Mdude Nyagali: Mwanaharakati wa Tanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana apatikana

Mwanaharakati wa tanzania Mdude Nyagali

Chanzo cha picha, Mdude Nyagali/ facebook

Muda wa kusoma: Dakika 4

Saa chache baada ya mawakili watatu kuwafungulia mashtaka maafisa wa polisi na vikosi vya usalama kuhusu kutekwa nyara na kuzuiliwa kinyume na sheria kwa Mdude Nyagali-mkosoaji wa Magufuli katika mitandao ya kijamii, wanakijiji wamempata ametupwa katika kijiji cha Makwenje , wadi ya Inyala katika jimbo la Mbeya.

Akizungumza kwa simu, mmoja wa watu waliokwenda kumbeba eneo la tukio, alisema kwamba wamempeleka katika Hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Ndio, tupo nae kwenye gari, tunarudi mjini, anaongea vizuri. Ila tunaenda naye kwanza hospitali," alisema akizungumza na gazeti la mwananchi nchini humo.

Awali, taarifa za kupatikana kwa Mdude, zilitolewa na Diwani wa Kata ya Nsalala, Mbalizi, Kisman Mwangomale aliyedai kupigiwa simu na watu wa eneo la Makwenje Kijiji cha Inyala Mbeya vijijini, wakiomba msaada wa haraka kwenda kumuokoa.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kulingana na mashahidi , alipatikana ametupwa katika eneo moja lililo na nyasi.

Habari hizo zilithibitishwa na Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano Chadema Tumaini Makene aliyesema: Ndugu yetu , mpiganaji mwenzetu Mdude Nyagali { Mdude Chadema} amewpatikana akiwa hai . Nimemsikia mwenyewe akizungumza kwa mbali nilipoomba kujiridhisha kuwa ni yeye alisema ''Tutazungumza baadaye''.

Aliongezea katika taarifa hiyo kwamba yuko hai. Anaweza kuzungumza kwa shida lakini anaugua maumivu makali huku hali yake ikiwa dhoofu.

Mdude inadaiwa alitekwa nyara na maafisa wa polisi waliojihami huku wengine wakijifunika nyuso zao siku ya Jumamosi jioni katika ofisi yake katika mji wa Vwawa , wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Tukio hilo lilizua hisia kali miongoni mwa mwanaharakati, vyombo vya kimataifa pamoja na wanachama wa upinzani nchini humo huku harakati za kutaka kijana huyo aachiliwe zikianzishwa mara moja.

Awali kamanda wa polisi Mkoani Songwe, George Kyando aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa ''hakuwa na ufahamu wowote wa taarifa ya kukamatwa kwa kijana huyo.

Kupitia hashtag ya #BringBackMdudeAlive katika mtando wa kijamii wa Twitter wanaharakati wa kutetea haki nchini Tanzania waliungana na wanaharakati wenzao nchini Kenya kushinikiza Mdude Chadema achiliwe huru na watekaji wake au wamrudishe akiwa salama.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiliitisha mkutano na wanahabari na kulaani kitendo hicho na kutoa wito kwa Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

''Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.'' alisema ilisema taarifa ya chama hicho iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Kabla ya kupatikana kwake maafisa wa polisi walikuwa wamekana kuhusika na utekaji wake licha ya ushahidi kuwatposhea kidole cha lawama.

CHADEMA pia kilivitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

''Baada ya kuendelea kupokea na kufanyia kazi taarifa mbalimbali, kuhusu tukio hilo la Mdude, Chama kitazungumza na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhusu suala hili, siku ya Jumatatu, Mei 6, mwaka huu, ili kupaza sauti kubwa dhidi ya tukio hili na mengine ya namna hiyo yanayohusu utekwaji na upotezwaji wa wananchi katika mazingira yenye utata unaoibua maswali yanayotakiwa kujibiwa na mamlaka au vyombo vilivyopewa dhamana ya Kikatiba na kisheria kuhakikisha uhai wa raia ni jukumu namba moja kwa Serikali yoyote iliyoko madarakani.''

Kwa upande wake Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi aliandika maneno haya katika mtando wake wa Twitter

Taarifa za awali kutoka kwa watu waliyoshuhudia tukio hilo zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelelekatika duka la Mdude Chadema, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea ili kutoa msaada, lakini ghafla watu waliokuwa wakimpiga Mdude walitoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu.

Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Ruka X ujumbe, 5

Mwisho wa X ujumbe, 5

Madai ambayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando alikanusha katika mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania

"Mimi ni mkazi wa eneo linalodaiwa kuwa risasi zimepigwa lakini sijasikia na kama unavyojua mji wa Vwawa ni mdogo ambao zikipigwa risasi lazima utasikia," alisema.

Hata hivyo, Kamanda Kyando amesema ataendelea kufuatilia kwa kina zaidi juu ya taarifa hizo.

Baada ya kutekwa kwa Bilionea Mohammed Dewji mweizi Oktoba mwaka jana Waziri wa mambo ya Ndani Tanzania Kangi Lugola alijitokeza na kusema kuwa kuna hofu kwa Watanzania juu ya matukio ya kutekwa na kuongeza kuwa hofu hiyo inabidi iondolewe.

Matukio ya watu kutekwa au kushambuliwa na watu wasiojulikana

  • Mauaji ya Kibiti mwaka 2017: Viongozi wa CCM, askari zaidi ya 10 na wananchi karibu 40 katika eneo la Kibiti walishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana.
  • 11 Februari, 2018 Kiongozi wa Chadema Daniel John alitekwa na kisha aliuwawa kikatili wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni. Mwili wake ulipatikana mnamo 14 Februari.
  • Aprili 2017, Mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzie wawili watekwa na watu wasiojulikana na kuachiwa baada ya siku 3.
  • Mnamo 7 Septemba, 2017, Mnadhimu Mkuu wa upinzani bungeni, mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Area D Mkoani Dodoma. Bw Lissu pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
  • 21 Novemba, 2017 Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communications Limited Azory Gwanda alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa hajapatikana.
  • Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Ben Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Visa 21 vya watu kutekwa viliripotiwa mwaka 2018 na kati ya hivyo watu 17 walipatikana salama.

Hata hivyo kwa miaka ya karibuni nchini Tanzania kutekwa, kuchukuliwa ama kushambuliwa na watu wasiojulikana kumekuwa ni hali ya kutisha.