Utafiti: Manufaa ya 'kushangaza' ya kuzungumza na mtu usiyemjua

Two women talking on the tube

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika shughuli zetu za kila siku tunakutana na watu tusiowajua au kufahamiana nao iwe ni kwenye magari ya usafiri wa umma, hotelini, kwenye bustani au madukani.

Lakini wengi wetu tunahofia kusema nao kwa kuhofia tutachuliwa vipi ama kufikiria huenda tusielewane.

Hatahivyo wataalamu wanasema hakuna haja ya kujitenga na mtu usiemjua ukikutana nae kwa mara ya kwanza kwa kuzingatia kigezo hicho.

Utafiti wao mpya unaashiria kuwa huenda mara nyingine watu wanapuuza umuhimu wa kutangamana na wenzao lakini mazungumzo kati yenu huenda yakawaacha wote wakiwa na furaha.

Huo ni mfano mzuri kuwa kuzungumza na mtu usiemjua ukiwa njiani kuelekea kazini kunaweza kuwa na manufaa kwenu nyote kuliko vile mulivyotarajia.

Ili kubaini hilo watafiti walizungumza na baadhi ya wasafiri katika vituo vy mabasi na treni mjini Chicago. Walitaka kufahamu jinsi walivyojihidi walipozungumza na watu wadiojuana wakiwa safari wakilinganisha na wao kukaa kimya au kufanya kitu kingine

Baadhi ya wa wale waliohojiwa walihisi kuwa kuzungumza na watu wasio fahamiana kungeliwaweka katika hali ngumu ambayo ingeliwafanya kuonekana wasumbufu au wao wenyewe kukwazika kwasababu hawajui ikiwa mtu yule angelipendelea kushiriki mazungumzo hayo.

Lakini walipofanya uchunguzi zaidi kwa kuwapajukumu hilo watu waliowashirikisha katika utafiti huo walibaini wale waliozungumza na watu wasiojuana nao walifurahia safari yao.

Commuters in Chicago wait for a bus

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti huo ulibaini kuwa karibu 40% ya wasafiri walikuwa tayari kuzungumza na watu wasiojuana.

Kila alieshiriki utafiti huo alijaribu kusema na abiria aliyekaa nae na wote waliafiki kuwa walifurahia mazungumzo baina yao.

Kuwa na hofu kuwa mtu usiyemjua huenda asiwe na haja ya kusema nawe ndio kizingiti kinachotufanya kutoweza kujenga uhusiano na watu wengine zaidi ya wale tunaojuana nao.

Utafiti aidha unaashiria kuwa hali ya watu kujenga mazingira kuwa mtu mgeni huenda asiwe na haja ya kusema nao kwa kuzingatia mazungumzo ya awali baada ya kuamkuana ni dhana potofu.

Mawazo ya watu wasiojuana

Uchunguzi mwingine uliofanywa katika magari mengine ya usafiri wa umma pia ulipata matokeo sawa na yale ya awali na walishangaa kujiona wakifurahia kuzungumza na watu waliokutana nao kwa mara ya kwanza.

Umuhimu wa mawasiloano kati ya watu wawili wasiojuana ulibainika uchunguzi zaidi ulipofanywa katika chumba cha watu kusubiri kupewa huduma.

Watafiti waligundua kuwa watu wasiojuana wanaweza kufahamiana kwa njia rahisi sana wote wakichukulia kitendo cha wao kusemezana kama sehemu ya utu na ustaarabu katika jamii.

Bila shaka, hakuna mtu anaweza kufurahia mtu au watu asiowafahamu wakijaribu kujileta karibu kwasababu haju dhamira yao.

Lakini hatua yenyewe ya kumsalimia mwanadamu mwenzako hupokelewa vyema kuliko watu wanavyodhania.

Ni watu wachache huzungumza na watu wasiowajua lakini wengi wao hufurahia kuzungumza nao wakihisi nia yao sio mbaya.

Group of people at a bus stop

Chanzo cha picha, Getty Images

Kitu kimoja muhimu ambacho watu hunufaika nacho wakisemezana japo hawajuani ni kuwa kila mmoja wao anapata fursa ya kubadilishana mawazo na mwenzake mazungumzo yao yakifanikiwa kuendelea baada ya salamu za kawaida.

Ikitokea wawe na maoni sawa juu ya jambo fulani hata wakiachana na kila mmoja wa aelekee katika shughuli zake, atasalia na kumbukumbu ya kwamba sio yeye peke yake aliye na msimamo fulani kuhusu jambo fulani.

Kuzungumza na mtu usiemjua pia wakatinmwingine hukuondolea msongo wa mawazo.

Hali ambayo itakufanya kutulia kwa mfano ukijipata sio wewe pekee unaechelewa wakati mwingine au kuchua muda mrefu bararani kutokana na msongamano wa magari.

Wanadamu ni viumbe wanaopenda kutangamana ndio maana kila mtu ana yule mtu ambaye anamini anaweza kusema nae akiwa na furaha huzuni au msongo wa mawazo.

Mtu au watu hao huwafanya wajisikie wamefarijika.

Badala ya kujitenga ukiwa na matatizo wataalamu washauri ujaribubkadri uwezavyo uzungumze na mtu hata kama hamjuani kwani kufanya hivyo kutakuepusha na mawazo mabaya kama vile kujiingiza katika unywaji wa pombe kupita kiasi hali ambayo itakuwa na athari kwa afya yako.

Kuwa na mahusiano mazuri katika kamii ni moja ya viungo muhimu vinavyotufanya kuwa watulivu na wenye furaha na kwa kiwango fulani huchangia jinsi tunavyojitahidi kutafuta kazi na kama kazi ipo tuweze kutafakari jinsi ya kujiendeleza maishani.

Presentational grey line

Kuvunja ukimya

BBC Crossing Divides logo

Kundi la Profesa Epley lilijaribu kulinganisha matokeo ya utafiti wao wa Chicago kwa kufanyia majaribio matokeo hayo kwa niaba ya BBC mjini London.

Utafiti huo mpya ulihusisha wasafiri 700 wa reli ya Greater Anglia kuingia jijini London.

Watafiti walishirikiana na kampuni za usafiri kutoa arifa ya mapema kwa wasafiri kuwa wanaendesha kampeini ya kuimarisha utangamano wa kijamii katika vyombo vya usafiri.

Ili kufikia lengo hilo - makampuni ya usafiri yaliwashauri wateja wao kusemezana na wasafiri wenzao hata kama hawajuani.

Mpango huo ulijumuisha:

  • Treni zote za kampuni ya Virgin yanayohudumu katika eneo la magharibi mwa jiji yalishiriki kampeini ya "chat coach"
  • Pia yalisambaza kadi zinazowaomba abiria kusemezana na zingine zikiwaomba kufurahia uwepo wao pamoja kwa tabasamu.
  • Kampuni hiyo pia iliwashauri watu wa matabaka mbali mbali kutangamana kwa kutumia huduma ya usafiri ya Glider inayounganisha Ireland Kaskazini nnamiji ya Mashariki na Magharibi mwa Belfast.

Matarajio ya huenda yakawa tofauti

Huenda ukafikiria ni watu wacheshi pekee ndio walionufaika na kampeini hiyo.

Lakini uchunguzi wa kina umebaini kuwa kila mtu alifurahia kuzungumza na mtu asiyemjua kwa mara ya kwanza walielekezwa kutabasamu na watu walio karibu nao.

Watafiti walibaini kuwa mazungumzo kati ya watu wawili wasiofahamiana hutegemea na tabia ya mtu binafsi na hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Wanasema baadhi ya watu huenda wasifurahie kwasababu ni wapole na wanapendelea kuwa kivyao.

Hali hiyo huenda ikamwathiri yule ambaye anapenda kuzungumza kwasababu atafikiria amepuuzwa.

Women chatting in the park

Chanzo cha picha, Getty Images

Hofu ya kuogopa kupuuzwa inaelezea kwa nini baadhi ya miji ina watu wengi ambao hawana muda na wenzao.

Pia unaweza kupata watu wawili wamekaa pamoja lakini kila mmoja anatumia simu yake ya mkononi kupitisha muda kwa kuangalia picha au kufuatilia matukio katika mitandao ya kijamii.

Presentational grey line

Ukarimu usio na mipaka

Wataalamu hata hivyo wanasisitiza umuhimu wa mtu kuzungumza na mtu yeyote au kujaribu kuwakaribisha wale wanaojaribu kujileta karibu nao kwa sababu utafiti umebaini ufanisi wa mazungumzo kama hayo.

Walitoa mfano wa watu kuishia kuwa marafiki na hatimae wapenzi kutokana na mazungumzo ya watu wawili waliokuwa hawajuani.

"Wakati mwingine ikimuona mtu asiyekujua akijaribu kusema nawe msikilize ila tumia busara yako kutathmini dhamira yake kwako." Wanasema wataalamu wa masuala ya kisaikolojia.

line