Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Wilson akubali mkataba mpya wa West Ham

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Callum Wilson akubali kusalia West Ham, Ibrahim Sangare aongezwa kwenye orodha ya wanaowindwa na Manchester United na Manchester City yakaribia kumsajili Tino Livramento.

Mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 34, amekubali mkataba mpya wa mwaka mmoja na West Ham wiki chache tu baada ya kuonekana kuwa mwenye kuondoka hivi karibu. (Telegraph - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United imemuongeza kiungo wa Nottingham Forest wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, 28, kwenye orodha ya wachezaji inaowataka wajiunge nao msimu huu wa joto. (CaughtOffside)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City inakaribia kumsajili beki wa pembeni wa Newcastle United, Tino Livramento, 23. (Football Insider)

Newcastle waonyesha nia thabiti ya kumsajili kiungo mahiri wa Uingereza Marcus Tavernier, 26, kutoka Bournemouth. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wachunguzi wa Real Madrid walimtazama kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali, 25, akiwa uwanjani, wakati timu yake ya Newcastle ilipotolewa kwenye Kombe la FA na Manchester City siku ya Jumamosi. (Sun)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Andy Robertson wa Liverpool anasema mazungumzo kuhusu mustakabali wake hayatatangazwa hadharani baada ya beki huyo wa kushoto wa Scotland, 31, kukaribia kujiunga na Tottenham mnamo mwezi Januari. (Athletic - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wako kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, mwenye umri wa miaka 31. (Christian Falk)

Winga wa Ujerumani Julian Brandt, 29, ataondoka Borussia Dortmund kwa uhamisho wa bila malipo mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

RB Leipzig wamekubaliana kuhusu masharti binafsi na kiungo mkabaji wa Borussia Monchengladbach Rocco Reitz, huku vilabu hivyo viwili vikiwa katika mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23. (Florian Plettenberg)

Imetafsiriwa na Asha Juma