Uhuru Kenyatta: Maafisa watakaohusishwa na ufisadi watatimuliwa serikalini

Unapotajwa katika kesi ya ufisadi na kupelekwa mahakamani utalazimika kuondoka serikalini , amesema rais Uhuru Kenyatta.
''Nitachukua hatua ya kumuondoa afisa yeyote wa serikali atakayekuwa na kesi ya kujibu mbela ya mahakama'', aliongezea.
Akizungumza wakati wa hotuba kwa taifa siku ya Alhamisi Uhuru amesema kuwa amekuwa katika shinikizo ya kuwafuta maafisa wa serikali.
Hakutakuwa na afisa atakeysazwa katika vita dhidi ya ufisadi .
Hatahivyo amesema kuwa serikali itafuata njia za kisheria katika kuwashtaki wahusika.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwisho wa X ujumbe, 2
Ufisadi serikalini
Amesema kuwa vita dhidi ya Ufisadi havitafanywa kupitia pingamizi na taarifa za vyombo vya habari.
"Vitendo vyetu havitakuwa vya shutuma...demokrasia yetu inafuata sheria hivyobasi mchakato wa kuwachukulia hatua wanaofanya makosa ni muhimu katika kutekeleza wajibu huo''.
Mapema Uhuru Kenyatta alifutilia mbali uteuzi wa jaji Joseph Mutava. Hii ni baada ya mahakama ya juu kupendekeza kuondolewa kwake kutokana na uovu aliotenda.
Aidha Amesema kuwa watu matajiri kupitia kiasi ambao maisha yao haiendani na kodi wanayolipa watalazimishwa kusema ni wapi walikotoa fedha ama mali hiyo, alisema katika machapisho yake katika mtandao wa Twitter.
''Haturudi nyuma katika mapambano dhidi ya ufisadi kwasababu tumejitolea kuhakikisha vizazi vijavyo vinarithi Kenya iliyo imara inayoheshimu utawala wa sheria.
Alisema kuwafunga jela au kuwatoza faini watu waliyoba mali ya umma haitoshi, lazima warudishe mali hiyo.
''Suala la uadilifu linatarajiwa kuwa jambo la kawaida siku za usoni'' alisema Bw. Kenyatta.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 4
Rais Kenyatta alisema kuwa hatapunguza kasi yake katika kuafikia malengo hayo mbali na yale ya kuhakikisha kuwa kuna maridhiano ambayo ametaja kuwa swala muhimu wakati alipokutana na kiongozi wa ODM Raila Odinga mnamo tarehe 9 mwezi Machi.
Awataka Wakenya kumuunga mkono katika vita hivyo
Aliwaambia Wakenya wanaopenda nchi yao kwamba lazima wakatae jinamizi hilo ili vita hivyo viweze kufaulu.
Kuhusu lengo la kuunganisha taifa, kufuatia kipindi kirefu cha uchaguzi wa 2017, rais Kenyatta amesema kutakuwa na fursa kwa Wakenya kuzungumzia kuhusu matokeo na mapendekezo yao.
''Nataka kusisitiza maneno niliosema awali kwamba bunge hili litapitisha shilingi bilioni 10 ili kuponya vidonda vya kihistoria ambavyo vimetiliwa sumu na siasa zetu na uhusiano mbaya kati jamii zetu'', alisema.
Kupitia usaidizi wa bunge letu pamoja na jamii zilizoathirika, tutatumia fedha hizo katika kuleta matumaini nchini kupitia ujenzi ,taasisi za urathi na vituo vya habari vya kijamii.