Kutoka Gaddafi hadi Khamenei: Kile anachosema Putin na asichosema baada ya kuuawa kwa washirika wake

Chanzo cha picha, DMITRY AZAROV/SPUTNIK/AFP via Getty Images
Mnamo tarehe 28 Februari, Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, aliuawa katika mashambulizi ya pamoja ya Israeli na Marekani. Siku iliyofuata, Bwana Putin alielezea kitendo hicho kama "uwasilishaji wa ugaidi" na "ukiuki wa wazi wa kanuni zote za maadili ya binadamu na sheria za kimataifa."
Lakini hakusema ni nani aliyefanya kitendo hicho. Ujumbe wake wa rambirambi kwa Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, haukutaja Marekani au Israeli.
Mnamo Januari 2025, Urusi na Iran walisaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati, lakini makubaliano hayo hayawatii Urusi kutoa msaada wa kijeshi ikiwa Iran itaangukia shambulio. Hii ni kwa sababu mkataba huo haukujumuisha kifungu cha ulinzi wa pamoja kinachowawezesha pande zote kutoa msaada wa kijeshi kwa upande mwingine. Mamlaka ya Urusi pia imesema kuwa Iran hakuwa ameomba msaada wa kijeshi kutoka Urusi, na mkataba huo haufungi Urusi kushiriki kimilitari moja kwa moja kwa ajili ya kuilinda Iran
Mnamo Juni 2025, wakati Marekani ililipua miundombinu ya nyuklia ya Iran, Bw. Putin aliiita "uvamizi usiohitajika kabisa dhidi ya Iran" ambao "haukuwa na msingi au haki," lakini tena hakumtaja Marekani kwa jina.
"Alapoulizwa kinachotokea ikiwa Marekani na Israel wangemuua Ali Khamenei, Putin alijibu: 'Sikatai hata kuzungumza kuhusu hilo.'"
"Idara ya Ufuatiliaji ya BBC imechambua maandishi yaliyoachiliwa na Kremlin na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi ili kuchunguza kauli za umma za Putin kufuatia kuanguka kwa washirika watano wa Moscow kati ya mwaka 2011 na 2026. Wakati Vladimir Putin ameweza kutaja wahalifu na mbinu katika kesi za awali, katika kesi za hivi karibuni amezungumza kidogo au kubaki kimya kabisa."
"Gaddafi na Yanukovych; maalum na ya kibinafsi"
Baada ya kuuawa kwa Muammar Gaddafi wa Libya mwezi Oktoba mwaka wa 2011, Putin alizungumza kwa kipana na urefu.
Alisema ndege zisizo na rubani zilizomlenga Gaddafi na majeshi ya kigeni yaliyokuwa huko "hawakufaa kuwa huko"
Alisema mauaji hayo yanakiuka sheria za kimataifa na kutoa wito kwa Umoja wa mataifa kuingilia kati.
Putin pia alizungumzia kuondolewa madarakani kwa Viktor Yanukovych, rais wa zamani wa Ukraine aliyeondoloewa madarakani mwezi Februari mwaka wa 2014.
Akiwahutubia wanahabri mwezi Machi 2014, aliwataja mawaziri wa mambo ya kigeni wa Poland, Ujerumani, Ufaransa kuwa walishirikiana na upinzani kumuondoa madarakani rais huyo wa zamani wa Ukraine.
idha Putin aliongezea kuwa alimsaidia Yanukovych kukimbilia eneo la Crimea.
Katika miaka iliyofuata Putin alizidi kuishambulia Marekani kwa kufanya mapinduzi nchini Ukraine kwa njia ya kimabavu.
Assad; Vitendo bila maneno
Baada ya kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad mwezi Disemba 2024, Urusi ilimpeleka Moscow, ila Putin hakuwakashifu wala kuwataja waliotekeleza kitendo hicho.
Wiki mbili tu baada ya al-Assad kuwasili nchini Urusi, Putin aliwaambia wanahabari kuwa bado hajakutana na rais huyo wa zamani wa Syria. Aidha aliongezea kuwa "matukio ya hivi karibuni Syria haimaanishi Urusi imeshindwa"
Miezi kumi na mitatu baadaye, Putin alikuwa akimpongeza rais mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa kwa kuleta utulivu nchini Syria.
Maduro: Hakuna vitendo wala maneno
Mwezi Januari 2026, wakati majeshi ya Marekani yalipomkamata aliyekuwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Putin hakutoa tamko lolote hadharani.
Naibu mwenyekiti wa baraza la usalama la Ursi, Dmitry Medvedev na balozi wa Urusi kwa Umoja wa Mataifa ndiyo walikashifu hatua ya Marekani. Ila ikulu ya Kremlin haikutoa tamko lolote.
Khamenei: Alitoa tamko bila kutaja aliyetekeleza mauaji
Kinyume na kukamatwa kwa Maduro, mauaji ya Ali Khamenei yalikashifiwa vikali na Ikulu ya Kremlin, ingawa Putin hakuwataja wahusika wa mauaji hayo.
Kulingana na Alexander Baunov, mshirika mwandamizi katika Kituo cha Carnegie Berlin, anauita mfumo wa Urusi kuwa 'lugha nyingi za kisiasa'. "Wizara ya Mambo ya Nje imepewa jukumu la kutumia kauli za kukosoa Marekani, huku Kremlin ikitekeleza sera tofauti kuhusu Donald Trump."
Baunov pia anasema kwamba kauli ya Vladimir Putin kuhusu Ali Khamenei ilikuwa dhaifu zaidi hata kuliko maoni yake yasiyo rasmi baada ya kuuawa kwa Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC, katika shambulio la Marekani mwaka 2020. 'Walienda na kumuua jenerali wa Iran, wamepoteza akili kabisa,' aliwahi kusema Putin wakati huo.
Putin hakutaja jina la Trump.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ekaterina Kotrikadze, mwanahabari aliye mafichoni, anasema kwamba Vladimir Putin yuko katika hali ngumu kwa sasa. Hawezi kuishambulia Marekani waziwazi kama alivyokuwa akifanya awali, lakini kimya pia kinaonekana kama ishara ya udhaifu.
"Moja baada ya mwingine, marafiki wake wa karibu wanaangushwa, jambo ambalo ni pigo kwa Putin. Lakini hawezi kujibu kwa sababu Kremlin bado ina matumaini ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na rais wa 47 wa Marekani," alisema Kotrikadze.
Mchambuzi wa siasa Alexander Morozov, akirejelea majibu "ya tahadhari" ya Kremlin, anasema kwamba vita vya Iran vimeonyesha jinsi mbinu za vita za Putin zilivyo za zamani na kuweka Kremlin katika nafasi ngumu.
Kulingana na mchambuzi wa siasa Sergei Shelin, rais wa Urusi "sasa anamwangalia Trump kwa mtazamo tofauti" na, kutokana na shaka yake ya asili, hofu yake inaongezeka.
Mwaka 2011, Seneta wa Marekani John McCain alisema kwamba Vladimir Putin angepatwa na "hatima sawa na ile ya Gaddafi." Putin alijibu kwa kuhoji afya yake ya akili.
Maelezo kama haya hayatazamwi tena na Marekani. Lakini majibu ya Putin yamebadilika kutoka tuhuma za moja kwa moja hadi hatua ambapo hawezizitaja tena majina ya watu anao wakashifu.















