Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Juve wanamtaka Spence wa Tottenham

Chanzo cha picha, Getty Images
Djed Spence wa Tottenham anatarajiwa kuichezea Juventus, Real Madrid yamweka Mauricio Pochettino kwenye orodha ya watakaowania nafasi ya ukocha, Liverpool yafikiria kumsajili winga wa Ufaransa Moussa Diaby.
Juventus wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Tottenham na Uingereza Djed Spence, 25, msimu huu wa joto (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanafikiria kumsajili winga wa Al-Ittihad na Ufaransa Moussa Diaby, mwenye umri wa miaka 26, huku mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa akitaka kuondoka katika klabu hiyo ya Saudi Pro League msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wameazimia kumshikilia kiungo wa kati Bruno Guimaraes, 28, na wanafanya mazungumzo ya mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Caughtoffside)
Real Madrid yamweka kocha mkuu wa Marekani na kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino, kwenye orodha ya watakaowania kuchukua fursa ya Alvaro Arbeloa huko Bernabeu kabla ya msimu ujao. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United haitakimbilia kumteua kocha wa kudumu licha ya kocha wa muda Michael Carrick kuwasilisha matakwa yake. (The Athletic - usajili unahitajika)
Beki wa Newcastle na Uingereza Tino Livramento, 23, hayuko karibu kukubali kujiunga na Manchester City katika mkataba wa majira ya joto licha ya uvumi. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 27, hana mpango wa kufanya mazungumzo na Liverpool kuhusu mkataba mpya msimu huu wa joto lakini anafurahia kuwa Anfield licha ya kuhusishwa na Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Napoli inataka kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay hadi 2030 katika juhudi za kuondoa nia yoyote ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 29 msimu huu wa joto. (Il Mattino - in Italian - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa West Ham Callum Wilson amekubaliana kwa maneno kuhusu mkataba mpya wa mwaka mmoja licha ya Celtic kuvutiwa na Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 34. (Sky Sports)
Manchester City huenda wasiondoe kipengee ambacho kitamfanya kiungo mahiri wa Marekani mwenye umri wa miaka 16, Cavan Sullivan, ajiunge nao kutoka klabu ya MLS Philadelphia Union msimu ujao. (The I - subscription required)
Kuna kipengele katika makubaliano ya awali ambacho kiliruhusu City kumtoa katika klabu ya MLS mapema ikiwa angeonyesha kuwa na matokeo mazuri kwa haraka lakini kuna uwezekano mdogo hilo litafamyika.

Chanzo cha picha, Shutterstock
Kiungo wa zamani wa Tottenham Ryan Mason ndiye mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya Igor Tudor kama kocha wa muda wa Spurs. (Football Insider)
Bayer Leverkusen itazingatia mustakabali wa kocha Kasper Hjulmand mwishoni mwa msimu. (Florian Plettenberg)















