya kuanza kwa uvamizi wa Ukraine.

Baadaye Moscow ilitangaza kumalizika kwa awamu ya kwanza ya oparesheni yake na kusema kwamba itaelekeza juhudi zake katika "ukombozi kamili" wa mkoa wa Donbas, ikimaanisha kuwa ilikuwa inakamilisha juhudi zake za kuishinda Kyiv.

Jumatatu wiki hii Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alitangaza kuwa Moscow tayari imeanza awamu mpya, baada ya kujiondoa na kuundwa upya kwa vikosi vya Urusi,

"Sasa tunaweza kuthibitisha kwamba wanajeshi wa Urusi wameanza vita vya Donbas, ambavyo wamekuwa wakivitayarisha kwa muda mrefu. Sehemu kubwa ya jeshi la Urusi sasa inahusika na mashambulizi haya," rais alisema katika ujumbe wa televisheni.

Unaweza pia kusoma

Wizara ya Ulinzi ya Urusi baadaye siku hiyo ilithibitisha kuanza kwa mashambulizi haya mapya kwa kuripoti kwamba imeshambulia mamia ya malengo ya kijeshi kusini na mashariki mwa Ukraine, karibu na miji kama Zaporizhia, Kramatorsk, Krivói Rog, Odessa na Odessa. Mykolaiv.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alisisitiza kwamba Urusi itatumia tu silaha za kawaida katika awamu hii mpya ya vita.

Jumanne hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alithibithisha rasmi kuanza kwa hatua hii mpya ya vita.

"Oparesheni mashariki mwa Ukraine inalenga, kama ilivyotangazwa tangu mwanzo, kukomboa kabisa jamhuri za Donetsk na Luhansk [zinazojitangaza]. Na oparesheni hii itaendelea," Lavrov alisema.

"Hatua nyingine ya oparesheni hii inaanza, na nina hakika itakuwa wakati muhimu sana katika oparesheni hii yote maalum," aliongeza.

Mashambulio ya Urusi ni makubwa kiasi gani?

Kwa wiki kadhaa, Moscow imekuwa ikikusanya wanajeshi katika eneo la Donbas baada ya kuachana na mashambulizi yake magharibi mwa Ukraine.

Humo elevándose de una refinería a 120 kilómetros de Donetsk el pasado 16 de abril.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maafisa wa Marekani wanasema Urusi ina vikosi 76 mashariki mwa Ukraine, na imeongeza vingine 11 katika siku za hivi karibuni. Vikosi hivi kwa kawaida hujumuisha wanajeshi kati ya 700 na 900 pamoja na vifaa vya kijeshi.

Kulingana na makadirio ya Ukrainei, kwa jumla kuna zaidi ya wanajeshi 700,000 wa Urusi katikaeneo la Don Bas.

Mtaalamu wa sera za usalama wa Urusi Aglaya Snetkov anabainisha kuwa vikosi vingine 22 vinaaminika kuwa karibu na mji wa bandari wa Mariupol ulioharibiwa kusini mwa Ukraine.

Ikiwa mji huo muhimu utaangukia mikononi mwa wanajeshi wa Urusi, itaruhusu vikosi vyake kuelekea kaskazini na kujiunga na mapigano huko Donbas.

Je, Moscow inaweza kutumia silaha za nyuklia?

Katika mahojiano na televisheni ya India, Lavrov aliulizwa ikiwa Urusi inazingatia matumizi ya silaha za nyuklia.

"Silaha za kawaida tu," alijibu.

Maafisa wa Ukraine hivi karibuni wamezionya nchi za Magharibi kuhusu uwezekano wa Moscow kutumia silaha za nyuklia za kimbinu.

Mwanzoni mwa vita, Rais wa Urusi Vladimir Putin aliamuru vikosi vya ulinzi wa Urusi [vinavyojumuisha silaha za nyuklia] viwekwe katika hali ya tahadhari, na baadhi ya maafisa wa serikali ya Urusi wamedokeza kuwa nchi hiyo itakuwa tayari kuzitumia chini ya hali fulani.

línea

Uchambuzi

Baadhi ya vikosi mahiri vya Ukraine vinapigana eneo la mashariki, lakini idadi yao ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya mahasimu wao.

Urusi ina hadi wapiganaji 76 hodari katika vikosi kadhaa vinavyopigana Ukraine. Vikosi hivyo vina hadi wanajeshi 1,000 ambao wanaelekeza mashambulizi yao eneo la mashariki. Wana uwezo mkubwa wa upigaji risasi na mashambulizi ya anga.

Ukraine imesema ili kuwa na nafasi yoyote ya kujilinda katika shambulio hili kubwa, inahitaji "vifaa vizito, silaha, makombora ya Starstreak, makombora ya vifaru na vitengo vya ulinzi wa anga."

Moscow inafahamu vyema jambo hili na imeanza kushambulia njia za usambazaji ambapo rasilimali hizi zinatoka: kutoka Poland, Slovakia na nchi nyingine za NATO.

Kusambaza tena vikosi vya jeshi la Ukraine vilivyoshindwa kwa wakati ili wajilinde dhidi ya shambulio hili ni mikimbio dhidi ya wakati.

Hili linaweza kuisha kwa njia yoyote ile, na hata kama wangeishinda Urusi katika vita vichache vilivyofuata, hatari hiyo bado isingeondolewa. Ninaogopa vita hii ina wakati zaidi uliobaki.

línea

Nini kimefanyika ardhini?

Mwandishi wa BBC Jonathan Beale anaripoti kuwa mashambulizi ya Urusi yameongezeka siku ya Jumanne.

"Mashambulio haya ya mizinga ya Urusi yamekuwa yakiendelea kwa muda bilia kusitishwa. Bila shaka ni wazi, oparesheni hizi zimeundwa kudhoofisha sio tu ulinzi wa Ukraine, lakini pia kudhoofisha idadi ya watu huko. Kwa sababu, kile Urusi inasema, sio tu kushambulia malengo ya kijeshi, pia inalenga raia. Tuliiona katika kituo cha treni cha Kramatorsk mapema mwezi huu," alisema.

Akiripoti kutoka kwa Dnipro, Beale anabainisha kuwa vikosi vya Moscow vinatumia mashambulizi haya kupima ulinzi wa Ukraine kutafuta sehemu dhaifu.

Mwanjeshi wa Ukraine akichimba mtaro katika eneo la Donetsk,

Chanzo cha picha, PA Media

"Kumbuka, Waukraine wamejikita kuzunguka eneo hili. Wamekuwa wakipambana na watu wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi kwa miaka minane iliyopita. Wamechimba mitaro na wapo katika inayolindwa vyema," anaeleza.

Katika hatua hii ya kwanza, vikosi vya Urusi vimepata angalau mafanikio machache muhimu kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Kreminna, mji wenye watu wapatao 8,000 katika mkoa wa Luhansk.

Maafisa wa eneo hilo wamesema vikosi vya Ukraine viliondoka katika eneo hilo ili kujipanga upya baada ya Moscow kuudhibiti mji huo siku ya Jumatatu. Mapigano yaliripotiw akatika mitaa ya mji huo Jumanne.

Mashambulia kadhaa ya maroketi pia yameripotiwa katika mji wa Kramatorsk.

Makundi yaliyojitenga na yanayounga mkono Urusi yalipata hasara kubwa kufuatia kifo cha Mikhail Kishchik, kamanda wa moja wa vikosi vyao mashariki mwa Ukraine.

Waziri Mkuu wa nchi inayojiita Jamhuri ya watu wa Luhansk (LNR), Sergei Kozlov, aliandika kwenye mtandao wa kijamii: "Habari za kusikitisha kutoka uwanhja wa makabiliano. Mzalendo wa LNR, Luteni Kanali Mikhail Kishchik, amefariki." .

Kozlov aliongeza kuwa Kishchik na wenzake walikuwa wamezingirwa na vikosi vya Ukraine karibu na Kreminna na kudai kwamba "alipigana hadi mwisho".