Watapisha vyoo wakumbukwa siku ya vyoo duniani. Wafanyakazi hawa maisha yao yako hatarini

Wapakua vyoo wakiwa kazini

Chanzo cha picha, Water Aid Report

Maelezo ya picha, Wapakua vyoo huwa na ndoo na koleo, vifaa duni katika kazi ya kupakua vyoo

Ni namna gani unaweza kushughulikia changamoto ya vyoo katika eneo la mji ambapo inakadiriwa kuwa 90% ya vyoo vya wakazi wake haviko kwenye mfumo rasmi wa maji taka?

Hii ni changamoto inayokabili jiji la Dar es Salaam, ambapo, suluhu yake kwa hakika ni moja kati ya kazi mbaya duniani.

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya vyoo, ripoti ya pamoja ya shirika la kazi duniani, Benki ya dunia na WaterAid imeeleza kuhusu mazingira ya hatari yanayowakabili ''wapakua vyoo''-Wafanyakazi wasio rasmi ambao husaidia shughuli za kusafisha mfumo wa maji taka.

Kwa hakika kazi hiyo ni miongoni mwa kazi isiyoweza kutamanika ulimwenguni.

Wakiwa na ndoo na koleo, wapakua vyoo wa Dar es Salaam huingia kwenye mashimo ya vyoo na kupakua haja kubwa.

Unaweza pia kusoma

Watu hawa ni muhimu kwenye mji ambo karibu nyumba tisa kati ya kumi haziko kwenye mfumo wa maji taka- na kutokana na ujenzi holela, magari ya serikalli hushindwa kufika kufanya kazi hiyo kitaalamu kwenye maeneo hayo yenye wakazi wengi.

Lakini wakazi hulipia huduma.

Mfanyakazi akisaidiwa kutoka shimoni

Chanzo cha picha, Water Aid

Maelezo ya picha, Watapisha vyoo huingia kwenye mashimo wakiwa hawana vifaa vya kujikinga

Watapisha vyoo, wengi wao wanaume, huwa hawana vifaa vya kujikinga.

Hushughulika moja kwa uchafu wa vyooni wakihatarisha afya zao kwa magonjwa mbalimbali. Wengi wao hupoteza maisha kwa sababu ya kazi hii.

Gesi za sumu, kama ammonia, hewa ya carbon monoxide na sulphur dioxide kwenye matangi ya maji taka zinaweza kuwafaya wafanyakazi hao kupoteza fahamu na hata kufa.

Hakuna takwimu duniani, lakini nchini India kwa mfano inakadiriwa kuwa wafanyakazi watatu hupoteza maisha.

Kwa kuwa si kazi iliyo rasmi, hakuna takwimu zinzoonyesha yale wanayoyapitia.

Wakati Dar es Salaam ikitarajiwa kuongezeka kufikia milioni 13.4 ifikapo 2035, kwa mujibu Umoja wa Mataifa, uhitaji wa huduma ya wafanyakazi hawa bado utaendelea kuwepo siku nyingi zijazo.