Urusi yaishutumu Ukraine baada ya meli yake kuzama katika bahari ya Mediterania

Chanzo cha picha, Serhii Sternenko/X
Meli ya Urusi ya gesi ya kimiminika (LNG) imezama katika bahari ya Mediterania kati ya Libya na Malta baada ya kukumbwa na mlipuko na kuwaka moto, maafisa wa bandari ya Libya wamesema.
Urusi imeishutumu Ukraine kwa kuishambulia Arctic Metagaz kwa "ndege zisizo na rubani" zilizorushwa kutoka pwani ya Libya.
Idara ya usalama ya serikali ya Ukraine SBU haijatoa kauli yoyote kuhusiana na madai hayo huku mamlaka ya bandari ya Libya imesema chanzo cha moto kwenye meli hiyo hakijabainika.
Raia wa Libya wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba takriban tani 62,000 za LNG kabla ya kukumbwa na milipuko na kwamba ilizama takriban maili 130 (240km) kaskazini mwa bandari ya Sirte nchini Libya.
Wizara ya uchukuzi ya Urusi ilisema Warusi 30 walikuwa ndani ya Arctic Metagaz.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Malta Byron Camilleri alisema wote walipatikana wakiwa "salama katika boti ya uoko" wakati wa operesheni ya uokoaji ya vikosi vya jeshi vya Malta.
Picha ambazo hazijathibitishwa zilizoibuka mitandaoni zinaonekana kuonyesha meli hiyo ikiwaka moto baada ya shambulio hilo la Jumanne.
Maelezo zaidi:




