Mzozo wa Tigray Ethiopia: Roketi yapiga pembezoni mwa Eritrea

An Ethiopian woman who fled the ongoing fighting in Tigray region holds a child in Hamdait village on the Sudan-Ethiopia border in eastern Kassala state, Sudan November 14, 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Kiongozi wa jimbo la Tigray, Ethiopia amesema jeshi lake limepiga roketi katika uwanja wa ndege wa Eritrea, usiku wa Jumamosi na kuongeza mzozo katika eneo hilo.

Kiongozi huyo amelishutumu jeshi la taifa kwa kutumia uwanja wa ndege kufanya mashambulizi Tigray.

Serikali ya shirikisho ya Ethiopia haijasema lolote kuhusu madai hayo.

Lakini mashambulizi hayo yameonekana kuwa yanaongezeka kwa siku 12-kati ya serikali ya Ethiopia na serikali ya Tigray.

Mapigano yanayoendelea Tigray, yameathiri Sudan, raia wa Ethiopia wapatao 17,000 wamekimbia Ethiopia, kwa mujibu wa UN.

Ethiopia imepita katika mabadiliko makubwa tangu waziri mkuu Abiy Ahmed kuingia madarakani mwaka 2018.

Alipata tuzo ya Nobel mwaka jana baada ya kufikia maafikiano na nchi jirani ya Eritrea, ambayo walikuwa wanapambana kwa miongo miwili.

Lakini mabadiliko makubwa aliyoyafanya aliyasimamia yaliwaweka pembeni watu wa jimbo la Tigray ambalo linaongozwa na chama cha kisiasa cha TPLF - na wiki za hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya chama hicho na serikali ya shirikisho.

Nini kimetokea Eritrea?

Usiku wa Jumamosi, wakazi wa Asmara waliripoti kuwa walisikia milipuko mikubwa , na mara ripoti kuw roketi ilipiga karibu na uwanja wa ndege iliripotiwa.

Hakuna athari iliyoripotiwa mpaka sasa.

Watu wa jamii ya Tigray walishutumu jeshi la Eritrea kuunga mkono jeshi la Ethiopia.

e

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakala wa habari Reuters ilimnukuu kiongozi wa Tigray Bwana Debretsion akisema kuwa jeshi lake limekuwa likipambana na makundi 16 ya jeshi la Eritrea katika siku za hivi karibuni.

Presentational grey line

Huku serikali ya Eritrea imekanusha kuhusika na mgogoro wowote.

Mwandishi wa BBC Will Ross amesema ripoti za mapigano katika maeneo ya mpakani na askari wa kutibwa katika hospitali za Eritrea, zinaonesha maelezo kuwa kinyume chake ndio ukweli wa mambo.

Makombora yanaporushwa ndani ya Eritrea yanafanya mzozo huu sasa kuwa mkubwa zaidi na kuna uwezekano kuwa mgumu kuusitisha.

Athari zinaweza kusababisha kukosekana kwa utulivu katika eneo lote

Lakini watu wengi wanaofahamu maendeleo ya hivi karibuni ya kisiasa walikuwa wametabiri kuwa shida itaaza punde Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa mshirika mkubwa wa kiongozi wa Eritrea, Isaias Afwerki.

Presentational grey line

Sasa viongozi hao wana adui mmoja - wanasiasa wa Tigrayan wa chama cha TPLF ambao waliiongoza Ethiopia kwa kipindi kirefu, pamoja na wakati ambao Ethiopia na Eritrea walipopambana mpakani na kuacha makumi maelfu wakipoteza maisha yao.

Wito wa kimatifa umepuuziwa na maelfu ya raia wanaendelea kukimbia nchi yao na kuelekea Sudan.

Hali ni mbaya kiasi gani?

Mamia ya watu wameuawa katika mzozo unaoendelea kufukuta katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, Shirika la kutetea haki la Amnesty International linasema.

Waziri mkuu Abiy Ahmed amelishutumu jeshi la kiongozi wa Tigray kufanya mauaji hayo ya watu wengi , wakati TPLF ikikanusha kuhusika na mauaji hayo.

Tume ya haki za binadamu ya Ethiopia imesema itapeleka kikosi kufanya uchunguzi.

Maisha yanaendaje huko Tigray?

Mawasiliano ni shida kwa sasa kwasababu intaneti na huduma za simu zimezimwa.

Kuna ripoti za uhaba wa unga na mafuta-hatari zaidi maji pia yamekuwa ya shida.

Huko Mekelle, ambako kuna idadi ya kati ya watu 400,000 ha 500,000, wanakabiliana na uhaba wa maji wakati awali walikuwa wanapata mara moja kwa wiki.

Familia zilikuwa zikinunua maji kutoka kwa wauzaji wa barabarani lakini sasa hakuna mawasiliano ya simu .

Ni kwanini serikali ya Ethiopia na TPLF wanapigana?

Hali ya wasi wasi imekuwa ikiongezeka kwa muda mrefu na uhusiano kati ya TPLF na serikali kuu umezota

TPLF ilitawala jeshi la Ethiopia na maisha ya kisiasa kwa miongo kadhaa kabla ya Bw Abiy kuingia mamlakani mwaka 2018 na kupitisha mageuzi mkubwa.

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa ka misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja , national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.

Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzoz wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

Kwa upande wake, waziri mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanadharau mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".

Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi