Tetesi za soka Jumatano: Arsenal wanamtaka Brandt

Brandt

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wana shauku ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Brandt, 29, mkataba wake wa Borussia Dortmund utakapomalizika msimu huu wa joto. (Metro),

Manchester United, Arsenal na Chelsea zote zina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Freiburg, Johan Manzambi, 20, kutoka Uswizi. (Teamtalk)

Hata hivyo, Arsenal wameachana na nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Italia wa Newcastle, Sandro Tonali, 25. (Chronicle)

Tonali

Chanzo cha picha, Getty Images

Kurudi Serie A pia kunaonekana kutokuwa rahisi kwa Tonali baada ya Newcastle kuweka bei ya pauni milioni 77 (euro 90) kwa mchezaji huyo, ambayo itaifanya Juventus ishindwe, lakini Manchester United na Manchester City bado wana nia naye. (Matteo Moretto )

Juventus wameanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Manchester City, Mreno, Bernardo Silva, kuhusu uhamisho wakati mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 31 utakapomalizika, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vikiwemo Galatasaray na Inter Miami. (Gazzetta dello Sport)

Brighton wana uhakika wa kuishinda Chelsea katika usajili wa majira ya joto wa winga wa Cologne Mjerumani Said el Mala, 19, ambaye amevutia katika msimu wake wa kwanza kwenye Bundesliga. (Football Insider)

Said el Mala

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea hawataki kumuuza mshambuliaji Liam Delap msimu huu wa joto licha ya Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 23 kufunga bao moja tu la Ligi Kuu katika msimu ulioathiriwa na jeraha. (Mirror)

Liverpool inabaki sokoni kwa msimu huu wa joto na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani wa Eintracht Frankfurt Nnamdi Collins anakilengwa, huku Arsenal pia ikimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Barcelona wanapanga mbadala wa Marcus Rashford ikiwa hawataweza kukubaliana kuhusu mpango wa kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 kutoka Manchester United kuwa wa kudumu. (Marca)

Marcus Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Millwall, Femi Azeez, huku Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 24 akifuatiliwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ikiwa ni pamoja na Everton na Brentford. (Teamtalk)

Tottenham, Crystal Palace na Manchester United zote zinavutiwa na meneja wa Bournemouth Andoni Iraola. Mkataba wa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 43 unaisha mwishoni mwa msimu. (i paper)