Uchaguzi Mkuu wa Ethiopia 2021: Masuala muhimu kuhusu Uchaguzi mkuu wa Ethiopia

Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Abiy Ahmed aliunda chama kipya cha siasa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu

Ethiopia inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu Juni 21 mwaka huu, licha ya kuendelea kwa mapigano na uwepo wa baa la njaa katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo, kunakokoleza mvutano zaidi baina ya makundi makubwa ya kikabila yanayozozana.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Agosti 2020 lakini ulisogezwa mbele, huku sababu inayotajwa zaidi kuwa ni janga la corona.

Wapiga kura watachagua wabunge 547 wa bunge la Shirikisho, na kiongozi wa chama kitakachoshinda atakuwa waziri mkuu. Uchaguzi mkuu uliopita ulifanyika mwaka 2015.

Kwanini Uchaguzi huu unatupiwa macho zaidi?

Hili ni jaribio la kwanza kwa waziri mkuu Abiy Ahmed tangu aingie madarakani akihaidi kumaliza uonevu nchini humo, ingawa tayari kuna wasiwasi kuhusu uhuru wa uchaguzi huo.

Waziri mkuu Abiy aliingia madarakani April 2018 kufuatia maandamano ya kupinga serikali ya muungano iliyokuwa na viongozi wengi kutoka kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) hali iliyotikisa usalama wa Ethiopia.

TAKWIMU

Amesaidia kubana mianya ya rushwa, aliwatoa wafungwa wa kisiasa, aliwateua wanawake wengi kwenye baraza la mawaziri, na kushiriki kuleta amani baina ya Ethiopia na majirani zake Eritrea, kufuatia vita kuhusu mipaka kati ya mwaka 1998-2000 iliyosababishja vifo vya maelfu ya watu.

Utayari wake wa kuboresha mifumo ya utendaji wa serikali ya nchi hiyo, ilimfanya akashinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019, lakini mwaka mmoja baadae akaongoza majeshi kwenye eneo la Tigray kuwaondoa TPLF, waliokuwa wanatawala eneo hilo, kitendo kilichosababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakiripotiwa kuachwa kwenye baa kubwa la njaa.

Tigray.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mapigano makubwa kwenye eneo la Tigray yamesababisha madhara makubwa kwenye maisha ya watu

Moja ya sababu iliyopelekea pande hizo kuzozana na kuingia kwenye mapigano ni pamoja na kuhairishwa kwa uchaguzi hapo mwaka jana, TPLF ikimtuhumu waziri mkuu Abiy kwa kutumia sababu ya janga la corona kujiongezea muda wa kusalia madarakani baada ya uda wake kumalizika Septemba 2020.

Nini mtizamo na maono ya Waziri Mkuu Abiy?

Abiy Ahmed, ambaye ametoka jamii ya Oromo, alichaguliwa na EPRDF kama kiongozi wa chama -na kuwa waziri mkuu mwaka 2018., Lakini baadae akavunja EPRDF iliyoundwa na vyama vinne vya siasa, na kujiunga na chama kipya cha 'Prosperity Party.' EPRDF ilikua madarakani tangu mwaka 1991 na kilishinda viti vyote katika uchaguzi wa mwaka 2015, uchaguzi ambao ulilalamikiwa kujaa udanganyifu wa kura.

Abiy Ahmed

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chama cha Abiy Ahmed, kinatarajia kushinda uchaguzi huo

Anasema kuwa na chama kimoja itasaidia kuleta umoja wa kitaifa na kupunguza migogoro ya kikabila. TPLF ilikataa kujiunga na chama hicho kipya cha Abiy, huku vyama vingine chini ya EPRDF, vya ADP, ODP na SEPDM vilikubali kuvunja vyama vyao.

Je kuna upinzani uliosalia?

Bodi ya taifa ya uchaguzi nchini Ethiopia, ilisema zaidi ya vyama 40 vimetangaza kusimamisha wagombea, lakini vyama vingi ni vya ngazi ya majimbo. Bodi hiyo ilisema zaidi ya wagombea 9,000 wamejitokeza kuwania nafasi katika uchaguzi huo kwa ngazi mbalimbali, ikisema idadi hiyo ni kubwa zaidi kutokea katika uchaguzi mkuu wa Ethiopia.

Berhanu Nega

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Berhanu Nega ni mgombea pekee wa upinzani (EZEMA) anayefahamika aliyejitokeza katika uchaguzi mkuu wa Ethiopia.

Hata hivyo upinzani umelalamikia ukandamizaji wa serikali uliosababisha kuvurugwa kwa mipango yao ya ya uchaguzi. Vyama vya siasa kwenye jimbo maarufu la Oromia, vimetagaza vitasusia OLF kimeshatagaza kujitoa mwezi March mwaka huu, kikilalamikia kushikiliwa kwa viongozi wake pamoja na kufungwa kwa ofisi zake ikiwemo makao yake makuu. Hivi ni vyama vya muda mrefu vikiwa na wafuasi wengi huko Oromia, anakotoka waziri mkuuAbiy.

Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi wa upinzani Jawar Mohammed yuko jela akituhumiwa kwa makosa ya kigaidi

Chama cha OFC, anachotokaJawar Mohammed, kilitangaza pia mwezi March kutoshiriki uchaguzi ho, kikieleza sababu zinazofanana na vyama vingine ikiwemo kushikiliwa kwa baadhi ya viongozi wake.

Uchaguzi huu utafanyika kwenye maeneo yote?

RAMANI

Jibu rahisi na la moja kwa moja ni Hapana.

Kwa mfano katika eneo lililokumbwa na machafuko la Tigray, uchaguzi hautafanyika, licha ya kwamba waziri mkuu Abiy alitagaza kushinda katika uchaguzi uliofanyika Novemba 2020. Jimbo hilo kwa sasa liko chini ya uongozi wa muda, baada ya bunge kupiga kura kuondosha utawala uliokuwepo wa TPLF ukisema ni batili. Bodi ya taifa ya Uchaguzi wa Ethiopia inasema, tarehe ya uchaguzi katika jimbo la Tigray itapangwa hapo baadae mara baada ya mamlaka za muda katika eneo hilo zitakapofungua ofisi kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo.

Upigaji kura umeharishwa pia katika majimbo 54 mpaka septemba 6, ikielezwa kwamba kukumbwa na tatizo la karatasi za kupigia kura.

Kwa mujibu wa Reuters jumla ya majimbo 78 kati ya 547 hayatafanya uchaguzi. Kumekuwa na ongezeko la vurugu za kikabila tangu Aabiy achukue madaraka, hali inayoleta hof kwamba huenda ikavuruga uchaguzi huo.

Uchaguzi utakuwa uhuru na haki?

Mwezi Mei, mwaka huu Umoja wa Ulaya EU iliondoa timu yake ya uangalizi kwenye uchaguzi huo wa Ethiopia kwa kile ilichokisema kwamba walishindwa kuafikiana na serikali katika baadhi ya maeneo.

Ikazituhumu mamlka za Ethiopia kwa kushindwa kuhakikishia uhuru timu yake hiyo na kukataa kuruhusu kuingiza vifaa vya mawasiliano kwa ajili usalama wa wajumbe wa timu hiyo.

Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Utawala wa Waziri Mkuu Abiy, umekumbwa na mapigano mengi katika maeneo mbalimbali ya Ethiopia

Bodi ama tume ya Uchaguzi ya Ethiopias ikajibu tuhuma hizo ikisema kwamba, inafanya uchaguzi kwa mujibu wa sheria za EWthiopia na viwango vya kimataifa.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya wapiga kura milioni 37 wamejiandikisha kupiga kura kati ya watu milioni 50 wenye sifa ya kupiga kura.