Noti ya $50 ya Australia ina makosa ya herufi katika neno uwajibikaji

Chanzo cha picha, Reserve Bank of Australia
Noti mpya nchini Australia ya $50 imechapishwa ikiwa na makosa ya herufi, ambayo inatazamwa kuwa aibu.
Benki ya akiba ya Australia (RBA) imeandika neno "responsibility" yaani jukumu hivi - "responsibilty" - katika mamilioni ya noti hizo mpya za rangi ya njano.
Imethibitisha kosa hilo la herufi leo na kueleza kwamba litasahihishwa katika noti zitakazochapishwa katika siku zijazo.
Lakini kwa sasa, takriban noti milioni 46 zinatumika nchini.
Zilichapishwa mwishoni mwa mwaka jana na zinamuonyesha Edith Cowan, mbunge wa kwanza mwanamke nchini Australia.
Kinachoonekana kama nyasi nyuma ya bega la Bi Cowan, ni maandishi madogo mno - ya nukuu ya hotuba yake ya kwanza bungeni.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe

"Ni jukumu kubwa kuwa mwanamke wa kipekee hapa, na nataka nisisitize haja iliopo kwa wanawake wengine kuwepo hapa," ni maneno yalioandikwa na kuregelewa mara kadhaa kwa hati ndogo mno katika noti hiyo.
Na neno jukumu kwa kizungu 'responsibility', limechapishwa mara zote bila ya herufi 'i' - na kuandikwa "responsibilty".
Imechukua zaidi ya miezi 6 kutambua makosa hayo ya herufi.

Chanzo cha picha, Reserve Bank of Australia
Noti hiyo ya $50 ndiyo inayotumika sana Australia, na imesambaa pakubwa.
Wakati noti hiyo mpya ilipochapishwa mnamo Oktoba, iliundwa kwa vigezo vya kiusalama kuzuia kuighushi.
Na kama basi unajiuliza iwapo noti hiyo inatumika - ndio, noti hiyo yenye makosa ya herufi inatumika kama sarafu ya nchini humo.














