Uchaguzi wa Ujerumani : Wapiga kura kuamua atakayewaongoza baada ya Merkel.

Misururu ya wapiga kura iliripotiwa nje ya vituo vya kupigia kura mjini Berlin wakati Wajerumani walipokuwa wakiendelea kupiga kura

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Misururu ya wapiga kura iliripotiwa nje ya vituo vya kupigia kura mjini Berlin wakati Wajerumani walipokuwa wakiendele kupiga kura

Kinyang'anyiro cha kuamua ni nani atakayemrithi Kansela wa Ujerumani, maarufu na ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi Angela Merkel kinaweza kuwa kikali huku Wajerumani wakianza uchaguzi wa wabunge hii leo.

Mitaa ya mji mkuu Berlin inakaribisha mashindano yam bio za marathoni za mwaka , lakini mpambano mkuu wa uchaguzi unafanyika kote nchini Ujerumani.

Angela Merkel amekuwa akionekana kwenye mikutano ya kampeni na Armin Laschet katika wiki iliyopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Angela Merkel amekuwa akionekana kwenye mikutano ya kampeni na Armin Laschet katika wiki iliyopita

Katika hatua za mwisho za kuwashawishi watu kupiga kura, Kansela anayeondoka madarakani alijiunga na mgombea kutoka chama cha conservative Armin Laschet katika mkutano wa kisasa Jumamosi katika mji wa kwao wa Aachen.

Kura za mwisho za maoni zinaonyesha kuwa huenda wasipate ushindi.

Zaidi ya Wajerumani milioni 60 wenye umri wa miaka 18 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo

Maelezo ya video, Angela Merkel:Ujerumani itamkumbuka vipi kansela huyu?

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi Jumapili, na vituo hivyo vinatarajiwa kufungwa sa kumi na mbili jioni.

Uchaguzi haukutabirika hadi pale Bi Merke alipoingia katika cheo cha juu kabisa cha kisiasa cha Ujerumani ambapo muda wake unafikia ukingoni.

"Suala la nani yuko mamlakani muhimu kusema ukweli," aliwaonya wapiga kura mara mbili katika kipindi cha saa 48 kabla ya uchaguzi kuanza. Ujumbe wake ulikuwa kwamba Ujerumani inahitaji utulivu na hali yake ya baadaye inawahijtaji vijana - na ni Armin Laschet ndiye mtu atakayewapatia hilo.

Huku wakimbiaji 25,000 rwakishiriki katika mbio za marathini za Berlin, mbio kubwa zaidi za kisiasa zinaendelea kote katika majimbo 16 ya Ujerumani.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huku wakimbiaji 25,000 rwakishiriki katika mbio za marathini za Berlin, mbio kubwa zaidi za kisiasa zinaendelea kote katika majimbo 16 ya Ujerumani.

Ubashiri wote haukuwa sahihi

Kuna mambo mengi ambayo sio ya uhakika kuhusu uchaguzi huu. Katika awamu ya kwanza zaidi ya robo tatu ya wapigakura hawakuw ana uhakika ni nani wa kumpigia kura, ingawa tayari idadi kubwa ya wapiga kura wamepiga kura zao

Kwa miezi kadhaa kura za maoni zimekuwa zikitoa matokeo tfauti, Chama cha Wahafidhina cha CDU na washirika wake wa chama cha Bavaria awali viliongoza kwa kura za maoni na wakati mmoja kile cha kijani- Green, kiliongoza, lakini baadaye kile cha Social Democrats cha Olaf Scholz kikaongoza.

Hotuba za Kansela Mekel za kila mwaka kati ya mwaka 2005 na 2019: Enzi ya Bi Merkel inakamilika mwishoi mwa mwak 2021.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Picha za hotuba za kila mwaka za Kansela Mekel kati ya mwaka 2005 na 2019: Enzi ya Bi Merkel inakamilika mwishoi mwa mwaka 2021.

Kwa wagombea wote watatu wanaopambania wadhifa Kansela ni Bw Scholz ambaye amewasisimua zaidi wapiga kura. Kama Naibu wa Bi Merkel imekuwa rahisi kwake kuliko hasimu wake Muhafidhina kuonekana kama mgombea anayeweza kuendeleza masuala ya kitaifa.

Lakini hata kama atashinda huenda akahitaji uungaji mkono wa vyama vingine viwili kuunda Muungano.