Angela Merkel: Wataalamu wanne wanachambua heshima atakayoiacha

Angela Merkel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Angela Merkel anamaliza muda wake wa utawala baada ya miaka

Wajerumani watapiga kura siku ya Jumapili katika uchaguzi ambao utakamilisha muhula wa mwisho wa Angela Merkel kama kansela wa Ujerumani.

Wakati Bi. Merkel anaondoka madarakani baada ya kushikilia usukani huo kwa miaka 16, je historia itamkumbukaje?

Tumewahoji wataalamu wanne kutathmini namna yake ya uongozi.

Merkel ataacha heshima gani kubwa kama kansela?

Merkel amebadilisha siasa za Ujerumani kujadili sera zaidi ya siasa anasema Matt Qvortrup, profesa wa siasa ya sayansi kutoka chuo kikuu cha Coventry na mwandishi wa kitabu cha Angela Merkel cha viongozi wenye ushawishi ulaya..

Siasa ya Ujerumani ilikuwa imetawaliwa na wanaume yaani kama klabu cha wanaume.

Lakini chini ya uongozi wa Bi. Merkel, mambo yameenda kisera zaidi.

Tatizo la hilo, nadhani, ni kwasababu muongozo huo umekuwa kiufundi na kisayansi. Bi. Merkel alipata mafunzo kama mwanasayansi na hivyo mtu kama yeye anatumia njia ambazo zina msingi wa ukweli.

German Chancellor Angela Merkel looks through a microscope

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi. Merkel ni mwanasayansi na aliwahi kufanya kazi kama mtafiti wa sayansi

Lakini hicho sio kile kinachomtambulisha bali namna yake ya utendaji kazi na jinsi alivyoleta mabadiliko katika siasa ya Ujerumani na siasa dunia kwa ujumla.

Kuna wakati siasa inakuwa muongozo mzuri, alijaribu kwa kuondoa baadhi ya mambo.

Charlotte Galpin: Mhadhiri wa siasa za Ujerumani na Ulaya katika chuo kikuu cha Birmingham

Bi. Merkel amekuwa akitajwa katika jarida la Forbes kuwa mwanamke mwenye nguvu sana duniani tena kwa miaka 10 mfululizo. Kuna kizazi cha Ujerumani ambacho hakijashuhudia uongozi wowote zaidi ya uongozi wa mwanamke.

Nafasi yake imekuwa ikiwakilisha umuhimu wa nafasi ya mwanamke na anajulikana kwa kuwaweka wanawake katika nafasi muhimu.

Kwa mfano, aliunga mkono Ursula von der Leyen, kuwa waziri wa kwanza wa ulinzi mwanamke nchini Ujerumani na rais wa Tume ya Ulaya.

European Commission President Ursula von der Leyen sits next to German Chancellor Angela Merkel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi. Merkel, akiwa na Ursula von der Leyen

Ingawa, uwakilishi huo haumaanishi moja kwa moja kwamba kulikuwa na mabadiliko makubwa, haswa kwa wanawake wasio wazungu na jamii ya wapenzi wa jinsia moja.

Suala la kulengwa kwa wanawake wa kiislamu na kampeni dhidi ya kile kilichotajwa kuwa uendawazimu wa jinsia kuenea eneo kubwa la Ujerumani ,kulipelekea chama kingine kuanzishwa cha mlengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD) .

Uchaguzi huu unakuja na mzunguko, katika masuala la jinsia -suala la lugha sahihi kuwekwa kisiasa , jambo ambalo bi Merkel alilikalia kimya kwa muda mrefu.

Dr Rüdiger Schmitt-Beck: Profesa wa sayansi na siasa ya kijamiikatika chuo kikuu cha Mannheim

Sera zake ndio urithi atakaouacha ambao umechanganyika na siasa za kushangaza.

Masuala mengi ya kisasa - kama ndoa ya jinsia moja, nishati ya nyuklia, na kukaribisha sera za uhamiaji - zisingetarajiwa kutoka kwa kansela wa chama cha Christian Democrats .

Hata hivyo nchi hiyo iko nyuma kwa masuala makubwa, kama ya kidigitali, sera za mabadiliko ya tabia nchi, na mabadiliko ya idadi ya watu.

Supporters of the AfD political party protest against German Chancellor Angela Merkel's liberal policy towards taking in migrants and refugees

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chama cha AfD kilipinga sera alizoweka Merkel dhidi ya wahamiaji na wakimbizi

Wakati Angela Merkel anaondoka madarakani wakati mazingira ya kisiasa yakiwa si mazuri . Hii inaleta hofu kwa kiasi fulani kuwa mfumo wa chama unazidi kuwa mgumu na chama cha AfD ambacho ,kinapinga sera ya uhamiaji.

Kuna chanzo, ukweli ni kuwa alikuwa kansela wa kwanza mwanamke. Nina uhakika mtindo wake wa kuongoza kwa busara utakuwa mfano wa kuigwa kwa mrithi wake yeyote atakayechaguliwa.

Kwa hilo ameweza kuaminiwa sana na washirika wa kimataifa.

Dk Katrin Schreiter:Mhadhiri wa masomo ya Kijerumani na Ulaya katika chuo cha Kings huko London

Yeye anadhani kuwa kiongozi mkuu wa Ujerumani anayemaliza muhula wake wa mwisho hakuweza kufanikisha baadhi ya mambo.

Uongozi wake ulikuwa unakosolewa vikali kwa kukosa maono. Lakini watu waliendelea kumpigia kura.

Anasema Merkel amekuwa na uwezo mkubwa uliomtambulisha na kuvutia mataifa mengi hasa linapokuja na suala ya kusimamia uchaguzi.

France's President Emmanuel Macron and Germany's Chancellor Angela Merkel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi. Merkel aliweka uhusiano wa karibu na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Jambo lingine la kukumbukwa analoliacha ni kwamba aliiweka ajenda ya chama chake cha Christian Democrats.

Alifanikiwa kusogeza wahafidhina karibu na wale wa mrengo wa kushoto wa Greens ambao ndio walikuwa wakosoaji wakubwa wa serikali yake.

Short presentational grey line

Mambo gani ni ya kuvutia kipindi akiwa kwenye nafasi yake ya Ukansela?

Matt Qvortrup: Anaamini kuwa alikuwa ni nguzo kubwa ya kunusuru uchumi hasa kwenye kipindi ambacho Euro ilikuwa inaporomoka mwaka 2008.

Nakumbuka kuzungumza nae tukiwa Brussels. Hasa kuhusu changamoto hiyo, alisema kuwa ikiwa uchumi wa masoko utawezekana basi ndio itanusuru changamoto hiyo, lakini cha kushangaza kulikuwa na muingiliano uliokwamisha mpango huo.Wakati wa pili mgumu kwake ni pale anasema ni mwaka Trump alipokuwa Rais.

Alihakikisha hatetereki kutetea siasa zake za ujamaa wa kimataifa.

German Chancellor Angela Merkel deliberates with US president Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi. Merkel alikuwa na misukosuko na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimshawishi kugombea muhula wa nne.

Mara tu baada ya Trump kushinda uchaguzi, Bw. Obama alisafiri kwa ndege kwenda Berlin kukutana na Bi. Merkel.Baada ya kuonana na Rais Obama alijihisi hakuna wa kuwa karibu nae, hakuwa na matumaini kama mwanzo.

Charlotte Galpin: Moja ya jambo alilowahi kufanya Merkel ni katika kusimamia mizozo ya duniani.

Kuna muda wakimbizi kutoka mashariki ya kati walikuwa wanafika Ulaya, Markel hakusita kufungua mipaka kwa mamilioni ya wakimbizi kuingia nchini Ujerumani alikuwa na kauli yake maarufu ya "wir schaffen das" - tunaweza kudhibiti hili.

German Chancellor Angela Merkel pauses for a selfie with a migrant

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ujerumani ilikuwa na jukumu kubwa la katika janga la wakimbizi, mwaka 2015

Ujerumani ilikuwa mstari wa mbele katika kuwapa hifadhi raia wa Syria waliokuwa wamekimbia vita nchini mwao.

Licha ya kuwepo vikundi vilivyopinga wakimbizi hao wa Kiislamu kuingia Ulaya.Dkt Rüdiger Schmitt-Beck; Jambo la tatu ambalo nalikumbuka ni kuhusu tukio la Merkel pamoja na waziri wa fedha walipohutubia taifa mwaka 2008 waliwahakikishia wananchi wake kuwa wataimarisha uchumi hasa kwenye kipindi ambacho kilikuwa kigumu kwa serikali ya Ujerumani.

Makubaliano aliyoingia mataifa ya Ulaya mojawapo ikiwa lile la kuiombea Ugiriki kupunguziwa deni baada ya Euro kutetereka.

Maamuzi ya Merkel ya mwaka 2015 ya kutokufunga mipaka kwa wakimbizi walikokuwa wakipita nchini Hungary.

Dkt Katrin Schreiter:Anaeleza kuwa jambo lingine ni la mwaka 2017 aliposhawishi wabunge kuruhusu ndoa ya jinsia moja.

Kabla ya uchaguzi mkuu, alitoa hotuba yake kwenye Jarida la wanawake. Ambapo alisema kuwa kuchaguliwa ni maamuzi kwa anapiga kura.

Two women are wrapped into a rainbow flag as they attend an LGBT rally in Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapenzi wa jinsia moja wametambuliwa tangu mwaka 2017

Miongoni mwa nukuu zangu za awali ambazo nilizipenda.

Mara tu alipoulizwa kuhusu kujisikia vipi anapofikiria kuhusu Ujerumani, alisema: "Nadhani madirisha yamefungwa vizuri sana, na hakuna taifa lingine ambalo linaweza kutengeneza na kufunga madirisha vizuri .

Hiyo inaonesha unyenyekevu wake.