Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kifo cha George Floyd: "Babangu amebadilisha dunia", ujumbe wa hisia uliotumwa na Gianna Floyd
Gianna Floyd ana umri wa miaka sita pekee lakini alitoa taarifa kali kwamba babake amebadilisha ulimwengu.
Gianna ni mwana wa kike wa George Floyd , mwanamume ambaye alifariki wakati alipokamatwa na maafisa wa polisi wa Minneapolis wakati afisa mmoja alipomwekelea goti lake katika shingo yake kwa dakika nane.
Kifo chake kilizua maandamano ya kupinga ubaguzi unaotekelezwa na polisi.
Maandamano mangine yalikuwa na amani huku mengine yakiishia kukumbwa na ghasia na wizi .
Matamshi hayo ya msichana huyo yanaonekana katika kanda ya video iliochapishwa katika mtandao wa instagram Jumanne iliopita na Stephen Jackson, mchezaji wa zamani wa mchezo wa kikapu wa NBA na rafiki wa Floyd .
'Babangu alibadilisha ulimwengu' , alisikika akitabasamu na Jackson anaongezea , hiyo ni kweli , baba alibadilisha ulimwengu''.
" Hiyo ni kweli GiGi, babako alibadilisha ulimwengu, Jackson aliandika katika ujumbe ulioandamana na video ambayo Alhamisi hii ilitazamwa zaidi ya mara milioni 1.7.
"George Floyd, jina la mabadiliko hayo.
Mkewe George Floyd alisemaje?
Wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika mji wa Minneapolis siku ya Jumanne , mamake Gianna , Roxie Washington , alizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Floyd.
''Sina mengi ya kusema , kwasababu siwezi kuunganisha maneno kwa sasa' , alisema katika ukumbi wa mji wa Minneapolis
"Lakini nilitaka kila mtu kujua kwamba hicho ndio maafisa hawa wa polisi walichukua akimuotesha mwanawe. Na mwisho wa siku wanaenda nyumbani na wanaishi na familia zao.
Katika taarifa fupi iliojaa hisia, alisisitiza kwamba mwanawe hana baba tena. hatomuona akikuwa ama hata kufuzu, hatoweza tena kuandamana naye wakati wa harusi yake, alisema Washington.
"Iwapo una tatizo na unamuhitaji baba yako hayupo tena'' , aliongezea.
"Niko hapa kwasababu ya mwanangu na George kwasababu nataka apatiwe haki kwa kuwa alikuwa mtu mzuri."
Mwendesha mashtaka aliwasilisha mashtaka ya mauaji siku ya Jumatano dhidi ya afisa wa polisi Derek Chauvin ,afisa wa zamani ambaye alimwekea goti katika shingo Floyd.