Uchaguzi mkuu Ethiopia: Je ni Fursa ya kuzaliwa upya kwa demokrasia au kuendelea kwa mizozo?

Ethiopia member

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwananchi wa Ethiopia akiwa amevaa bendera ya taifa hilo kupinga mauaji yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Ethiopia inajiandaa kufanya kile ambacho waziri mkuu wake anakieleza kama jaribio la kwanza la nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu huru na wa haki, lakini unafanyika wakati nchi hiyo ikiwa katika usalama wenye mashaka,vyama vya upinzani vikisusia uchaguzi huo na jimbo lake la Tigray ambalo sio tu kitovu cha mapigano bali liko kwenye hatari kubwa ya baa la njaa.

Kura
Maelezo ya picha, Idadi ya wapiga kura, kwa mujbu wa bodi ya Taifa ya uchaguzi Ethiopia

Uchaguzi huu unatoa picha ya hatma ya Ethiopia - nchi ambayo sio tu inahaha kujitambulisha kama taifa linalokua kiuchumi barani Afrika, lakini pia taifa linalokuwa kwa kasi kidemokrasia, kutaka kuhitimisha miongo kadhaa ya uchaguzi uliojaa udanganyifu.

Je Ethiopia inaweza kuvuka mtihani huu? na uchaguzi huu unaweza kuwa sehemu muhimu kuhusu mzozo wa Tigray wakati huu ambapo serikali inakabiliwa na mashinikizo makubwa ya kimataifa ya kusitisha mapigano katika eneo hilo?

Prosperi
Maelezo ya picha, Wafuasi wa waziri Mkuu Abiy Ahmed, wanaimani kubwa na kiongozi huyo kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Waziri mkuu kijana wa Ethiopia, Abiy Ahmed alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019, kama sehemu ya kutambua mchango wake lakini kama sehemu ya kuchagiza mabadiliko makubwa ya kimfumo nchini humo, kusaidia kupunguza ama kuondoa migogoro ya kikabilia nchini humo. Miaka miwili baadae, unaweza kuanza kuhoji kama kweli lengo la Abiy la kufanya mabadiliko nchini Ehtiopia liko kwenye muelekeo sahihi?

Hakuna shaka hata kidogo kwamba Bwana Abiy na chama chake kipya cha Prosperity kilichozaliwa kutoka chama tawala cha EPRDF, atashinda uchaguzi mkuu huo, na kumuwezesha kuwa na majukumu makubwa ya kusimamia na kutekeleza sera yake ya umoja inayofahamika kama 'tuje pamoja'' (medemer)"medemer," or "coming together". .

Makabila
Maelezo ya picha, Mgawanyo wa makabila

Chini ya kauli mbiu hiyo, Bwana Abiy anaonekana kuiondoa nchi hiyo kutoka taifa la utawala wa kikabilila chini ya EPRDF, kuwa taifa linalotawaliwa na serikali moja ya kitaifa.

Maana yake ushindi atakaoupata, ukiambatana na la lugha tamu ya ushawishi utaiweka tume ya uchaguzi ya taifa hiyo katika changamoto kubwa.

Tahadhari ya baa la njaa

Serikali ya Ethiopia inashikilia msimamo wake kwamba, kutofanyika uchaguzi katika eneo lililokumbwa na machafuko la Tigray ni jambo la bahati mbaya, licha ya kwamba eneo hilo lina viti vichache bungeni.. Jimbo hilo la Tigray litafanya uchaguzi wake pale machafuko yatakapokoma na hali ya mambo kurejea kawaida.

Jumuiya za kimataifa zimeonya kwamba, eneo hilo limekumbwa na baa la njaa, lakini serikali inasisitiza kwamba, si kweli, eneo hilo halina njaa. Lakini pia kuna wasiwasi wa hali ya usalama katika maeneo mengi ya Ethiopia - kwa mfano Afar, Somali, Amhara, Oromia, Harari, Benishangul-Gumuz, South Wollo na maeneo mengine. Karibu watu milioni mbili wamekimbia makazi yao huko Tigray, na kukimbilia katika maeneo mengine kutokana na vita.

Ghasia
Maelezo ya picha, Maeneo ya ghasia machafuko ya kisiasa

Hali tete ya usalama huenda ikaathiri idadi ya wapiga kura watakaojitokeza kupiga kura lakini pia ushiriki wa vyama mbalimbali vya siasa hasa vya upinzani katika uchaguzi huo. Lakini serikali inaweza kujipiga kifua ikisema uchaguzi huu unapaswa kutazamwa kwa jicho jema, kwa sababu unaonyesha kuna demokrasia kwa sababu unashirikisha vyama vya siasa zaidi ya 50.

Suala la usalama ni suala linalotazamwa zaidi. Kama ilivyotokea kwa Tigray kuamua kusogeza mbele uchaguzi wake wa ndani hasa wakati wa janga la corona mwaka jana, jambo lililotazamwa na serikali kuu kama halikuwa halali kisheria.

Tigray

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wameanza kupoteza maisha huko Tigray, maafisa wa serikali kwenye jimbo hilo wamethibitisha.

Mataifa ya Ulaya yanalaumiwa kwa kufumbia macho yanayoendelea Ethiopia

Ni vizuri kukumbuka uzoefu wa nchi ya Urusi baada ya mabadiliko ya Soviet, mageuzi yaliyoongozwa na Mikhail Gorbachev na Boris Yeltsin yakarejesha ukandamizaji chini ya Vladimir Putin. Mataifa ya magharibi ambayo awali yalifurahia hali ya mambo Ethiopia na kiongozi huyo mshindi wa tuzo ya Nobel, yameanza kuonyesha kusikitishwa.

Mataifa yenye nguvu ya G7 mara kadhaa yemtoa matamko kuhusu mageuzi nchini Ethiopia, huku Rais wa Marekani Joe Biden akimuonya waziri mkuu Abiy kuhusu kuendelea kwa mapigano na kuleta ugumu wa migawanyiko ya kikanda na kikabila katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hata hivyo mamlaka za Ethiopia zilijibu kwa ghadhabu dhidi ya kauli hizo za mataifa ya Ulaya na Marekani kuingilia masuala ya Ethiopia na kutaka kuonekana wema.

Prosperity Party rally
Maelezo ya picha, Chama cha Waziri mkuu Abiy cha Prosperity kinatarajia kushinda uchaguzi mkuu wa wa mwaka huu Ethiopia

Ni wakati sasa wa Bwana Abiy kuamua kusuka ama kunyoa, hasa wakati huu ambapo wanadiplomasia wa Magharibi kupitia mashirika yao ya mmisaada kutoa ahadi za kutoa misaada baada ya uchaguzi. Ni ngumu kufikiria kwamba kiongozi huyo wa Ethiopia amejiandaa kukwepa kile kilichotokea mwaka 1984, baa la njaa. Lakini wakosoaji wa Bwana Abiy wana wasiwasi na maamuzi yake ya mashaka ya namna alivyoshughulikia mzozo wa kidiplomasi dhidi ya mataifa ya Misri na Sudan kuhusu mto Nile, mapigano kwenye jimbo la Tigray na mzozo na majirani zake, Eritrea.

Maswali yako mengi ya kujiuliza kwa mfano; je uchaguzi huu utakuwa wa kujibanza tu na kuficha ukweli lakini utakaoipeleka nchi hiyo kwenye demokrasia? au kichocheo cha mizozo isiyokwisha? Waweza kusema kwa sasa barani afrika hakuna nchi iliyo katika wakati mgumu kuhusu uchaguzi wake kama Ethiopia.