Bobi Wine na Kizza Besigye waungana kukitimuwa NRM cha rais Museveni Uganda

Chanzo cha picha, ISAAC KASAMANI
Mbunge wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi na mwanaharakati wa kisiasa na mpinzani Dkt Kizza Besigye wameahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.
Chama tawala cha NRM kimekuwa madarakani tangu 1986.
Taarifa ya pamoja imeashiria kwamba baada ya mashauriano kati ya viongozi hao wawili, wamekubaliana kuhusu masuala kadhaa wakati wanapokuja pamoja kushirikiana kisiasa dhidi ya rais Museveni, Daily Monitor linaripoti.
Hapo jana akizungumza na waandishi habari Kyagulanyi maarufua Bobi Wine alisema wamekuwa wakishauriana katika mikutano kadhaa na vyama tofuati vya kisiasa nchini kikiwemo cha Democratic Party maarufu DP bloc na hivi karibuni na kiongozi wa People's government, Dkt Kizza Besigye.
"Tunaungana na vikosi vingine vya kutaka mageuzi, tunajua kwamba kumaliza haya (struggle) mapambano, ni muhimu kwetu kukaa pamoja," amesema Bobi Wine.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Katika mkutano na waandishi habari hii leo wasemaji wa People Power, kundi linaloongozwa na Bobi Wine, Joel Ssenyonyi na Betty Nambooze, msemaji wa 'People's Government' ambayo ni kambi ya Dkt Besigye, wametangaza kwamba pande hizo mbili zitatakeleza shughuli zao za kisiasa kwa pamoja katika kutafuta njia za kumtoa madarakani Rais Museveni.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kiongozi wa upinzani na hasimu mkubwa wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Bw Kizza Besigye amewahi kusema kwamba miaka mingi ya Bw Museveni kusalia madarakani ndiyo chanzo cha ukosefu wa usalama na mauaji ya watu mashuhuri nchini humo, hasa katika mji mkuu Kampala.
Ushirikiano wa Bobi Wine na Besigye una maana gani kwa utawala wa Museveni?

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uganda Tumusime, anasema ushirikiano kati ya Bobi Wine na Kizza Besigye sio tishio kwa serikali ilioko madarakani.
Anaeleza utofuati wa sera na maslahi kati ya viongozi hao wawili ambayo anasema inafanya kuwa vigumu kwa muungano au ushirikiano wa aina hiyo kuwa thabiti.
"Kila mtu ana nia yake, malengo yake, wameamua kukubaliana au kufanya jambo pamoja lakini wakati ukifika wa kusema tuchague mgombea wa muungano wetu, watu wataanza kupata mawazo tofuati," anasema Tumusime.
Ameongeza kwamba ushirikiano huu hauna uzito wowote kwa kutazama pia tofauti na uhasama uliokuwepo katika siku za nyuma kati ya viongozi wa upinzani na wafuasi wa vyama vyao.
Tumusime anakiri kwamba siasa nchini Uganda imebadilika kadri miaka ilivyosogea lakin imaslahi ya kibinafsi ni tatizo linaloendelea kuwepo kati ya viongozi wa kisiasa.
Kizza Besigye ni nani?
Kanali (Mstaafu) Dkt Kizza Besigye Kifeefe alizaliwa mwaka 1956 katika wilaya ya Rukungiri, magharibi mwa Uganda.
Besigye alifuzu kama daktari baada ya kusomea Chuo Kikuu cha Makerere, mjini Kampala.
Alijiunga na chama cha Museveni cha Uganda Patriotic Movement muda mfupi baada ya kuondolewa madarakani kwa Idi Amin 1978.
Mwaka 1982, alijiunga na Museveni vitani baada ya kuzuiliwa miezi miwili katika hoteli moja mjini Kampala akituhumiwa kushirikiana na waasi.
Baada ya Museveni kuingia uongozini, alimteua Dkt Besigye, wakati huo akiwa na umri wa miaka 29, kuwa waziri wa nchi aliyesimamia masuala ya ndani na masuala ya siasa za taifa.
Dkt Besigye alipanda cheo jeshini na kufikia cheo cha kanali.
Alistaafu muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2001, miezi michache kabla ya kujitokeza na kutangaza kwamba angewania urais.

Chanzo cha picha, ISAAC KASAMANI
Alipata asilimia 28 ya kura zilizopigwa akilinganishwa na mshindi, Museveni, aliyepata asilimia 69.
Baada ya kushindwa, Besigye aliwasilisha kesi Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya uchaguzi. Alishindwa kesi hiyo na akakimbilia uhamishoni Afrika Kusini akilalamikia kudhulumiwa kisiasa.
Alirejea Novemba 2005 na kuongoza chama cha FDC kwenye uchaguzi wa februari.
Hata hivyo alikamatwa wiki chache baadaye na kufunguliwa mashtaka kadhaa yakiwemo uhaini na ubakaji.
Aliachiliwa huru wiki mbili baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi.
Besigye husifiwa sana kutokana na moyo anaoonyesha anapotoa hotuba zake na wengi wamemsifu kwa kusimama na kupinga utawala wa Museveni.
Hata hivyo, wakosoaji wake humshutumu wakisema hana uchu wa madaraka na baadhi husema hawezi kufanikisha mabadiliko yoyote kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Museveni.














