Kifo cha George Floyd: "Babangu amebadilisha dunia", ujumbe wa hisia uliotumwa na Gianna Floyd

Gianna Floyd

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Gianna ni mwana wa kike wa Floyd mwenye umri wa mika sita ambvaye alifariki akiwa amekamatwa na maafisa wa polisi tarehe 25 Mei
Muda wa kusoma: Dakika 2

Gianna Floyd ana umri wa miaka sita pekee lakini alitoa taarifa kali kwamba babake amebadilisha ulimwengu.

Gianna ni mwana wa kike wa George Floyd , mwanamume ambaye alifariki wakati alipokamatwa na maafisa wa polisi wa Minneapolis wakati afisa mmoja alipomwekelea goti lake katika shingo yake kwa dakika nane.

Kifo chake kilizua maandamano ya kupinga ubaguzi unaotekelezwa na polisi.

Maandamano mangine yalikuwa na amani huku mengine yakiishia kukumbwa na ghasia na wizi .

Matamshi hayo ya msichana huyo yanaonekana katika kanda ya video iliochapishwa katika mtandao wa instagram Jumanne iliopita na Stephen Jackson, mchezaji wa zamani wa mchezo wa kikapu wa NBA na rafiki wa Floyd .

'Babangu alibadilisha ulimwengu' , alisikika akitabasamu na Jackson anaongezea , hiyo ni kweli , baba alibadilisha ulimwengu''.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

" Hiyo ni kweli GiGi, babako alibadilisha ulimwengu, Jackson aliandika katika ujumbe ulioandamana na video ambayo Alhamisi hii ilitazamwa zaidi ya mara milioni 1.7.

"George Floyd, jina la mabadiliko hayo.

Mkewe George Floyd alisemaje?

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika mji wa Minneapolis siku ya Jumanne , mamake Gianna , Roxie Washington , alizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Floyd.

''Sina mengi ya kusema , kwasababu siwezi kuunganisha maneno kwa sasa' , alisema katika ukumbi wa mji wa Minneapolis

"Lakini nilitaka kila mtu kujua kwamba hicho ndio maafisa hawa wa polisi walichukua akimuotesha mwanawe. Na mwisho wa siku wanaenda nyumbani na wanaishi na familia zao.

katika mkutano na vyombo vya habari ,Roxie washinton , mamake Gianna na mkewe George Floyd alitaka haki kufanyika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, katika mkutano na vyombo vya habari ,Roxie washinton , mamake Gianna na mkewe George Floyd alitaka haki kufanyika
George Floyd akiwa amembeba Gianna

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, ''Hana baba tena.hatomuona akikuwa ama hata kufuzu, hatoweza tena kuandamana naye wakati wa harusi yake'', alisema Washington.

Katika taarifa fupi iliojaa hisia, alisisitiza kwamba mwanawe hana baba tena. hatomuona akikuwa ama hata kufuzu, hatoweza tena kuandamana naye wakati wa harusi yake, alisema Washington.

"Iwapo una tatizo na unamuhitaji baba yako hayupo tena'' , aliongezea.

"Niko hapa kwasababu ya mwanangu na George kwasababu nataka apatiwe haki kwa kuwa alikuwa mtu mzuri."

Alikuwa mtu mzuri , Washington alisema kuhusu Floyd

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Alikuwa mtu mzuri , Washington alisema kuhusu Floyd

Mwendesha mashtaka aliwasilisha mashtaka ya mauaji siku ya Jumatano dhidi ya afisa wa polisi Derek Chauvin ,afisa wa zamani ambaye alimwekea goti katika shingo Floyd.