Birtukan Mideksa: Mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi wa Ethiopia

Birtukan Mideksa speaks to media after the handover ceremony at the Parliament in Addis Ababa, Ethiopia on November 22, 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Mfungwa wa zamani wa kisiasa ambaye alikimbilia uhamishoni Marekani, Birtukan Mideksa sasa ndiye anayesimamia uchaguzi wa kwanza wa ubunge Ethiopia, tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipoingia madarakani mwaka 2018 kwa ahadi ya kumaliza miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu.

Akimpendekeza Bi Birtukan, 47, katika nafasi muhimu ya uwenyekiti wa bodi ya uchaguzi, Waziri Mkuu alimuelezea kama mtu ambaye "kamwe hatashurutishwa na hata serikali, kutekeleza majukumu yake".

Wengi walikubaliana na kauli hiyo kwani amejijengea hadhi ya kuwa mtu mkakamavu na mwenye misimamo akiwa Wakili, Jaji na Mwanasiasa.

Chama cha People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF), kilikubali kushindwa kwake kulitokana na "umaarufu mdogo" na wala sio kuibiwa kura.

Baadaye alikuwa jaji, ambapo aligonga vichwa vya habari mwaka mmoja baadaye kwa kukataa muingilio wa kisiasaa katika idara ya mahakama na kuagiza kuachiliwa mara moja wa waziri wa zamani wa ulinzi Siye Abraha.

Kukamatwa kwake na kufunguliwa kwa mashtaka ya ufisadi dhidi yake kulionekana kama jaribio la kuvunja ushawishi wa upinzani ambao ulikua tisho kwa Waziri Mkuu wa wakati huo Meles Zenawi.

Kesi ya "Siyes' ndio iliyoangaziwa. Lakini wote [ Bi Birtukan na majajji wengine ]walijaribu kukabiliana na utawala wa nchi hiyo kimya kimya ," alisema rafiki yake, ambaye hakutaka jina litajwe.

Meles Zenawi alituhumiwa kwa kuongoza Ethiopia kwa mkono wa chuma (kimabavu)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meles Zenawi alituhumiwa kwa kuongoza Ethiopia kwa mkono wa chuma (kimabavu)

Kutokana na uchu wa kutaka mabdiliko, Bi Birtukan alirejea tena katika ulingo wa siasa, akishikilia nafasi muhimu katika uundaji wa Muungano wa Umoja na Demikrasia (CUD) kukabiliana na chama cha EPRDF katika uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2005, ambao ulionekana na wengi kuwa uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali katika historia ya Ethiopia, upinzani ukidai kuibiwa ushindi.

Kama afisa wa ngazi ya juu wa CUD, Bila shaka Bi Birtukan alilengwa na vikosi vya usalama na alikua miongoni mwa maelfu ya watu waliozuiliwa katika msako uliofanywa baada ya uchaguzi. Polisi waliwapiga risasi karibu wa 200.

Kushtakiwa na rafiki

Mtandao wa chini kwa chini kwa chini uliokuwa umebuniwa na CUD ulivunjwa, lakini kutoka ndani ya jela, viongozi wake - akiwemo Bi Birtukan - waliufufua tena na kuupatia jina la Baraza la Kimataifa la Kinjit (KIC), kuhamasisha msaada kwa kampeni ya kupigania demokrasia.

"Walikuwa wakijadili na kufanya uamuzi wakiwa njiani kueleka mahakamani," alisema rafiki wa Bi Birtukan, ambaye hakutaka kjinalake litajwe.

Picha hii iliyopigwa Juni 17, 2021 inamuonesha mfanyakazi wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi akiwaelezea watu jinsi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Juni 21, 2021

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu milioni 37walijiandikisha kupiga kura, amaafisa wanasema

Mnamo 2006, Bibi Birtukan alikuwa miongoni mwa wafungwa wengi - akiwemo mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu nchini Ethiopia, Daniel Bekele - ambaye alishtakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na uhaini.

Birtukan Mideksa, chairperson of Election Board of Ethiopia, announces the results of a referendum regarding the new federal region of Sidama in Hawassa about 200km south of capital city of Addis Ababa, on November 23, 2019

Chanzo cha picha, AFP

Walipigwa na butwaa, walipogundua mmoja wa wandesha mashtaka alikuwa Shimels Kemal - rafiki wa Bi Birtukan - ambaye alimuomba jaji kuwahukumu adhabu ya kifo.

"Lilikuwa tukio la kushangaza," mmoja wa watu waliomjua, alisimulia BBC Amharic.

"Shimels hajui msamaha. Anachanganya siasa na masuala ya kibinafsi. Alijihisi kusalitiwa wakati wenzake wapoliamua kufuata mkondo mwingine wa kisiasa."

Jaji alipinga ombi la mwendesha mashtaka na badala yake kuwahukumu kifungo cha maisha.

Baada ya kulazimika kumuacha binti yake mdogo kulelewa na mama yake, Bi Birtukan alianza kuhudunmu kifungo chake katika jela hatari la Kaliti, ambako alikuwa mpatanishi kati ya pande hasimu za CUD baada ya tofauti kubwa kuibuka miongoni mwa viongozi wake.

Kura
Maelezo ya picha, Idadi ya wapiga kura, kwa mujbu wa bodi ya Taifa ya uchaguzi Ethiopia

"Hakusuluhisha tatizo lakini alifanikiwa kubuni upya mtandao wa chini kwa chini wa chama hicho" alisema rafiki yake Bi. Birtukan.

Akiwa jela, alikuwa mmoja wa wafungwa waliofanya mazungumzo na jopo la wazee ambao walifikia mwafaka kati yao na serikali.

Hatua ambayo ilichangia kuachiliwa kwao mwaka 2007 baada kuzuiliwa jela kwa miezi 18, huku Bi Birtukan akiwa miongoni mwa wale waliotia saini hati za kujutia "makosa" na kumuomba msamaha Waziri Mkuu Meles.

Uamuzi huo ulizua utata katika mrengo wa upinzani, ijapokuwa alijaribu kupuuza umuhimu wa tukio hilo katika hatuba aliyotoa akiwa ziarani nje ya nchi.

Mkuu wa polisi wa wakati huo Wokneh Gebeyehu - ambaye sasa ni katibu mtendaji Igad - alimwamuru aombe radhi, akimshtaki kwa kukiuka masharti ya msamaha wake.

Bi Birtukan alikataa kuomba msamaha, na wakati wa Krismasi ya mwaka 2008, alirudishwa tena jela kuhudumia kifungo chake cha maisha.

People hold a paper that shows a list of political parties in Addis Ababa, Ethiopia, on June 17, 2021, who are running for the upcoming June 21, 2021 elections

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mpango wa elimu ya wapiga kura umefanywa ili kupunguza hatari ya kura kuharibika

Maelezo zaidi:

People hold a paper that shows a list of political parties in Addis Ababa, Ethiopia, on June 17, 2021, who are running for the upcoming June 21, 2021 elections

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mpango wa elimu ya wapiga kura umefanywa ili kupunguza hatari ya kura kuharibika

Katika taarifa iliyochapishwa na gazeti la Addis Neger nchini Ethiopia muda mfupi kabla akamatwe tena, aliandika: "Pengine haya ndiyo maneneo yangu ya mwisho" na katika tamko hilo muhimu licha ya utata uliozunguka uamuzi wake wa kuomba msamaha, aliandika: "Nilitia saini hati hiyo. Huo ni ukweli ambao siwezi kuubadilisha, hata nikitaka kufanya hivyo."

Masharti yake mapya gerezani yalikuwa makali zaidi, na alifungiwa peke yake kwa muda wa miezi miwili, na alinyimwa hata haki ya kumuona binti yake.

Kukimbilia uhamishoni Marekani

Hatua hiyo iliongeza shinikizo kutoka kwa umma kutaka ahurumiwe. Shirika la kimataifa la kutetea haki Amnesty International lilimwita mfungwa wa dhamiri na gazeti la Mail & Guardian la Afrika Kusini likimuelezea kama mfungwa maarufu wa kisiasa nchini Ethiopia.

Oktoba mwaka 2010, Bi Birtukan aliachiliwa tena baada ya kujadili msamaha mwingine.

Kuachiliwa kwa Birtukan Mideksa mwaka 2010 ilikuwa faraja kubwa familia na marafiki zake

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kuachiliwa kwa Birtukan Mideksa mwaka 2010 ilikuwa faraja kubwa familia na marafiki zake

Baada ya kuachiliwa, yeye na binti yake walikimbilia uhamishoni nchini Marekani, ambako alisomea chuo cha Harvard Kennedy na baadaye kufanya kazi na Shirika la Marekani linalosaidia kukuza demokrasia kote duniani -National Endowment for Democracy (NED).

Alirejea nchini Ethiopia baada ya Bw. Abiy kuingia madarakani na kuahidi kukomesha miaka kadhaa ya uongozi wa kidhalimu.

Lakini furaha iliyofuatia uteuzi wake imefifia kwa kiwango fulani.

Hatimaye uchaguzi unafanika leolicha ya vyama vikuu vya upinzani kususia, vikisema hakuna mazingira ya kuendesha uchaguzi hutru na wa haki .

People hold a paper that shows a list of political parties in Addis Ababa, Ethiopia, on June 17, 2021, who are running for the upcoming June 21, 2021 elections

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mpango wa elimu ya wapiga kura umefanywa ili kupunguza hatari ya kura kuharibika

Miongoni mwa wakosoaji wa Bi. Birtukan ni Profesa Merera Gudina, ambaye amemfahamu kwa miaka 21. Anaongoza chama cha Oromo Federalist Congress (OFC), ambacho kimesusia uchaguzi.

Baada ya OFC na chama kingine kususia uchaguzi katika jimbo la Oromia, mzozo katika jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi na kuahirishwa kwa uchaguzi katika baadhi ya maeneo ya the Somali, "uchaguzi sasa unafanyika katika jimbo la Amhara na [mji mkuu ] Addis Ababa", aliongeza.

Lakini msomi wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa Mesenbet Assefa, anasema Bi. Birtukan amefanya kazi nzuri.

"Kosa sio la bodi ya [uchaguzi] au serikali. Vyama vya kisiasa vina wajibu wa kufanya kile kinachohitajika kidemokrasia - mageuzi - sio kutumia silaha kuondoa serikali madarakani."

Bi Birtukan mwenyewe ameangazia matarajio yake juu ya uchaguzi. Katika barua kwa Bunge la Seneti nchini Merekani mnamo Mei, alionya "mapungufu hayawezi kuepukika kwani ... kadri demokrasia unavyokuwa ndivyo na mazingira ya siasa na usalama inavyobadilika"