Mzozo wa Israeli na Wapalestina: Shambulio la ndege za Israeli lapiga vyombo vya habari vya kimataifa

Jengo la gorofa mjini Gaza, lenye ofisi za vyombo vya habari Associated Press (AP) na Al Jazeera limeanguka baada ya kupigwa na shambulio la roketi ya iliyofyatuliwa na ndege ya Israeli.
Wafanyakazi hao ambao wengi wao wanafanyia kazi vyombo vya habari vya kimataifa walikua tayari wameondoka kwenye jengo hilo baada ya mmiliki wake kupata onyo kutoka kwa Israeli mapema juu ya mashambulizi, linasema Shirika la habari la Reuters.
Afisa habari wa Ikulu ya White House ya Marekani Jen Psaki ametuma ujumbe wa Twitter muda akisema : "Tulikuwa tumewasiliana mapema na Waisraeli kwamba wahakikishe usalama wa waandishi wa habari na vyombo huru vya habari ni muhimu katika uwajibikaji ."
Awali mitandao ya kijamii ilionesha picha za video za tukio la shambulio la roketi kwenye jengo lenye ofisi za vyombo AP na Aljazeera:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mauaji ya watoto
Wakati huo huo Watu 13 wameuawa, waliwemo watoto wanane, katika mashambulio hayo ya anga ya ndege za israeli baada ya maroketi kupiga kwenye kambi ya wakimbizi ya Gaza.

Muhammad Hadidi, baba ambaye watoto wanne wameuawa katika shambulio hilo lililopiga kwenye kambi ya wakimbizi ya Shati iliyopi mjini Gaza, anasema amepoteza kila kitu.
Mke wake , Maha, na watoto walikuwa wakiishi na kaka yake wakati jingo lilipowaangukia.

Chanzo cha picha, Anadolu Agency/Getty Images
Mtoto wake mchanga wa miezi mitano Omar, anasemekana kuwa ndiye pekee aliyenusurika, baada ya kupatikana akiwa amekwama kwenye vifusi vya jingo lililopigwa na ndege za Israeli , akiwa kando ya mama yake ambaye amekufa.
Hadidi anataka "dunia isiyo na haki kuona uhalifu huu", aliliambia shirika la habari la AFP , alipokuwa akizungumza nalo nje ya hospitali ya Shifa mjini Gaza.
"Walikuwa salama katika nyumba zao , hawakuwa wamebeba silaha, hawakuwa wamebeba maroketi," alisema kuwahusu watoto wake ambao "wakiwa wamevaa nguo zao walizonunuliwa kwa ajili ya Eid al-Fitr".
Unaweza pia kusoma:
Kwa ujumla, mashambulio ya anga yamewauwa watu 10 kutoka katika ukoo mmoja, wakiwemo watoto wanane, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina mjini Gaza.
Mapema madaktari wa Israeli walisema kuwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 na zaidi aliuawa wakati jengo moja lilipopigwa na roketi katika kitongoji cha mji mkuu wa Israeli Tel Aviv cha Ramat Gan.

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, AFP
Polisi walinukuliwa na gazeti la Times la Israeli wakisema eneo hilo lilipigwa na maroketi mawili na kwamba watu wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Milipuko ya makombora na mabomu imekuwa ikiripotiwa katika vitongoji Rishon Lezion na mji wa Waarabu Taibe, karibu na Tel Aviv, lakini bado haijawa wazi iwapo kuna majeruhi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2












