Mzozo wa Tigray: Ni kwanini hali Ethiopia inaelekea kutodhibitiwa

Chanzo cha picha, AFP
Ethiopia inaonekana kukaribia kutumbukia haraka katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Mapigano kati ya jeshi la serikali ya shirikisho ambayo yanaongozwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na jeshi la jimbo la Tigray linaloongozwa na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF yamesababisha vifo vya mamia ya watu na yanatishia kuligawanya taifa.
Wakati mapigano yanaendelea , pande hizo mbili bado zipo kwenye vita ya maneno pia. Kila upande unajaribu kuvutia upande wake na kila upande unajaribu kuushawishi ulimwengu una nia nzuri.
Serikali mjini Addis Ababa na TPLF zinashutumiana kufanya mashambulizi. Bwana Abiy alisema maafisa wa polisi waliuawa kikatili.

Chanzo cha picha, AFP
Kiongozi wa Tigrayan Debretsion Gebremichael alisema kuwa Ethiopia inashirikiana na nchi jirani ya Eritrea kufanya mashambulizi.
Mpaka uchunguzi huru utakapofanyika, basi taarifa zinazoenea zitabaki kuwa shutuma tu bila ya kuwa na ushaidi, jambo linalotumiwa kuchochea hisia za uhasama.
'Miaka ya giza'
Pande hizi mbili zinaiona historia ya Ethiopia kwa namna mbili tofauti kabisa.
Mfalme wa Ethiopia Haile Selassie aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya mwaka 1974. Kikosi cha jeshi la junta kinachofahamika kama mamlaka ya Derg.

Chanzo cha picha, AFP
Raia wa Tigray wanakumbuka kuwa miaka hiyo ilikuwa ya giza, ambapo kila siku walisikia milipuko na milio ya risasi, ambapo uvamizi wa makombora ya ndege za kijeshi aina ya jet ziliwalazimisha kutembea nyakati za usiku pekee.
Katika shambulio moja baya la anga mwaka 1988 katika mji wa Hausien, wachuuzi 1800 waliuawa , moshi na vumbi vilibadili mchana kuwa giza kama usiku.
Mapigano yaliyoongozwa na TPLF, jeshi la Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF) lilishinda jeshi la serikali mwaka 1991.
Siku waliochukua madaraka , kiongozi wa EPRDF Meles Zenawi, kutoka jamii ya Tigray, alisema lengo lao la kwanza ni kufanya raia wa Ethiopia kula milo mitatu kwa siku.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa zaidi ya utawala wa miaka 27 ya EPRDF, vifo vya wanawake na mtoto vilipungua kutoka kati ya mmoja kwa watano kufikia kwa mmoja kati ya 20.
Njaa iliisha.
Vita kubwa za wenyewe kwa wenyewe ziliisha pia.
Lakini Ethiopia haikuona demokrasia.Waziri mkuu Abiy na wafuasi wake waliupa uongozi huo jina la miaka 27 ya gizani.
Vijana waliminywa haki ya kujihusisha kwenye siasa.
Walisema jamii ya Tigray illihodhi siasa na uchumi kwa manufaa yao binafsi, kulingana na AFP
Bwana Abiy mara nyingi hudai kuwa huwa anaongea kutokana na mamlaka aliyopata kutoka kwa Mungu.
Alex De Waal
Mchambuzi wa Ethiopia
Abiy Ahmed, ametoka jamii ya Oromo, alichaguliwa kuingia madarakani wakati ambao kulikuwa hakuna mgawanyiko.
EPRDF ilimchagua kama kiongozi wa chama -na kuwa waziri mkuu mwaka 2018.
Mara akajitoa EPRDF na kuanzisha chama kipya cha 'Prosperity Party.'
Hatua ambayo ilimpa umaarufu. Ukosoaji wake ulichochea mtazamo wake wa kugawanyika hakujengi.
Abiy alifanya jitihada za kupatana na Eritrea, jambo ambalo lilimpa tuzo mwaka jana na kuwa karibu na rais Isaias Afwerki, licha ya kuwa kiongozi huyo kuwahi kusema kuwa itaishambulia Ethiopia, kwa kuanza na jeshi lake.

Chanzo cha picha, AFP
Bwana Abiy ni Mpentekoste na huwa anazungumza pale anapopewa mamlaka kutoka kwa Mungu.
Katika uandishi wake, pamoja na mukhtasari wa PhD yake, alisoma kwa nyenzo za msaada wa shule ya biashara. Ujasiri wake ulimpa nguvu ya kuona kuwa ni kiongozi anayeweza kukabiliana na uhalisia wa mambo.
Bila ya kuwa na shaka aliungwa mkono na jamii kubwa ya Amharas ambao wako Addis Ababa na jamii ya Amhara. Lakini si yeye au chama chake kipya kimekabiliana na jaribio la uchaguzi.
'Katiba '
Bado Bwana Abiy anasema kuwa TPLF imevuka mipaka wakati ilipositisha uchaguzi mwezi Septemba.
Serikai ya shirikisho haikutoa idhini kwa uchaguzi huo na chama cha Prosperity kisingeweza kushiriki katika uchaguzi.

Chanzo cha picha, AFP
Wadau wa TPLF walitaka uchaguzi ufanyike mwanzoni mwa mwaka lakini uchaguzi huo ulihairishwa kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona na kuwa serikali iliyoko madarakani imemaliza muda wake bila ya siku ya kupiga kura kufahamika.
Wanasema kuwa huko wana mamlaka nako kutoka kwa wapiga kura.
Malumbano kuhusu katiba ya Ethiopia yanasimamia nini…
Taifa hilo lina mfumo wa serikai shirikishi kati ya serikai na jimbo ambalo linaongoza eneo lake.
Mwaka 1994 muda mfupi baada ya EPRDF kuchukua madaraka. Bwana Abiy ametaka kukabiliana na hilo.
Kwa namna ya kipekee, majimbo ya Ethiopia walipewa haki ya kujiongoza.
Wazo la mgawanyiko huo lilikuwa ni kama kutakuwa na kuanguka kwa demokrasia , kila jimbo linaangalia kwa namna yake..
Hatua hiyo ilikuwa si kwa jamii ya Tigray peke yake lakini pia hata kwa jamii nyingine ambazo ni makundi yaliyoachwa ikiwemo Oromo -ambayo ni jamii kubwa zaidi Ethiopia.
TPLF haikutaka mgawanyiko huu.Lakini kile kinachoendela leo hii kinawapeleka katika mkondo huo wa kujigawa.
TPLF ina wanasiasa kutoka Oromos na jamii nyingine kusini mwa Ethiopia.
Lakini jamii zote hizo wanathamini kipengele cha kujitawala katika katiba.
Vivyo hivyo , kundi moja kati ya hayo - Sidama - ilipiga kura ilikuwa na jimbo lao mwaka jana.
'Kuongoza au kuharibu'
Mwaka huu bwana Abiy alienda kinyume dhidi ya vijana waliomuweka madarakani .
Baada ya mauaji ya muimbaji wa Oromo Hachalu Hundessa, watu zaidi ya 150 waliuawa katika maandamano na Abiy aliwafunga zaidi ya watu 10,000.
Miongoni mwao alikuwa Jawar Mohamed, muasisi wa mtandao wa habari wa Oromo,anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
Mwingine kiongozi wa upinzani Lidetu Ayalew ambaye yupo bado gerezani licha ya mahakama kumuachia huru.
Kundi la wenye silaha linalojiita 'Oromo Liberation' liliuawa zaidi ya wanakijiji wa 50 wa Amhara katika eneo la Wollega , wiki mbili zilizopita.
Bwana Abiy analaumiwa kwa kuona raia wake kuwa maadui .

Chanzo cha picha, AFP
Serikali yake ni washirika wa Amhara ambayo inataka kusitisha mfumo wa serikali shirikishi ili kujipendelea upande wao.
Kuna sababu nyingi za kukosoa mfumo huu wa uongozi lakini makundi yanayopinga yameweka wazi kuwa hawawezi kuongozwa kinyume na matakwa yao.
Taarifa za vita zinaonesha kuwa raia wa Amhara wameathirika na mapigano hayo.
Ripoti kutoka Addis Ababa na miji mingine zinaeleza kuhusu kushikiliwa kwa watu wengi wa jamii ya Tigray.
Jeshi la serikali limefungia taarifa kufika Tigray. Vilevile usambazaji wa misaada ya kinadamu imekuwa shida.

Chanzo cha picha, Reuters
TPLF imesema imewakamata wanajeshi waliovamia Tigray.
Bwana Abiy alitangaza vita kwa madhumuni ya kuisimamia Tigray.
Hakuna anayeamini kuwa hilo linawezekana , rais wa Eritrea ambaye baadhi wanaamini kuwa anahusika katika mipango ya kuivamia Tigray, hajasema lolote.
Mzozo wa Ethiopia unaongezeka kila siku.
Jambo ambalo linaweza kugharimu maisha ya maelfu ya watu .












