Msanii wa vipodozi Kabul: 'Wanawake kama mimi ni walengwa wa Taliban

A woman in a burkha walks past a shop where posters of models are covered over

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sura zilizopakwa rangi nyeusi nje ya saluni mjini

Katika siku ambayo Taliban ilichukua udhibiti wa mji mkuu wa Afghanistan Kabul, mabango ya matangazo nje ya urembo yanayoonesha mavazi ya bibi harusi yalichorwa kila mahali.

Saluni katika maeneo ya jiji zilifungwa pia. Wakati baadhi ya biashara zikiwa zimeapa kuendelea kama kawaida haraka, baadhi wakihofia hali yao ya baadaye.

Afsoon (sio jina lake), msanii wa vipodozi aliyejificha, anaelezea jinsi sekta ya urembo imekuwa ya maana kwa wanawake wa Afghanistan.

Ni vigumu kutafsiri maana halisi ya kauli ya Dari takaan khordum kwa lugha nyingine.

Kwa tafsiri ya haraka tunaweza kusema inaelezea tukio la nadra ambalo linatikisa msingi wako, ambapo baada yake utakuwa umebadilika kabisa- kama kifo cha mtu unayempenda, mtu ambaye ni nguzo ya maisha yako.

Uzoefu wa Afsoon na hisia za takaan alizipata kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti 2021.

Jumapili asubuhi 4:00 aliamshwa na simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzake wa saluni ambako alikuwa akifanyia kazi. Afsoon alikuwa katika kipindi cha furaha zaidi, akinukia shampuu zenye harufu nzuri za manukato na kupaka mchangantiko wa rangi za kucha za wateja wake.

"Usije leo kazini ," mfanyakazi mwenzake Afsoon alimwambia alipopiga picha . "Tunafunga. Ni mwisho."

Akiwa ameketi kwenye kitanda chake, Afsoon aliitazama simu yake ya mkononi. Kidole gumba chake kiliinuka juu na chini ya skrini huku akitazama makumi ya jumbe kutoka kwa marafiki zake na familia na halafu akatazama mamia kadhaa ya jumbe za mitandao ya kijamii.

Alijihisi kama ameshikwa na ganzi na mwenye msukumo wa aina fulani kiasi kwamba alihisi baridi kali mwilini na akajihisi mgonjwa wakati ule.

Jumbe zote zilikuwa sawa. Taliban wameingia katika mji mkuu Kabul.

Katika kipindi cha siku 16 majeshi ya magharibi na wanadiplomasia wao walikuwa wameondoka kuelekea makwao.

"imekwisha " alijirudia mwenyewe. Ulikuwa ni muda wa kujificha.

A poster of a bride with her eyes and mouth painted over

Chanzo cha picha, Getty Images

Afsoon ana umri wa miaka tarkiban 25 na anajiona kama mwanamke wa kisasa wa Afghanistan.

Anapenda mitandao ya kijamii, anapenda filamu , anaweza kuendesha gari na ana malengo na matamanio yake ya kikazi.

Afsoon hawezi kukumbuka miaka ya 90, muongo aliozaliwa, wakati kwa mara ya kwanza Taliban walipopiga marufuku saluni za urembo nchini humo.

Lakini alikulia Afghanistan ambako maduka ya urembo yalikuwa ni sehemu ya maisha yake.

Katika miongo miwili tangu uvamizi ulioongozwa na Marekani ambao uliondosha Taliban katika mwaka 2001, zaidi ya saluni 200 zilifunguliwa katika mji wa Kabul pekee, huku mamia kadhaa ya saluni zikifunguliwa katika maeneo mengine ya nchi.

Kama msichana mwenye umri wa kubalehe alikuwa akirambaza kwenye majarida na mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuangalia mionekano ya urembo, na alikuwa akitembelea saluni na wanawake katika familia yake kupodolewa.

Alipenda sana kila kitu kuhusu saluni na urembo kwa ujumla.

Kucha zilizopakwa rangi mbali mbali, msanii huyu wa vipodozi aliinama kuwapaka rangi za kope, na mapodozi mengine ya uso wanawake na kuzifanya sura zao kung'aa na kuwa zenye mvuto huku akiwatengenezea mitindo tofauti ya nywele.

Hatimaye Afsoon alitimiza ndoto yake ya kufanya kazi kama mmoja wa wasanii wenye mafanikio zaidi wa vipodozi. Hakuna kitu kingine chochote alichokitaka zaidi.

Sawa na maduka ya urembo mjini Kabul, saluni ya Afsoon ilikuwa na madirisha ambayo yalikuwa yamefunikwa na mabango ya wanawake warembo ambayo kwa kawaida hutumiwa kutangaza biashara ya saluni.

Picha hizo zilimaanisha kwamba mpitanjia katika mitaa ambayo hupitiwa zaidi na wanaume ya Kabul angeweza kuangalia ndani ya saluni yake.

Wakati wote kulikuwa na zaidi ya wanawake kumi na mbili ndani yake, wawe ni wanamitindo au wateja-ambao walikuwa ni tofauti kuanzia madaktari hadi waandishi wa habari, kuanzia wanamuziki na nyota wa televisheni hadi maharusi waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya siku kuu yao pamoja an wasichana wadogo waliokuwa wakiambatana na mama zao.

Biashara ilikuwa inashamiri kila siku, iwe harusi au watu waliotaka kujipendezesha tu na saluni ilikuwa na shuguli nyingi nyakati za sherehe kama vile Idd ,kwa siku hizo ilibidi watu wajisajiri siku nyingi kabla ili waweze kuhudumiwa.

" Nawapenda wanawake. Nilitaka kufanya kazi na kujenga mahali ambapo wanawake wangehisi kuwa huru na kupendeza," Afsoona asema. "Tulikuwa tunapumzika katika mahala ambapo tulikuwa mbali na wanaume."

Lakini Jumapili tarehe 15 Agosti Taliban ilichukua udhibiti wa kasri ya rais, miaka yake ngumu ya miaka ikaisha kwa siku moja.

An Afghan female model with make-up of the Afghanistan flag painted on her face

Chanzo cha picha, Nilab Adelyar

Maelezo ya picha, Picha: Wasanii wa vipodozi raia wa Afghanistan wanaoishi nje ya nchi-kama vile mshawishi wa urembo anayeishi Canada Nilab Adelyar - amekuwa akionesha mshikamano na wanawake wanaofanya kazi hii.

Ni takriban saa sita usiku mjini Kabul na Afsoon anaongea nasi kwa sauti ya chini kwa simu. Anaogopa sana . Aliondoka nyumbani kwao siku ile ya Jumapili na kupata nyumba salama.

"Wanawake katika sekta ya urembo, hususan kama mimi ambao walikuwa wanaonekana kwa umma na watu na kazi yetu ni walengwa ," anasema.

Baada ya siku kutoka kwa rafiki yake akimwambia asije kazini , Afsoon alisikia kwamba picha yoyote yenye matangazo linalowakilisha urembo wa mwanamke lilikuwa linapakwa rangi juu na wakazi wenye uoga.

Rafiki yake Afsoon alipaka rangi juu ya picha yake kama mwanamitindo, kama ishara ya kuwafurahisha Taliban ili kuwaepusha rafiki zake za kike waliokuwa na biashara za urembo.

"Hakuna njia ambayo wangeidhinisha sura abazo hazijafunikwa kwa vilemba, au kuonekana kwa shingo za wanawake ," anasema. "Wamekuwa wazi kila mara kuhusu Imani yao kwamba mwanamke hapaswi kuwa wa kuvutia.

"Ni mwisho wa sekta ya urembo nchini Afghanistan."

A billboard poster on which the face of a woman has been scratched out

Chanzo cha picha, Getty Images

Afsoon hana mwaliko au karatasi ambayo ingemuwezesha kupata fursa ya kukaa katika ndege ili kuondoka Kabul.

Hana njia ya kuondoka.

Anawasiliana na wenzake katika kikundi cha mawasiliano. Malipo ya mwisho waliyoyapata yalikuwa ni ya tarehe 24 Agosti. Hakuna mshahara mwingine watakaoupata sasa. Saluni imefungwa wote wamekubali kuwa hawatarejea tena kazini.

Afsoon hawezi kuzungumza kuhusu hali yake ya baadaye, anasema.

Nini kitakachofuata, hana uhakikia. Hajafikiria jinsi atakavyovaa sasa, au hata ni lini atatembea nje.

Kwa sasa, rangi ya siku zijazo aliyoifikiria imepakwa rangi nyeusi juu yake, na yuko katika mshituko ambao haujulikani ataupona lini.

"Kuwa hai ni jambo pekee ninaloweza kufikiria juu yake. Siogopi kufa-lakini sio kama hivi-kuogopa na kutokuwa na matumaini ," anasema.

"Kila dakika nahisi kama Taliban watanijia ."

Taarifa zaidi kuhusu wanawake nchini Afghanstan:

Afghan woman

Chanzo cha picha, Getty Images

Afghanistan imetajwa kuwa eneo hatari zaidi duniani kwa wanawake. Utafiti mmoja unasema 87% ya wanawake nchini humo hupitia unyanyasaji wa aina moja au nyingine wa kingumbani.