Mzozo wa Israeli na Wapalestina: Fahamu Waarabu Waisraeli ni akina nani na ni kwanini wanadai wanatengwa.

Israeli Arab women voting in the village of Jaljuliya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waarabu wa Israeli wanaweza kupiga kura lakini wengi wanasema wanabaguliwa

Wiki hii imekuwa wiki ya msururu wa mashambulio katika maeneo ya ya Waisraeli na Wapalestina.

Baada ya siku za ghasia, Israeli iliweka kipindi cha dharura katika mji wa Lod. Karibu na mji mkuu Tel Aviv, baada ya Waarabu katika mji huo kuandamana.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Israeli kuweka hali ya dharura dhidi ya Waarabu tangu mwaka 1966.

Maelezo ya video, Tazama jinsi jengo la Ghorofa Gaza linavyoanguka katika shambulizi la angani la Israeli.

Lakini je Waarabu wa Israeli ni akina nani ?

Historia ya Waarabu wa Israeli

Israeli protesters, Jewish and Arab, hold a demonstration in Jaffa on April 19, 2021

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, PICHA Waarabu na Wayahudi wakiandamana pamoja Aprili 2021 juu ya jaribio la kununua nyumba katika mji wa Jaffa karibu na Tel Aviv.

Ndio maana sio jambo la kushangaza unasikia kwamba Israeli ni ardhi ya Wayahudi, lakini pia kuna watu Wayahudi.

Kuna waarabu walio wachache, ambao asili yao ni kutoka Palestina lakini pia ni raia wa Israeli.

Israeli ina jumla ya idadi ya watu takriban milioni tisa, na karibu moja ya tano ya watu hao - ambao ni sawa na takriban milioni 1.9 ni Waarabu.

Walikuwa ni Wapalestina ambao waliendelea kuishi Israeli baada ya kuundwa kwa taifa mwaka 1948, huku 750,000 kati yao ama walikimbia au nyumba zao zilichukuliwa baada ya kuibuka kwa vita vilivyofuatia.

Wakimbizi wamevuka mpaka na kuingia katika maeneo ya West Bank na ukanda wa Gaza na katika makambi ya wakimbizi katika katika maeneo hayo.

Waliobaki nchini Israeli hujiita Waarabu au Waisraeli Wapalestina au Wapalestina.

Waarabu wa Israeli wengi wao ni Waislamu, lakini swan a maeneo mengine ya Palestina.

Tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kwanza wa Isreli, Waarabu walipewa haki ya kupiga kura Januari 25, 1925- lakini wanasema wamekuwa wakibaguliwakatika nchi hiyo kwa miaka.

Dr. Limor Rubin (2nd R) and nurses put on protective gear, as they prepare to enter an isolated ward to treat Covid-19 patients

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati wa janga la corona, Waarabu na Wayahudi walishirikiana kuwahuduamia wagonjwa katika hospitali

Waarabu na Wayahudi wa Israeli hawakuingiliana sana, ingawa janga la corona liliwalazimisha kufanya kazi pamoja.

Moja ya ushirikiano ulikluwa ni kupitia sekta ya afya -ambapo Waarabu na Wayahudi wakikutana katika hospitali moja ambapo ungekuta mmoja ni daktari wa kliniki na mwingine ni daktari bingwa wa maradhi.

Unaweza pia kusoma:

Asilimia 20 ya madaktari wote wa Israeli ni Waarabu, 25 asilimia ni manesi, na asilimia 50 ni wataalamu wa Famasia.

Lakini ni vigumu kuelewa uhusiano kati yao ingawa wote ni raia wa nchi moja.

Kwa mfano, jeshi lina nafasi muhimu nchini Israeli na mafunzo ya kijeshi ni ya lazima kwa raia wote. Lakini pia mafunzo hayo sio muhimu kwa Waarabu.

Ubaguzi

Close up of Yakov, an Israeli settler was captured on video in the garden of a Palestinian family's home in Sheikh Jarrah, East Jerusalem

Chanzo cha picha, muna.kurd15

Maelezo ya picha, PICHA: Video imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ya muyahudi ambaye anadai kuwa nyumba inayomilikiwa na familia ya mpalestina ni yake

Waarabu Waisraeli mara kwa mara wamekuwa wakisema kuwa wanabaguliwa dhidi ya nchi yao wenyewe, na makundi mengi ya haki za binadamu yanaamini hili.

Shirika la haki za binadamu la kimataifa Amnesty International linasema Israeli imetangaza rasmi ubaguzi dhidi ya Wapalestina wanaoishi nchini humo.

Ripoti ya Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch iliyotolewa mwezi Aprili 2021 inasema kwamba serikali ya Israeli ni ya kibaguzi, inafanya uhalifu dhidi ya Waarabu Waisraeli na Wapalestina wanaoishi katika miji iliyovamiwa West Bank na Fail.

Wizara ya mambo ya nje ya Israeli ilipinga ripoti hiyo iliyoitaja kuwa "uongo".

Waarabu wanasema serikali ina historia ndefu ya kuchukua ardhi na kuwashutumu Wayahudi kwa kuwabagua katika bajeti na masuala ya kitaifa.

Sheria za kila kundi pia ni tofauti nchini.

'Ng'ombe aliyetengwa'

Kwa mfano, sheria ya Israeli ya kupata cheti cha uraia inawapendelea zaidi Wayahudi, ambao wanaweza kupata mara moja paspoti bila kujali walikotoka

Wapalestina walifurushwa na watoto wao hawana haki

Mwaka 2018, bunge la Israeli lilipitisha sheria inayopiga marufuku matumizi ya Kiarabu kama lugha ya taifa-na Kiyahudi- na baadae kubuni "mazingira bora " kwa Wayahudi.

Ayman Odeh, mbunge wa Kiarabu katika bunge la Israeli, alisemaIsraeli ilipitisha sheria ya 'kuwaheshimu Wayahudi', na kuwaambia Waarabu kwmaba 'ng'ombe aliyetengwa atakuwepo wakati wote nchini Israeli .'

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliahidi usawa lakini akasema " ni jukumu la wengi kuamua".kuhusu hilo.